Ghafla tu Ngara na majimbo mengine yanatetewa yabakie Kagera, sababu ni Kabanga Nickel

Ghafla tu Ngara na majimbo mengine yanatetewa yabakie Kagera, sababu ni Kabanga Nickel

Faida za hiyo Nickel haziwezi kupatikana bila kuanzisha MkoanMpya ?
Basi angeanzisha nchi Mpya kabisa hapo Chato
Tatizo umesikia neno chato unabaki kuhisi muwasho kweye makalio

Ungesikia kigoma au ngara yenyeqe ungetikisa mkia kama mbwa aliyemuona chui.
Mtabaki na hasira ila ipo siku mtatulia tu kimyakimya na mtaenda vhato kutafuta mahitaji yenu.
 
Ni unafiki wa kiwango cha SGR Muhaya kujifanya anaipenda Ngara wakati siku muhaya anamwita mhangaza mrundi
 
Sasa mbona na wewe ni yale yale unamcheka mwenzio nini sasa “unatuchannya” “darasa la Sana” [emoji3][emoji3][emoji3]
Darasa la Saba, ya kwangu ni 'predictive text" ya smart phone.
 
Kijiografia Bukoba ni mbali kuliko Ngara kulinganisha na Chato. Pia kuna hii jitihada ya wabunge wa Kagera kuanzisha upendo baada ya kuona mgodi wa Nickel upo tayari, na yenyewe inatia shaka.

Kuna ubaguzi ndani ya mkoa wa Kagera, kuna ile hali ya mwenye nacho kutaka abaki nacho na asiyenacho hata kidogo alichonacho akipoteze.
Kwa muktadha huo basi makao makuu ya Mkoa yawe Biharamulo na siyo Chato
 
Tatizo umesikia neno chato unabaki kuhisi muwasho kweye makalio

Ungesikia kigoma au ngara yenyeqe ungetikisa mkia kama mbwa aliyemuona chui.
Mtabaki na hasira ila ipo siku mtatulia tu kimyakimya na mtaenda vhato kutafuta mahitaji yenu.
Yule Marehemu Dikteta Mwendakuzimu angekuwepo angewaamrisha Mvae Bikini na Mngevaa Qmamae zenu
 
Hayati John Magufuli alipambana sana Uzalishaji wa mgodi wa Nickel wa Kabanga Nickel uanze uzalishaji akiwa hai. Mipango ya Mungu huwa ina tofauti na ile ya binadamu.
Hakuweza kuishi mpaka kuona haya yanayoendelea hivi sasa. Angeridhika kwa asilimia mia moja. Utoke jasho kuupigania mradi mkubwa wenye maslahi ya kiuchumi halafu ufanikiwe, na wewe usiwe na sababu ya kugongesha glasi za mvinyo na marafiki zako, hiyo haiwezekani.

Lengo la JPM lilikuwa ni uanzishwaji wa Mkoa mpya unaojumuisha Chato na wilaya zote zilizo karibu. Utajiri wa mradi wa Nickel utauhakikishia mkoa huo mapato ya uhakika. Ndio maana hayati akapigana kadri alivyoweza na alipofariki akaacha hatua za mwishoni za ukamilishaji wa uanzishwaji wa mradi.

Kichekesho ni huu upendo 'mpya' unaoonyeshwa na baadhi ya wabunge ya kuwataka watu wa Ngara wasiunge mkono nia ya kuwa na mkoa watakaokuwa na ushawishi na pengine maendeleo ya kweli. Bukoba ni kilomita 320 kutoka Ngara, ni mbali kulinganisha na Chato.


Wanakuja na utetezi wa kihistoria ambao hauna faida yoyote zaidi ya kuendeleza 'status quo' ya siku zote. Wanataka waendelee na kujikweza na kujitukuza kupitia uwepo wa Bukoba kama makao makuu ya Mkoa wa Kagera. Ni mawazo yale yale ya kuendeleza 'ubwenyenye' ule ule wa miaka yote. Ni aina ya mawazo yeny dharau za kikabila ya kutaka ustaarabu ubakie ule ule wa miaka yote.

Miaka imepita kwa kasi na sasa kama taifa tunaitafuta miaka 60 ya Tanzania. Kama ni mtu tayari keshakuwa mtu mzima, hawezi kuishi kwa kukariri akiongozwa na falsafa zile zile za kale. Baadhi ya mikoa inajikuta ikikumbatia umaskini kwa sababu ya wanasiasa kuamini katika utamaduni ule ule wa siku za nyuma, pasipo kukubaliana na mabadiliko yanayokwenda sambamba na ukuaji wa miaka 60 ya Tanzania.

JPM alipambana mpaka mradi wa Nickel umeanza kazi. Mkoa wa Kagera unahitaji changamoto mpya ili uweze kuondokana na kuongozwa na hulka zile zile zisizoyagusa maisha ya mtu mmoja mmoja. Tuondokane na hizi imani potofu za kisiasa zinazodumaza maendeleo ya ukanda ule. Ni wakati wa baadhi ya watu wa Kagera kuanza kufikiria upya uwepo wa mkoa mpya wenye kila sababu za kisasa za uwepo wake.
Sio sababu kuu, Ila inaweza kuwa moja wapo ya sababu. Lakini hebu tufikirie tena kidogo, kwa sababu huo mkoa utakuwa na idadi kubwa ya wakazi wenye asili ya Rwanda na Burundi ambao walikimbia nchi zao. Je haiwezi kutokea siku moja hawa watu wakataka kujitenga na Tanzania au sehemu yao kuirudisha kwenye moja wapo ya nchi hizo, serikali chini ya vyombo vyake vya usalama nadhani watalichukulia kwa uzito pia suala hili.
 
Kuita watu wanyamahanga sio tusi wala kejeli. That time hakuna mtu anajua dunia ina jamii ngapi na races ngapi, neno mnyamahanga lilimaanisha mtu wa mataifa mengine asiyejua Kihaya wala tamaduni zake.

Wewe ukiita mtu Mchina, Mzungu, Myahudi au Msomali nawe ni mshenzi na mkabila kama Wahaya na una dharau watu kwa kuwa sio kabila lako. Does it make sense?
Ila na kule Kwa gaidi wanasema chasaka badala ya mnyamahanga
 
Phillipo Bukililo sijaona uhusiano wa nickel na kuanzisha Mkoa wa Chato. Mimi binafsi nilimuona Magufuli kama mtu mkatili na mbinafsi sana ambaye Tanzania hajawahi kutokea.

Akiwa Waziri wa Ujenzi wakati wa B Mkapa alibasidili ramani ya barabara isipite Biharamulo ila ikapita Chato. Alipokuwa Rais ametumia madaraka yake makubwa kupeleka Kijijini kwao Chato miundombinu mikubwa kama Airport, Referral hospital, TRA, CRDB na Mbuga ya Burigi kwa kutumia raslimali za taifa.

Chochote kinachofanyika kuhalalisha UBADHIRIFU wa Magufuli kwa kuifanya Chato kuwa Mkoa nakiita ni UHAYAWANI.

Ile miundombinu inabidi ibakie hivyo hivyo katika ngazi ya wilaya kama ilivyobakia Gbadolite ya Mobutu Seseseko. Tunataka watu wakibisha kuwa tulikuwa na Rais kichaa na mwizi tuwaonyeshe mfano halisi
Thanks Tundu
 
Chato kuwa mkoa inalazimishwa tu Wala hakuna any substantial reasons zaidi ya ubinafsi. Kama unabisha nenda kashangae traffic light sehemu iliyojaa mikokoteni, Ni ajabu na kweli. Baba wa taifa angekuwa mbinafsi nadhani Butiama ungekuwa zaidi ya majiji yote ya nchi hii.
Trafiki light sehemu ya mkokoteni ni suala la kawaida. Sijui kama uliwahi kuziona picha za Albania ya miaka ya 1980 wakati punda wakikatiza katikati ya mtaa halafu linganisha na hizi za leo hii uione tofauti kubwa.

Chato ya 2040 ni tofauti na hii ya 2020. Bukoba wamejisahau kwa kuwa makao makuu ya mkoa wa Kagera.
 
Hivi kila patakapokuwa na uzalishaji wa kitu fulani basi mkoa uanzishwe? Vigezo vya kuanzisha mkoa vinajulikana si kwa ajili ya Nickel. Ingekuwa hicho ni kigezo basi Tunduru wangedai mkoa walipogundua Alexandrite au Songosongo na Mnazi Bay etc nao wangeomba iwe mikoa. Hili la kuanzishwa mkoa wa Chato ni la kisiasa zaidi kuliko uhalisia. Mkoa kama Tabora ambao ni mkubwa kwa eneo mbona hatujasikia baadhi ya wilaya kutaka zigawanywe ili kuunda mkoa mwingine? Come out with concrete reasons msifikirie kujitenga kwa sababu ya nickel ambayo imekuwepo tokea zamani
Kagera kuendelea kuishikilia Ngara ni uendelezaji wa mkoa usiokuwa na maendeleo wala tija kwa wakazi wa Ngara na tarafa zake mbili.
 
Back
Top Bottom