Ghafla tu Ngara na majimbo mengine yanatetewa yabakie Kagera, sababu ni Kabanga Nickel

Mleta mada uko sahihi sana Tena mno

Kuna maeneo yalionewa sana na kuwa marginalized mno na ndio walionewa watu hopeless ambao hata maendeleo hawana na Hakuna mtu mwenye mpango wa kuoa au kuolewa na mturkana

Kenya maeneo kama Turkana walionewa na kuwa marginalized sana yalipogunduliwa madini na mafuta wakajitia kuleta za kuleta

Waturkana hawakukubali
Sasa hivi bajeti kubwa inaenda huko kujikomba

Magufuli aliliona Hilo kuwa kukomboa eneo maginalized Kama Hilo wapewe mkoa wao madini yalipogunduliwa yawe yao kuleta heshima Kagera na Tanzania kuwa si vizuri ku marginalize mtu one day Mungu aweza mtoa vile vile

Kuna madini kibao yamegunduliwa mikoa marginalized kuanzia Kusini,Dodoma na Singida,na huko na Pemba na nyanda za juu kusini

Naunga mkono uanzishaji mkoa eneo marginalized baada ya madini kugunduliwa na wao wafaidi mirahaba nk

Mleta mada analysis yako imeenda shule hasa.Naunga mkono hoja
 
Hujajibu Swali wewe Mfuasi wa Marehemu Dikteta Mwendakuzimu
Faida za Nickel haziwezi kuwa realized Mpaka kuanzisha Mkoa Mpya ?
Any relationship / Dependence ?
Washangae jamaa zetu ambao upendo umewazidi siku za karibuni baada ya kugunduliwa kwa Nickel huko Kabanga.

Kuna suala zima la urasimu wa Bukoba ambao miaka na miaka unabakia kuwa ni mji wakati Tanga imeshakua ni jiji tayari.
 
kwanini mtu wa bukoba amusemee mtu wa Biharamulo au ngara?kwanini wabunge wa ngara na biaharamulo wamepewa million 69 kila mmoja ili waunge kubaki bukoba..je kunanini nyuma ya lesa hizo..ndo tunahoji
Hao wabunge uchaguzi ujao kila mwana ngara na biharamulo ahakikishe hapati kura hata moja ndani ya vikao vya CCM na hata akipitishwa asipewe kura hata moja

Na waelezwe wazi Kama wangechukua pesa kupinga kwamba hizo ndizo kiinua mgongo Chao kichafu wasithubutu kuleta sura zao kugombea 2025 wahamie Bukoba
 
Magu alikuwa na akili sana, aliona ukanda ule upo marginalized sana akaanza kwa nguvu ujenzi wa barabara za Kigoma ili pafunguke.

Nickel ikianza kuchimbwa kule kutazidi kufunguka. Ubaguzi upo kuanzia Ngara penyewe, wabunge wote siku zote ni lazima watoke tarafa ya Bugufi ambapo ni wahangaza, sisi washubi wa bushubi akijitokeza mgombea atapigwa vita vya chini kwa chini ili aukose ubunge.

Hali imekuwa ni hivyo kwa mkoa mzima wa Kagera, kuna watu wa tabaka la juu la kati na la chini, ndani ya mkoa mmoja.
 
Safari hi Ngara na Biharamulo wananchi lazima kuwa kitu kimoja bila kujali itikadi za vyama mkoa upatikane

Marginalization haiwezi endelea forever .Wanaona madini yamegunduliwa wanaanza kuleta za kuleta .Mwana Biharamulo na Ngara popote ulipo join hands hao wabunge 2025 piga chini wote asipeleke pua yake Ngara au Biharamulo kugombea apewe sifuri kila eneo
 
Mimi kama mkazi na mwekezaji wa Ngara napingana na mawazo ya huu mkoa mpya, kwa sababu kinachotafutwa ni pesa za umeme rusumo, pesa za border, pesa za kabanga nickel ziende kuendeleza chato isiyo na mapato....
Ngara ibaki wilaya ndani ya kagera kwani hakuna tunachopungukiwa hadi sasa...
 
Nchi hii imejaa wapuuzi sana mkuu. Watu tuliowatanguliza mbele ni hovyo tu. Yaani mikoa mikubwa kabisa imeachwa wanaenda kulazimisha kitu kwa ajili ya kumfurahisha mtu
Haipo nia ya kumfurahisha aliyetangulia mbele ya haki. Siasa za kanda ya ziwa nadhani huzifahamu, uliza upewe mwanga kabla hujachangia.
 
Kijiografia Bukoba ni mbali kuliko Ngara kulinganisha na Chato. Pia kuna hii jitihada ya wabunge wa Kagera kuanzisha upendo baada ya kuona mgodi wa Nickel upo tayari, na yenyewe inatia shaka.

Kuna ubaguzi ndani ya mkoa wa Kagera, kuna ile hali ya mwenye nacho kutaka abaki nacho na asiyenacho hata kidogo alichonacho akipoteze.
 
Kuitenganisha Ngara na Bukoba ni sehemu ya utaratibu wa kitaasisi wenye tija kubwa kwa wananchi wa eneo husika.
maslahi mapana yapi. kwani Chato inakosa nini Geita. uchoyo ndio unawafanya mnahaha. Kwani hatujui kama huyo dikteta alikuwa anapokonya vitu anapeleka Chato?
 
Wewe kinachokuuma ni nini? Au tauapungukiwa nini mkoa wa chato ukianzishwa na makao makuu yake yakawa chato.?

#MaendeleoHayanaChama
Chato kuwa mkoa inalazimishwa tu Wala hakuna any substantial reasons zaidi ya ubinafsi. Kama unabisha nenda kashangae traffic light sehemu iliyojaa mikokoteni, Ni ajabu na kweli. Baba wa taifa angekuwa mbinafsi nadhani Butiama ungekuwa zaidi ya majiji yote ya nchi hii.
 
Mnyamahanga ni yule asiyejua kishubi/kihangaza na sio kihaya.
We jamaa kusema ukweli umeathirika na inferiority complex hakuna point yoyote hapa. Kama point yako Ni umbali kwenda makao makuu ya Mikia, kwa taarifa zipo sehemu unasafiri umbali zaidi ya huo uliohutaja kwenda mkoani, na hao wasemeje? Tuseme ukwelikuna mamba Hayati Magufuli aliyaasisi kwa personal interest na si public interest. Naomba Madam President Samia S. Hassan apige chini mambo yote yasiyo natija aliyoanzisha Mtangulixi wake.
 
maslahi mapana yapi. kwani Chato inakosa nini Geita. uchoyo ndio unawafanya mnahaha. Kwani hatujui kama huyo dikteta alikuwa anapokonya vitu anapeleka Chato?
Wewe sio mwenyeji wa kanda hiyo kwa maandishi yako tu. Unachangia mada ukiwa na hayati akilini kwako!.
 
Wewe huna maslahi na kanda au mkoa wa za Kagera. Sisi wenye mkoa ndio wenye uchungu.
 
Hivi kila patakapokuwa na uzalishaji wa kitu fulani basi mkoa uanzishwe? Vigezo vya kuanzisha mkoa vinajulikana si kwa ajili ya Nickel. Ingekuwa hicho ni kigezo basi Tunduru wangedai mkoa walipogundua Alexandrite au Songosongo na Mnazi Bay etc nao wangeomba iwe mikoa. Hili la kuanzishwa mkoa wa Chato ni la kisiasa zaidi kuliko uhalisia. Mkoa kama Tabora ambao ni mkubwa kwa eneo mbona hatujasikia baadhi ya wilaya kutaka zigawanywe ili kuunda mkoa mwingine? Come out with concrete reasons msifikirie kujitenga kwa sababu ya nickel ambayo imekuwepo tokea zamani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…