Gerson Msigwa ya nini unateseka namna hiyo?

Li ngunda ngali

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2023
Posts
707
Reaction score
2,572
Aisee, kama yupo binadamu anayetoa povu la utetezi kwenye hilo la DPW basi ni Gerson!

Unajiuliza, kwa nini anatumia nguvu namna ile? Ya nini jambo linaloonyesha hana japo theluthi ya uelewa kwalo analazimisha kulitetea hali inayopelekea mwisho wa siku anaonekana mburula tu mbele ya welevu?!

Huenda anatetea ugali wake, sawa-lakini, ya nini basi asiwe anaambatana na mwanasheria japo mmoja wa Serikali ili pamoja na yote awe anamsaidia kudadavua baadhi ya mambo yahusuyo sheria?

Gerson, punguza kujipendekeza basi, unajianika!
 
Yaaaani wewe ulitegemea mshahara wa Bi Mkubwa uende bure bure tuu?

Mathematically:

Product = input! (no waste products!!!)
 
Mwachiluwi hata mimi ni mdogo wangu yule, tuliteseka wote kipindi alipokuwa Ruvuma.

Maeneo kama Mpitimbi, Litola, Mtakanini, Mlete, Mletele, Hanga monasteli, Madaba, Mahanje Mission na kwingineko kote huko, tuliambatana wote.

Tatizo, kwenye hilo la BANDARI, ni mweupe. Awaache wenye uelewa kwenye hayo mawanda waliseme.
 
Anajaribu kuleta ufafanuzi mzuri kwenye jamii ila kama anasoma hapa atajua kipi anatakiwa kukifanya au kukiboresha namuamin sana kaka angu anapenda kujifunza kila siku kutoka kwa watu walio mzidi maarifa
 
Aisee, kama yupo binadamu anayetoa povu la utetezi kwenye hilo la DPW basi ni Gerson!

Unajiuliza, kwa nini anatumia nguvu namna ile? Ya nini jambo linaloonyesha hana japo theluthi ya uelewa kwalo analazimisha kulitetea hali inayopelekea mwisho wa siku anaonekana mburula tu mbele ya welevu?!

Huenda anatetea ugali wake, lakini, ya nini basi asiwe anaambatana na mwanasheria japo mmoja wa Serikali ili pamoja na yote awe anamsaidia kudadavua baadhi ya mambo yahusuyo sheria?

Gerson, punguza kujipendekeza basi, unajianika!
Na kwa bahati mbaya, jambo lolote usilolijua, kwa jinsi unavyozidi kulitetea au kulielezea, ndivyo unavyozidi kuonekana ni kwa kiasi gani hulijui jambo hilo..!!
 
Mwachiluwi anapenda kutoa ufafanuzi sawa lakini kwenye hilo la BANDARI ufafanuzi haumpendi!

Kwa faida yake, siku nyingine akitaka kulitolea ufafanuzi aambatane na mwanasheria wa Serikali ili endapo kutatokea ukakasi kwenye hayo mawanda, asaidiwe na mtaaluma.

Vinginevyo, atazidi kujiharibia tu.
 
Yuko chini ya taasisi ya urais , kwa maana nyingine ni msemaji wa rais pia , lazima umsaidie boss wako pale anapokata pumzi ya kusema.

Yuko sahihi kwa anachokifanya japo ufafanuzi ndo unamkataa .
 
Mwachiluwi anapenda kutoa ufafanuzi sawa lakini kwenye hilo la BANDARI ufafanuzi haumpendi!

Kwa faida yake, siku nyingine akitaka kulitolea ufafanuzi aambatane na mwanasheria wa Serikali ili endapo kutatokea ukakasi kwenye hayo mawanda, asaidiwe na mtaaluma.

Vinginevyo, atazidi kujiharibia tu.
Amesikia kaka mkubwa
 
Msigwa ana kazi ngumu sana, anajua kabisa maswali ya msingi kuhusu ule mkataba hawezi kuyajibu, hivyo hakuna mwenye kuhangaika nae, ajabu yeye anaendelea kupiga kelele tu, ilimradi mwisho wa mwezi alipwe mshahara!.
 
Aisee, kama yupo binadamu anayetoa povu la utetezi kwenye hilo la DPW basi ni Gerson!

Unajiuliza, kwa nini anatumia nguvu namna ile? Ya nini jambo linaloonyesha hana japo theluthi ya uelewa kwalo analazimisha kulitetea hali inayopelekea mwisho wa siku anaonekana mburula tu mbele ya welevu?!

Huenda anatetea ugali wake, lakini, ya nini basi asiwe anaambatana na mwanasheria japo mmoja wa Serikali ili pamoja na yote awe anamsaidia kudadavua baadhi ya mambo yahusuyo sheria?

Gerson, punguza kujipendekeza basi, unajianika!
Hawa ndio wote wanaosema Dubai ni nchi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom