Ghafla tu Ngara na majimbo mengine yanatetewa yabakie Kagera, sababu ni Kabanga Nickel

Kuna swali la msingi kauliza na hujamjibu..

Kauliza hivii..

Faida ya nickel haiwezi kuonekana mpaka mkoa wa chato uanzishwe?

Itakua vyema kama ukimjibu.
Mkoa wa Chato unatupunguzia safari ya kwenda na kurudi ya kilomita 320 tunapotaka kufuata ofisi za kiserikali Bukoba. Chato ni karibu kuliko Bukoba, naomba umwambie hivyo.
 
Hakuna Taifa litakalovunjika, sana sana kutakuwa na ufanisi unaotokana na ukaribu wa Chato kuliko umbali wa kufika Bukoba.
 
Mnyamahanga ni yule asiyejua kishubi/kihangaza na sio kihaya.
 
Hawa watu ni "mafala" sana. Yani ukiwauliza sababu ya kuunda mkoa mpya wanataja neno Magufuli. Angewaambia sasa wanaume anza kuvaa sidiria hawa wapuuzi wasio na akili wangevaa
Wenyeji wa huko ndio wenye uchungu kuliko waswahili wa humu JF.
 
Wewe Kimla unatuchannya na mwandiko wako. Jamani darasa la Sana muwe mnasoma na ku like tu siyo lazima muandike
 
Hakuna Taifa litakalovunjika, sana sana kutakuwa na ufanisi unaotokana na ukaribu wa Chato kuliko umbali wa kufika Bukoba.
Kufika Bukoba kufanya nini. Kipi watu wa Chato wanakosa watakipata Bukoba?
Na ili wajipatie hicho wanachokosa ni lazima wawe mkoa na kwa kuunganisha maeneo mengine
 
Phillipo Bukililo sijaona uhusiano wa nickel na kuanzisha Mkoa wa Chato. Mimi binafsi nilimuona Magufuli kama mtu mkatili na mbinafsi sana ambaye Tanzania hajawahi kutokea.

Akiwa Waziri wa Ujenzi wakati wa B Mkapa alibasidili ramani ya barabara isipite Biharamulo ila ikapita Chato. Alipokuwa Rais ametumia madaraka yake makubwa kupeleka Kijijini kwao Chato miundombinu mikubwa kama Airport, Referral hospital, TRA, CRDB na Mbuga ya Burigi kwa kutumia raslimali za taifa.

Chochote kinachofanyika kuhalalisha UBADHIRIFU wa Magufuli kwa kuifanya Chato kuwa Mkoa nakiita ni UHAYAWANI.

Ile miundombinu inabidi ibakie hivyo hivyo katika ngazi ya wilaya kama ilivyobakia Gbadolite ya Mobutu Seseseko. Tunataka watu wakibisha kuwa tulikuwa na Rais kichaa na mwizi tuwaonyeshe mfano halisi
 
Wewe Kimla unatuchannya na mwandiko wako. Jamani darasa la Sana muwe mnasoma na ku like tu siyo lazima muandike

Sasa mbona na wewe ni yale yale unamcheka mwenzio nini sasa “unatuchannya” “darasa la Sana” [emoji3][emoji3][emoji3]
 
Jaribu kwanza kuigawa Tabora na Morogoro kwa maana hizo ni kijografia ndo zinahitaji kugawanywa kwa sasa lakini si Kagera.
 
Leo ndio wamekuwa na upendo kwa eneo la mpakani siku zote wakituburuza.

Imefika tamati sasa.
Hujajibu Swali wewe Mfuasi wa Marehemu Dikteta Mwendakuzimu
Faida za Nickel haziwezi kuwa realized Mpaka kuanzisha Mkoa Mpya ?
Any relationship / Dependence ?
 
Hoja yao nyingine ni kwamba hizo wilaya zinazopendekezwa, asilimia kubwa ya wakazi wake ni watu wenye uraia tata, ni watu asilia wa Burundi. Ni kama wanalilia kuwa na nchi,ndaniya nchi.

Haya mambo tusiyatazame juu juu. Oneni yanayotokea kwenye sekta ya uchimbaji mdogo wa madini kutokana na kuwa na Waziri mtusi.
 
Hujajibu Swali wewe Mfuasi wa Marehemu Dikteta Mwendakuzimu
Faida za Nickel haziwezi kuwa realized Mpaka kuanzisha Mkoa Mpya ?
Any relationship / Dependence ?
wanakasikazini mpooo
 
Mawazo ya kizamani. Obama ni mkenya lakini katawala taifa babe duniani. WAHYA tulieni mkoa wa chato upo waja kwa kasi
 
Magu aliwatenda watu wa ngara bukoba huko hawajasahau..angekuepo angepitisha kimabavu sasa hayupo acha watu wajitutumue alaa
 
Mimi kwetu Ngara na ni Mtanzania halisi. Mkoa wa Kagera utakuwa ndani ya mipaka ya Tanzania. Ondoa wasiwasi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…