Get Rich or Die Tryin: Niliyoyapitia katika ukuaji wangu

Get Rich or Die Tryin: Niliyoyapitia katika ukuaji wangu

Sema mkuu majukumu mengi
Mda mwingi nipo kwenye gari nawapeleka wazungu porini
Ukishakuwa ndani ya mbuga simu un aweka mode ya ndege ili kuepusha kusumbua wanyama:
Sasa narudi jioni nikiwa nimechoka sana
Sena leo nitaendeleza kwa kirefu
Aaah sawa mkuu wa kambi
 
Sema mkuu majukumu mengi
Mda mwingi nipo kwenye gari nawapeleka wazungu porini
Ukishakuwa ndani ya mbuga simu un aweka mode ya ndege ili kuepusha kusumbua wanyama:
Sasa narudi jioni nikiwa nimechoka sana
Sena leo nitaendeleza kwa kirefu
Una majukumu mengi
 
MI huwaga siangalii series huwa naangalia full movie masaa 2-3 nmeshamaliza

na kwanini mtu ukishajiona umetulia uandike story yako vzr kwa urefu yaan mtu unaandika hata hutumii nusu saa unatumia dk 15 tu useme itaendelea kweLi
Uandishi unapaswa utulize akili na mawazo ili kueleza na kuandika kwa weledi mkubwa,

Zipo story ambazo unaweza kuandika kwa DK 15,
Na zipo zingine unaandika kwa masaa 3 kwa kufikiria na kutumia akili kubwa,,..

Ndy sababu ya kuandika inaendelea ili upate nafasi ya kupumzika na kupata wasaa wa kufikiria Zaidi.
 
SEHEMU YA TISA:=.......
BASI baada ya kuajiriwa na leopard rours shida ikaanzia hapo,ghafla nikaanza kufilisika kazi nikasimamishwa,ile hiace niliyonunua ikapata ajali,mpaka saSa hivi ipo pale central imeshikiliwa,kwangu na kwa familia mambo yakawa magumu,dingi akafariki daah nilipata majanga sana.

Huwezi amini nikaanza kuwa mlevi,ni kawa boda boda mtaani tena namtafutia mtu hesabu nilifikisika manzima,afya ikadorora kwa unywaji wa pombe,bangi ndo ikawa chakula kwangu toka asubuhi mpaka jioni navuta bangi tu mpaka mdomo ukawa mweusi kama wa kunguru,macho mekundu yani ulikuwa ukinitizama unajua huyu mvutaji bangi.

Kipindi hicho zile pombe ya vijogoo na banana ndo imepamba moto,nikawa mlevi sana,mama kila kukicha akawa analia tu,wife akarudi kwao watoto tayari washakuwa na umri wa kwenda chekechea sina kitu chochote.

Nikauza vitu vyote vya ndani,nikawa na lala chini,nguo sibadilishi wala siogi hata week 2 zinaisha,mvua ikininyeshea ndo tayari nimeoga.

Nilikuwa siamini uchawi kama upo,toka nikiwa mtoto sijawahi kuamini ila nikaanza kuamini nimerogwa,usiku silali nanyongwa nikaanza kukimbia nyumba na kulala club za gongo,siku nyingine mtaroni popote pale nilikuwa nalala.

Watu wakawa wananicheka nimefulia,madharau mtu hujamchokoza anakupiga makofi bila sababu kweli hali kwangu ilikuwa mbaya,ndugu wakaanza kugombania mali halizoacha baba,ikawa vita juu ya vita.

Siwezi kuamini siku napata taarifa ya msiba kuwa kaka zangu wawili wamepata ajali ya pikipiki ngurero nawamekufa hapo hapo,aisee nililia sana,basi tukafanya msiba tukawapumzisha kaburini.

Tatizo likaja nyumba zile waliojenga kaka zangu hati waliwakabizi wake zao,wakazingangania kuwa nizao basi tukaona tuwaachie.

Ndugu upande wa baba wakagombania mali za kaka yao,ikawa uchawi live unaona bila chenga,mara kwenye mpaka wa shamba unakuta sanda,nazi zimevunjwa yani ikawa tabu juu ya tabu.

Mali za baba zikagawanywa ndugu wakachukua zote mama akabaki na room 3 tu tena za udongo,wewe sikia ndugu tu yani hakuna watu wabaya kama ndugu..
Kipindi hicho nadharaulika sisikikizwi tena kwenye kikao cha familia sikuruhusiwa kuingia ndani waliniita mlevi sina point ya kutoa daah haya maisha yasikiye tu..

Boda boda nayo akapewa mtu,nikawa sina kazi yeyote ile yani nikawa mweupe ile room 4 zangu zikaanza kupasuka ukutani,ukuta wa nyuma ukaanguka,zile bati nikauza zote ela niliyopewa nikalowea pombe yote.

Yani sijui nikumbiaje,akili ilifungwa manzima nikawa nafikiria pombe na bangi mda wote,chakula nilikiona sumu hali ikazidi kuwa mbaya,aisee nilikuwa nimekufa nikiwa bado hai..

Huwezi kuamini kama ndo yule niliyekuwa na hiace,familia bora mtu yeyote alipokuwa anahadithiwa maisha yangu ya zamani yalivyokuwa manzuri aligoma kuwa sio mimi.

Aisee itaendeleeea.....
Haya maisha haya anajua MUNGU tu...
Hii imenihuzunisha sana. Mungu akutie nguvu bro. Duniani shida ji nyingi sana.
 
Mwamba kaandika yalio msibu
Kwetu sisi ni funzo hapo kwa hapo ni burudani maana tuna enjoy hadithi ya mangi shangali.
Kama ukiona mpwayungu kachangia uzi wa mtu kwa heshima juu huo uzi umemkosha.
Sasa huyu dogo analeta mzaha tu. Dunia ni ngumu sana na hii imenifundisha kutomdharau wala mcheka mtu maishani mwangu.
 
Wewe jamaa unatabia za kishoga
Mwanaume tumeumbwa roho nzuri
Unatabia za kike,sasa unafurahia mangi shingali kupigwa banned.
Acha tabia za kishoga
Akitamkacho mtu ndiyo akifanyacho naamini hizo ulizotaja ndo tabia zako hongera sana
Tahadhali Sinunui wanaume wenzangu Nina mke mzuri tu home
 
Natumaini wote wazima humu,japo changamoto zipo ila tunatakiwa tukomaye nazo maana haina jinsi:

Hizo changamoto tumeumbiwa sisi binadamu,hata uende wapi zipo pale zinakusubiri.

Nimependezewa niwaletee niliyoyapitia katika ukuaji wangu mpaka nilipofikisha 20s,najua utajifunza moja au lingine.

Mangi shangali..
ARUSHA,TANZANIA.

YAFUATAYO YANAFURAHISHA..

UTANGULIZI:-
NIlizaliwa katika hospital ya mount meru iliyopo katika jiji la arusha.kipindi hicho baba alikuwa anafanya kazi katika benki ya nbc,mama alikuwa mfanya biashara soko kuu arusha kipindi hicho soko lilikuwa linaitwa soko la bondeni kitambo hicho..

Katika ukuaji wangu na story nilizopewa na wazazi wangu pamoja na ndugu zangu waliokuwa nami nilipokuwa mtoto.

Mama anasema nilikuwa mtundu sana tena ujeuri,nilipokuwa na miaka 4 nilikuwa najifungia kwenye friji,kwa watu wanajua yale mafriji ya zamani yalikuwa makubwa sana sasa nilikuwa naingia ndani,nakujifungia humo mama ananitafuta kumbe nipo ndani ilikuwa tafurani sana.

Mama anasema nilikuwa nashika kiwembe najikata mwenyewe mkononi na hata sitoi chozi,nilikuwa na matukio ya hatari kuna siku nilichomeka pasi mkutani nikipigwa na shoti nikazimia kwa masaa 6 watu walijua nimekufa.

Tulikuwa na mtindo wa kudandia gari kwa nyuma, lilechuma lakupanda lilikuwa limeoza kuwa kutu silikakatika bana niliburuzwa mpaka ngozi kwenye tumbo zikatoka.

Aisee ngoja nifupishe maana nilikuwa na matukio ya hatari sana ambayo kama sio kudra za mwenyenzi MUNGU nisingekuwa hai leo hii..

Nilipofikisha umri wa kwenda darasa la kwanza nilijiunga katika shule ya sanawary iliyepo arusha,nilisoma vinzuri mpaka kufika darasa la 4 ndio tatizo lilianza maana nilikuwa ujeuri shuleni na mkorofi,wanafunzi niliyesoma nao kipindi hicho walipata joto ya jiwe maana nilikuwa sionewi ovyo,nilikuwa napigana na walionizidi darasa tena la saba.

Shule tulikuwa na tabia ya kupigana
Tunaenda mtoni huko hakuna watu,natafutiwa mbabe wanaomuona ubabe wao natembeza kichapo heavy nikawa naogopeka shule nzima mpaka vijana wa darasa la Saba waliniwazia maana nishawatandika wababe wao .walimu walipata tabu nilipogoma kusoma hakuna mwalimu alithubutu kunichapa nilipochelewa namba na usafi sikupe ratiba yeyote ya usafi darasani.

Niliingia shule mda walimu wanaingia tena mikono mfukoni,nilikuwa mkorofi ila darasani sikuwahi kushuka chini ya mtu wa 5,matokeo ya mitihani nilifanya vyema.

Itaendeleea...

Hakuna mwanafunzi anayeshindikana na walimu, na aendelee kukaa Shule, shule yenye sanawari?

1183de440afe15d9e92e13217df69bcc.gif
 
Back
Top Bottom