Gerson Msigwa: Zaidi ya 80% ya taarifa za utekaji hazina ukweli

Mtoa Taarifa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2024
Posts
213
Reaction score
671
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema matukio yanayoripotiwa Polisi kuhusu utekaji nchini mengi yanabainika kuwa ni ya uongo.

"Kuna matukio yanatangazwa kwenye mitandao na vyombo vya Habari mtu katekwa, nataka nikwambie katika matukio yote yaliyoripotiwa polisi kwa mfano, zaidi ya asilimia 80 au 90 mpaka sasa, imethibitishwa kwamba hawakutekwa. [..] Sio kila mtu ambaye haonekani ametekwa." -

Your browser is not able to display this video.
 

Ule uchunguzi wa haraka wa Ali Kibao hakutia neno?

Cc Tlaatlaah, Lucas Mwashambwa hadi hapo mnasimama naye machozi yakiwabubujika?
 
kwa hiyo 10% ni ya kweli. Basi hiyo asilimia kumi ielezwe ni kina nani wanafanya utekaji
 
Huyu a anaonges porojo tu, amtafute Emmanuel Joseph Kisaju kupata ukweli wa kuteka na kuua
 
Asilimia 80 au 90?

Yeye mwenyewe mbona kama hana uhakika?
 
Enhe hiyo 10% ya waliotekwa Serikali imechukua hatua gani kukomesha?
 
Mmmhh!
Is it?
Namshauri Gerson Msigwa bora akae kimya, asipende kujihusisha na masuala tata na magumu kama haya ya watu kutekwa, kuteswa na kisha kuuawa. Anyamaze kimya ili kulinda usalama wake na wa familia yake sambamba na kulinda heshima yake. Haya mambo anayojaribu kuyaelezea ni mazito sana, yapo nje ya uwezo wake.
 
Kwa nini anasema 80% AU 90%?
Kwa sababu hana uhakika ila yupo sahihi kuwa si kila anayesemwa katekwa katekwa. Hata hivyo 10% inatosha kuwafanya watendaji wa serikali wawajibike. Hata kwa tukio la yule mzee wetu tu kutekwa kwenye basi mchana kweupe na kuuwawa kisha kutupwa.
 
Kwa data ipi as evidence
 
Dah!
 
Nasikia hii inaitwa kujitoa ufahamu, kujizima data au kujilipua. Zamani tuliita kujifanya hamnazo. Ila duuuh I'm.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…