King Kong III
JF-Expert Member
- Oct 15, 2010
- 56,205
- 79,515
ukituma wewe fedha kupitia kwenye simu yako kwenda kwenye simu nyingine, ile tozo tuliyokuwa tunaipigia kelele imefutwa
Huu ni ukweli usiosemwa na hawa wababaishaji. Unaondoa Tozo ya kutuma halafu unadabo Tozo ya kutoa unasema umepunguza makali? Hao waandishi wanaowahoji huwa hawana contents kiasi kwamba hawajui kinachoendelea?Tozo ya kutoa pesa imeongezeka kwa asilimia 50%
Ni mali za watanganyika zinazouzwa na CCM kwa waarabuhizo bandari ni za ukoo wenu?
Wanajua kucheza na akili za watu!Dah π π π π π π π π.
Wanajua ukisha weka pesa kutoa ni lazima.
Nani kakwambia kwamba bandari inauzwa tatizo lako unawasikiliza wapotoshaji ambao watakosa ulaji bandari ikiendeshwa na muwekezaji na wewe unafata mkumbo hupati manufaa yoyote nyinyi ndio mnaoingizwa kwenye matatizo hao kina slaa na lissu wakiona mambo mazito wanakuwa cheni na wanakumbilia ulaya walikoziweka familia zao.Kuanzia tarehe 1/7/2023,ilitangazwa kuwa serikali sikivu ya mama imesikia kilio Cha watanzania imeondoa tozo kwenye miamala ya simu,lakini jambo lililofanyika ni usanii tu,tozo zimetolewa kwenye miamala ya kutuma tu lakini kwenye miamala ya kutoa tozo Iko palepale.
Uhalisia uliopo ni watu wachaje sana huweka pesa kwenye simu zao na Kisha kutuma Kwa mtu mwingine,wanafanya hivyo kuepuka gharama za kutuma,wengi wao humpa wakala namba ya simu iliyokusudiwa kutumiwa Hela Kisha wakala anatuma mojakwamoja.
Hivyo serikali imeona miamala hiyo Haina faida kwao imeamua kuondoa tozo,tozo zinazosumbua watu wengi ni za kutoa pesa Kwa wakala ni Si kutuma Kwa mtu mwingine,serikali iache propaganda za kusema wameondoa tozo,tozo Bado ni changamoto.
Nisihamishe mada,suala la kuuza bandari za Tanganyika halikubaliki Kila mtanganyika Hana budi kulipinga Kwa ajiri ya vizazi vijavyo