Get Rich or Die Tryin: Niliyoyapitia katika ukuaji wangu

Get Rich or Die Tryin: Niliyoyapitia katika ukuaji wangu

Daah kwenye mungi hapo story inafanya nisiipende any way story ya kweli wengine mungu hawawasaidii.
 
Yote niliyoyaandika zilikuwa utangulizi sasa story lenyewe niliyokusudia linaanza hivi:...

Sehemu ya kwanza:=...

Tamaa za fedha zilijaa akilini mwangu,kipindi hicho nilikuwa darasa la 7 ndo namaliza ila kiumbo mimi ni mrefu nilijiona nimekuwa tayari hata shule sikupenda sana,ebu fikiria ndugu darasani akili zimo ila shule sitaki kabisa,nawaona kaka wanakula bata na mapikipiki wamependeza na maviatu ya gharama kubwa kipindi kile ukivaa kiatu cha cat,timberland ma makoti ya leather unaonekana wewe mjanja hiyo na zungumzia 2004.

Nilipomaliza darasa la Saba tu niliwaambia wazazi naenda kutafuta pesa mgodini aisee hilo jambo lilikuwa kubwa sana kwa wazazi,ndugu walinishauri sana ila sikuwasikia nilipowaona kaka zangu walioniachia ziwa wanapesa za maana tena wakiwa na miaka 24 bado wadogo nilipatwa na tamaa la ajabu sana..

Wazazi hawakuwa nala kufanya walinipa baraka zote mwanangu nenda kapambane:nikiwa na miaka 15 kwa mara ya kwanza naingia merelani hiyo mgodini dingi na maisha ya kule sio ya kitoto.unaambiwa hivi mgodini na bandarini ndo kazi za hatari zenye kuogopesha,ila siku ogopa chochote.

Kwa mara ya kwanza naingia merelani simanjiro nikiwa juu ya pikipiki cc 250 la brother nikiwa na miaka 15 tuu sio powah arifu


Itaendeleeaaa...
Ndio Kuna Uzi wangu niliwahi kupost wa Sitosahau Wema alionitendea Mungu Mimi nilifika point ya Mwishohuna kazi +stress za mapenzi nikamuomba Mungu Aniue au aniondolee Matatizo [emoji16]ni ndani ya Usiku mmoja niliamka usiku nikalia sana Kwa kuomboleza kukuuuu sijawahi jiachia nikalia Kwa uchungu mbele za Mungu ....naona Mungu mwenyewe Machozi yalimlenga lenga[emoji1][emoji1]Asubuhi jicho likiwa limevimba nikapokea simu Moja ikabadili Kila kitu.....Sasa kwenye comments mtu anakuandikia Kwamba ni chai......yaani unabami unashangaaa uandike chai Ili iweje chai yenyewe hujadanganya una Range Sport[emoji854][emoji16]hahaaaaa....tuheshimu muda wa mtu kujitolea kuandika....na kama ni chai acha usisome.....nyuzi ni nyingi mno [emoji120]
Mkuu leta link ya Uzi wako... Hizi shuhuda kuna la kujifunza
 
Mkuu mbona series mnaangalia?

Hivi mnadhani uandishi ni Sawa na kuhamisha kabati?
MI huwaga siangalii series huwa naangalia full movie masaa 2-3 nmeshamaliza

na kwanini mtu ukishajiona umetulia uandike story yako vzr kwa urefu yaan mtu unaandika hata hutumii nusu saa unatumia dk 15 tu useme itaendelea kweLi
 
MI huwaga siangalii series huwa naangalia full movie masaa 2-3 nmeshamaliza

na kwanini mtu ukishajiona umetulia uandike story yako vzr kwa urefu yaan mtu unaandika hata hutumii nusu saa unatumia dk 15 tu useme itaendelea kweLi
Sema mkuu majukumu mengi
Mda mwingi nipo kwenye gari nawapeleka wazungu porini
Ukishakuwa ndani ya mbuga simu un aweka mode ya ndege ili kuepusha kusumbua wanyama:
Sasa narudi jioni nikiwa nimechoka sana
Sena leo nitaendeleza kwa kirefu
 
Back
Top Bottom