Geti la Airport lliivunjwa wakati wananchi wakitaka kumuaga Hayati Magufuli

Geti la Airport lliivunjwa wakati wananchi wakitaka kumuaga Hayati Magufuli

Yale mema na maono yake ni vyema Yaenziwe. pia ina staajabisha sana kuona wale waliokuwa wakikosoa Baadhi ya mambo yake mfano waliosema alimiliki kampuni za kandarasi na kujipa kazi wao wakifanya yaliyosawa wakati Huu naona Hawata kaa salama.

Sanjari na waliokuwa wakimshutumu kwa Ubadhirifu na Ufisadi.

Kwa kuwa Haki inakata pande zote sio moja.

Ni hayo tu.
KAZI zinazoonekana Kwa macho alizofanya Magu zinaonyesha Uzalendo wake juu ya nchi hii.

Kundi Hilo dogo linalohujumu Watanzania wasipige hatua kimaendeleo ndani na nje ya chama, litaondoka tu.

Ni suala la muda.
 
Walikamatwa watu sehemu nyingi Sana. Jiwe afe tena huko aliko
Usilolijua,

Mwili wa Magu umejitenga na Roho tu,

Magufuli halisi hajafa, na Bado anadai KAZI na maono alivyokuwa nayo juu ya nchi yatimie.

Tupo kuhakikisha, Ile Tanzania ya Magufuli inafikiwa.

Tusubiri.
 
Atakumbukwa kwa kazi nzuri ya kuwatanguliza wahuni motoni.

Binafsi nilipenda style yake ya kuwashughulikia wahuni.
KAZI ya kuhakikisha unagawanya raslimali za nchi Ili maskini nao wapate chochote Si KAZI ndogo.

Magu alijua kuwatia moyo maskini wafanye KAZI Kwa bidii Ili kujenga Nchi Yao.
 
Jiwe kishakufa. Tena alikufa kizembe sana. Hata muandike mpk server ya jamiiforums ijae hafufuki.

Acheni uwongo. Watanzania kila Kona ya nchi walitaka kuchinja mbuzi ili kufurahia kifo cha dikteta jiwe lkn polisi wakaanza kuwakamata.
20231112_185139.jpg
 
Salaam, Shalom,

Baada ya tarehe 17 march 2021, Mh Samia Suluhu Hassan kutangaza kifo Cha HAYATI Magufuli, Nchi ilizizima,

Binafsi, nilikuwa naendelea kufuatilia tetesi za kifo hicho baada ya taarifa nyingi kusambaa kutokana na ufinyu wa taarifa sahihi. Ilipothibitishwa taarifa hiyo, simanzi ilianza Rasmi.

Ilipowadia siku ya kusafirisha mwili baada ya kuaga pale uhuru, safari ya kuelekea airport ilianza, mwili ulikuwa unapelekwa Airport Ili uende Zanzibar, Kisha Mwanza, kisha Chato Kwa maziko.


Wananchi sijui waliingiwa na nini, jamani sijui nini kiliwapata vijana wale baada ya kuambiwa kuwa hawaruhusiwi kuingia ndani ya uwanja wa ndege wa Dar Kwa sababu za kiusalama.

Nilichokishuhudia Kwa muda mfupi ni uwanja wa ndege kujaa vijana wengi sana na hakuna aliyeweza kuwazuia, walikuwa wamelivunja gate Kwa sekunde chache Kisha kujaa ndani ya runways za airport na ndani ya uwanja wa ndege!

Kila mahala ulipopitishwa mwili wa HAYATI Magu, wananchi walitaka waone Kwa macho ndipo waamini Kweli Magu ameenda.

Niliona kijana mmoja akikimbiza jeneza lile, na alikiambia Kwa umbali mrefu sana, nilijiuliza Kwa jinsi chato kulivyo mbali, kijana yule asingeweza kufika Kwa kukimbia Kwa miguu. Ni kama aliona, tumaini na Imani alivyokuwa nayo kupitia kwa kiongozi wake linaondoka mbele ya macho yake😪

Nililia Kwa huzuni kuu, ndipo nikajua kuwa KAZI ya mtu Huwa inamfuata na kupaza sauti.

Alipofariki Mwl Nyerere, nilishuhudia vilio vile vya wananchi. Tofauti na msiba wa Mwl Nyerere na Magufuli ni kuwa Magufuli alifariki akiwa madarakani na ndoto alizopanga kuzitimiza hakuwa amekamilisha.

Asikwambie mtu, Nchi kuondolewa na Rais aliyepo madarakani, uchungu na taharuki Kwa wananchi Huwa haielezeki.

Taifa lilivuka salama katika msiba Ule, na hiyo ni Ishara kuwa Mungu anaipenda sana Nchi yetu.

Ahsante Mungu Kwa zawadi ya Rais na HAYATI Magufuli.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Amen
MKuu utaliza watu usiwakumbushe majonzi leo hii mpuuzi mmoja anasimama kwenye mimbari na upara wake kama tako fyoko fyoko!
 
Leo kumbukumbu nyingi mbaya na nzuri zinapita vichwani mwa watanzania. Wapo wanaokumbuka baba zao na kaka zao waliouwawa kinyama katika uongozi wa hayati magufuli, wapo wanaokumbuka nafasi zao walizopoteza baada ya magufuli kufariki, wapo waliopoteza kazi zao wakati wa hayati magufuli nao wana kumbukumbu mbaya, wapo wanaokumbuka kasi ya maendeleo wakati wa awamu ya 5 nao wanaomboleza. Kwahiyo naungana na wewe Tuvumiliane wote ambao kila mmoja anakumbuka alivyoguswa na marehemu iwe kwa ubaya au kwa uzuri.
Rest assured.

Magulification will go on.

Aluta Continua
 
Back
Top Bottom