Katibu mkuu wa CCM awe
I) Mwenye uwezo mkubwa wa kujenga na kutetea hoja Kwa sababu mwaka huu na ujao ni wakati wa kupanda majukwaani kutetea hoja za Kwa nini kitu Fulani kipo namna Fulani.
2. Mwenye sifa njema za kimaadili zinazokubalika na zisizotiliwa shaka na uadilifu wake uwe ni taswira ya kung'aa Kwa jamii.
3. Asiwe mtu wa makundi au muumini wa kundi lolote maana ana jukumu la kukiunganisha chama.
4. Ni mwenye kuzifahamu siasa za Chama Cha Mapinduzi na mwenye upeo na uelewa mkubwa wa siasa za nchi yetu Kwa sababu mara nyingine atakiwalisha chama kwenye mikutano ya kimataifa.
5. Mwenye kuuishi ujamaa Kwa vitendo na muumini wa siasa za ujamaa na kujitegemea.
6. Awe na uzoefu wa kutosha na mwenye kukielewa chama na angalau awe amewahi kuwa mtumishi ndani ya Chama.
Nina Imani Dkt. Samia atatuletea mtu mwenye sifa hizi