Gesi Asilia Iliyoshindiliwa (CNG) Ndiyo Mwarobaini wa Bei ya Mafuta Tanzania

Gesi Asilia Iliyoshindiliwa (CNG) Ndiyo Mwarobaini wa Bei ya Mafuta Tanzania

Dunia nzima sijawai ona gari ya gas ila naona gari ya umeme na
Mafundi wa bongo wanaobadilisha gar ya mafuta kitumia mfumo wa gas weng ni matapeli na wanaharibu na kupunguza uwezo wa gari

Bora nijipange kununua Hybrid mafuta nanusa tu 1 litre natembea 25km
 
Kiukweli gesi bado haijatufaidisha kabisa, gesi ya kupikia tuu Kila siku inazidi kupanda kana kwamba tunaitoa South Africa
 
Unadhani waarabu wanapenda mafuta yao yadode?
Huyo mmarekani nae lao moja.
Sema Nini serikali itupe kozi vijana ya kujifunza kufunga hiyo gesi.
ADA KUBWA
 
Naomba mamlaka husika za juu hili swala la ufungaji wa gesi asilia kwenye vyombo vya moto ufatiliwe, kuna mbung'i linapigwa kimya kimya bila ya wengi kufahamu, haiwezakani vifaa vya kufungia viwe ghali sana na hata kupatikana kwake ni mtiti.
 
Naomba mamlaka husika za juu hili swala la ufungaji wa gesi asilia kwenye vyombo vya moto ufatiliwe,kuna mbung'i linapigwa kimya kimya bila ya wengi kufahamu, haiwezakani vifaa vya kufungia viwe ghali sana na hata kupatikana kwake ni mtiti.
Ahsante kwa ushauri wako boss, hili litafanyiwa kazi.
 

Tanzania inakadiriwa kuwa na mita trilioni 230 za ujazo za gesi asilia, ingawa zilizothibitishwa mpaka sasa ni futi trilioni 57.5, hivyo kuiweka kwenye ramani ya dunia ikishika nafasi ya 82.

Gesi hiyo tayari imeanza kuzalishwa katika visiwa vya Songosongo wilayani Kilwa, mkoani Pwani na eneo la Msimbati mkoani Mtwara, ikitumika kuzalisha umeme na kuendesha mitambo ya baadhi ya viwanda nchini.

Pamoja na wingi wa hazina ya gesi hii muhimu, kwa kiasi kikubwa Tanzania bado inategemea mafuta kuendesha mitambo ya viwanda vyake pamoja na magari ya mizigo na abiria na pia baadhi ya majenereta ya kuzalisha umeme unaosambazwa na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).

Uhalisia wa hali ukiwa hivyo, Shirika la Petroli Tanzania (TPDC) kwa upande wake lina mkakati wa kuanzisha vituo vya kujaza gesi kwenye magari yaliyoongezewa mfumo unaotumia gesi.

Bei ya mafuta imeathiriwa sana na vita vya Russia na Ukraine vinavyoendelea. Mafuta yalipanda bei na jinsi yalivyopanda, bidhaa nazo zilipanda bei na nauli zilipanda. Thamani ya vitu vingi ilionekana kupanda bei kwa sababu mafuta yalipanda.

Hivyo gesi hiyo ndiyo suluhisho la tatizo la mafuta nchini. Kwa wastani kg 1 ya CNG inakufikisha km 15 wakati lita 1 ya petroli inakufikisha km 10. Lakini pia unaokoa 33.5% ya gharama unapotumia CNG hata kama bei ya CNG ni sawa na ya petroli.


Julai 2020, TPDC, ilisema Sh28 bilioni zilitengwa kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya kujaza gesi kwenye magari. Vituo vya CNG vinatarajiwa kujengwa katika kituo cha mabasi yaendayo haraka kilichopo Ubungo, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na pembezoni mwa Barabara ya Sam Nujoma na vituo vidogo vya kupokelea na kusambaza gesi asilia vingejengwa Soko la Samaki Feri, Hospitali ya Taifa Muhimbili na katika kiwanda cha dawa cha Kampuni ya Kairuki Pharmaceutical kilichopo Zegeleni mjini Kibaha.

Hivyo kutokana na hilo, uelewa wa umma juu ya matumizi ya gesi asilia unapaswa kuongezwa ili kuikomboa nchi kutokana na matatizo ya kupanda kwa bei ya mafuta duniani.

Na hilo ndilo ninalolifanya sasa kuhakikisha Tanzania inaelewa umuhimu wa kutumia gesi asilia iliyoshindiliwa kama nishati kwenye magari kwa kuendelea kuandika makala kwenye mitandao ya kijamii.

Hivyo kubadilisha magari ya Tanzania ili yatumie vyanzo mbalimbali vya nishati imekuwa ikiongezeka kila siku. Watanzania wengi zaidi wabadilishe magari yao yatumie gesi asilia ili wanufaike na maliasili nono zinazopatikana katika taifa letu.


Songosongo Kilwa Mkoani Pwani? Are you serious?
 
Back
Top Bottom