Ghalib wa GSM atoa vielelezo kuthibitisha Umiliki wa Kiwanja na Nyumba. Aagiza wanasheria kumchukulia hatua anayepotosha umma

Ghalib wa GSM atoa vielelezo kuthibitisha Umiliki wa Kiwanja na Nyumba. Aagiza wanasheria kumchukulia hatua anayepotosha umma

These are stupid dots.Tuambie unayojua maovu aliyofanya Hayati Magufuli.Hamchoki tu,mnapaka matope hata marehemu!You are so evil.Ni uzuchi tu na kusingizia watu.
 
Leo Wakili Msomi wa Kampuni ya GSM Alex Mgongolwa atafanya mkutano na Waandishi wa habari kuanzia Saa 6 kamili Mchana GSM HQ Salamander Tower Samora Avenue.

====

Hayawi hayawi Yamekuwa...

======

Huu hapa ndio uthibitisho, nimesema ni kielelzo namba moja, mteja wangualiponambia nilichukua hatua aya kwenda kukithibitisha Wizara ya Ardhi na Ardhi walithibisha na hakijapatikana mtaani kimepatikana katika mamlaka ambayo inatambulika.

Ukichukua namba ya kiwanja ukaenda Masjala ya ardhi matokeao yatakuja mmiliki wa kiwanja hiki ni Ghalib Said Muhamed, na ukifikia masjala ya Ardhi ukaonesha kiwanja nmaba ngapi, hati namba ngapi utapata matokeo hayo ambay nimekueleza, hata hao ambao wanaodai kwamba hiki kiwanja ni cha kwao wakienda watapaya matokeao hayo.

Baada ya umilikishwaji huu mteja wangu alidhamiria kufanya maendelezo kwa kuwa alikuwa na nia ya kufanya maendelezo ambayo ni ya kimsingi yana gharama kubwa, aliamua mnamo tarehe 19, 9,2019 kuingia kwenye mkataba wa ujenzi na kampuni ya ujenzi inayoitwa Group 6 Internatinal, na huu ndio mkataba wa ujenzi na unajieleza, kwa hiyo huingii mkataba wa kuendeleza ujenzi kama kiwanja hicho hakipo kwa jina lako, naomba mziangalie hizo tarehe vizuri nitazieleza baadaye kutokana na upotoshaji wa tarehe ambazo kimsingi hazihusiani kabisa na kiwanja hiki.

Kwa kuwa sheria ya nchi hii hazikuruhusu wewe kufanya maendelezo bila kibali, mteja wangu alifata taratibu za kuomba kibali na kibali kilitoka kuwa ana ruhusu ya kufanya maendelezo na kilitoka 16, 10, 2017 na kilitoka kwa jina la Ghalib Said Muhamed, na unapofanya maombi ya kibali lazima mamlaka ijiridhishe kuwa wewe ndie mmiliki na kama jina litakuwa tofauti hutapata kibali. Na kwa kuwa mamlaka ya Ardhi Kinondoni ilijiridhisha na kumpa kibali na Mkandarasi akaanza ujenzi na Mteja wangu alilipa fedha zote na hadaiwi na Mkandarasi na kuna Risiti za TRA ili kuonesha kuwa mteja wangu ndiye mmiliki na alianza kumili kiwanja mwaka 20016. na alifata taratibu zote za kumiliki na kujenga na kwamba ana vibali vyote.

Kwa kumalizia upo upotoshaji wa kidhana mbao sio sahihi kwamba ardhi mnaweza mkamilikishana watu wawili kama mtakavyotata, hii sio sawa na haiko kisheria, kwanza mmliki wa Ardhi ni Rais na sisi tunafanya upangishaji ambao utatajwa muda kama ni miaka 30, 100 nk. Hivyo ili umiliki Ardhi ni lazima mauziano hayo ya ardhi mamlaka ithibishe.

Sisi kama wana sheria, mteja wetu ametuagiza kutoa vielelezo vyote ili kuonesha kuwa yeye ndio mmiliki halali wa ardhi hiyo na kwamba mtu yoyote anayeda kuwa ni mmiliki wa Ardhi hiyo atoe Hadharani vithibitishi vya kisheria vilivyothibitishwa na mamlaka husika kuwa yeye ni mmiliki.

Pili Mteja wangu ametuelekeza kulinda heshima yake ya kibiashara kwa kuchukua hatua za kisheria kwa mtu yoyote ambaye anafanya upotoshaji wwote na sisi tuko tayari kwenda hatua zozote za kisheria na tuna ruksa za kisheria za kuchukua kwa mtu yoyote ambaye anaathiriwa kinyume na sheria kwenda ngazi yoyote ya kisheria ili kuyatetea haya ambayo kimsingi maelekezo halali.

Pia, soma:

Video: Makonda yamkuta makubwa, Ghalib wa GSM adai nyumba yake

Dah akili kubwa imefanya yake
 
Hahah!

Huyu jamaa si juzi tu alikuwa miongoni mwa waombolezaji kwa msiba wa hiyo familia...

Kumbe nyuma ya pazia ni mkwapuaji wa mali za watu...
 
Huyu mwanasheria ni poyoyo, huo ushahidi wa GSM ni wa kubumba maana mwenzake kaleta ushahidi wa tangu 2013. Pamoja na udhaifu wa Makonda hapo Riziwani Kikwete anahusika na hii kitu nawahakikishia itakuja kumgharimu yeye na huyo GSM.
Makonda naona huu usemi wa "bora upoteze hirizi kuliko kufiwa na mganga" sasa hivi unauelewa vizuri sana, rudisha kiwanja hicho acha kelele
 
Inawezekana kutokana na changamoto za awamu ya tano ilibidi kweli GSM wamkabidhi kiwanja Paul Makonda wakakubaliana wa backdate tarehe isomeke 2013 kabla ya Makonda kupata Presidential appointment ambayo inamlazimu ku declare kila mali anayomiliki

Inawezekana pia baada ya JPM kutokuwepo na baada ya kupata baraka za Mamlaka mpya imebidi arudishiwe plot yake

Maana naskia za chinichini wale wote walioporwa mali zao kwa dhulma au kufungwa kwa uhujumu uchumi wanaendelea kuachiwa

Kwanini GSM hataki kueleza mazingira yoyote yaliyosababisha Makonda alazimishe kuwa hicho kiwanja no chake

Kwanini wote Makonda na GSM hawataki kwenda Mahakamani badala yale wote wanashinda kwny mitandao kutulisha story za uongo na kweli

Wote Gharib na Paul kuna ka sehemu muhimu wana ki skip kwny story yao ni sawa na ile story ya Mama Mkwe na Mka mwana kutuhumiana uchawi kwa kuwa walikutana kwa Mgang na kila mmoja hataki ijulikane
 
Inawezekana kutokana na changamoto za awamu ya tano ilibidi kweli GSM wamkabidhi kiwanja Paul Makonda wakakubaliana wa backdate tarehe isomeke 2013 kabla ya Makonda kupata Presidential appointment ambayo inamlazimu ku declare kila mali anayomiliki

Inawezekana pia baada ya JPM kutokuwepo na baada ya kupata baraka za Mamlaka mpya imebidi arudishiwe plot yake

Maana naskia za chinichini wale wote walioporwa mali zao kwa dhulma au kufungwa kwa uhujumu uchumi wanaendelea kuachiwa

Kwanini GSM hataki kueleza mazingira yoyote yaliyosababisha Makonda alazimishe kuwa hicho kiwanja no chake

Kwanini wote Makonda na GSM hawataki kwenda Mahakamani badala yale wote wanashinda kwny mitandao kutulisha story za uongo na kweli
Wewe umeongea pointi. Ndiyo maana ushahidi wa GSM ni wa kubumba
 
Ukweli mchungu ni kuwa GSM alitoa kiwanja kweli kwa bashite kwa makubaliano wanayoyajua wao.
Ila sasa hivi wanakihitaji tena kwa sababu wanazojua wao, Ila mfanikishaji wa haya ni prince wa yule mzee wetu.
Vita vya wanasiasa havina mwisho mzuri. Ila polr yake bashite, prince anamkomalia sana tatizo ni ule uswahiba wake na mama. Bila hivyo pangechimbika zaidi
Wale waswahili huwa hawasamehi, kisasi ni haki kwao.
 
Back
Top Bottom