Ghalib wa GSM atoa vielelezo kuthibitisha Umiliki wa Kiwanja na Nyumba. Aagiza wanasheria kumchukulia hatua anayepotosha umma

Ghalib wa GSM atoa vielelezo kuthibitisha Umiliki wa Kiwanja na Nyumba. Aagiza wanasheria kumchukulia hatua anayepotosha umma

Tena wamemtumia Ridhiwani kama waziri wa wizara ya ardhi.

Ina maana Ridhiwani alipelekwa pale maksudi ili kumkomoa Makonda.

Bila Kikwete hakuna GSM....hawa ndio wale Home Shopping Center.

Walikuwa wakinyanyasa wafanyakazi mbaya kabisa ile enzi ya JK...na sasa wamerudi ulingoni upya.

Ni wahuni kuanzia usitishaji mkataba wa TFF mpaka kufukuza waajiriwa wao wa kihindi usiku kinyemela.

Time....will....tell....
Maksudi amkomoe nane nyie hamna akili na marehem mungu wenu?? Unapora ardhi hati hufuatilii unajua mungu atakuwepo miaka yote watoto wa mjini wamemuonesha picha,hii sasa inaenda kufikua makaburo yote kams mwenzie saabovu!!
 
Bashite na Sabaya sio Maguli na hawakufanya waliyofanya kwa maelekezo ya Magufuli.Pia kumbuka kwamba no President can be everywhere at the same time.Zako Ni accusations za kijinga zinazochangiwa na chuki zinazoambatana na uovu.
Magufuli alijuw anapenda kufanya kazi na watu wenye haiba yake. Yote waliyotenda akina Aanaya, Makonda, Chalamila, Luhaga Mpina, Mnyeti, Mrisho Gambo, yalikuwa na Baraka zake. Alipenda mijitu isiyotumia akili kwa vile mwenyewe alikuwa katili
 
Leo Wakili wa Kampuni ya GSM, Alex Mgongolwa amefanya mkutano na Waandishi wa habari kuanzia Saa 6 kamili Mchana GSM HQ Salamander Tower Samora Avenue.

====

Kilichojiri, full text:

======

Mwanasheria:
Huu hapa ndio uthibitisho, nimesema ni kielelezo namba moja, mteja wangu aliponambia nilichukua hatua aya kwenda kukithibitisha Wizara ya Ardhi nao walithibisha na kithibitisho hiki hakijapatikana mtaani kimepatikana katika mamlaka ambayo inatambulika.

Ukichukua namba ya kiwanja ukaenda Masjala ya ardhi matokeao yatakuja mmiliki wa kiwanja hiki ni Ghalib Said Muhamed, na ukifikia masjala ya Ardhi ukaonesha kiwanja nmaba ngapi, hati namba ngapi utapata matokeo hayo ambay nimekueleza, hata hao ambao wanaodai kwamba hiki kiwanja ni cha kwao wakienda watapata matokeao hayo.

Baada ya umilikishwaji huu, mteja wangu alidhamiria kufanya maendelezo kwa kuwa alikuwa na nia ya kufanya maendelezo ambayo ni ya kimsingi yana gharama kubwa, aliamua mnamo tarehe 19, Septemba 2019 kuingia kwenye mkataba wa ujenzi na kampuni ya ujenzi inayoitwa Group 6 Internatinal, na huu ndio mkataba wa ujenzi na unajieleza. Kwa hiyo huingii mkataba wa kuendeleza ujenzi kama kiwanja hicho hakipo kwa jina lako, naomba mziangalie hizo tarehe vizuri nitazieleza baadaye kutokana na upotoshaji wa tarehe ambazo kimsingi hazihusiani kabisa na kiwanja hiki.

Anaendelea:
Kwa kuwa sheria ya nchi hii hazikuruhusu wewe kufanya maendelezo bila kibali, mteja wangu alifuata taratibu za kuomba kibali na kibali kilitoka kuwa ana ruhusa ya kufanya maendelezo na kilitoka 16, Oktoba 2017 na kilitoka kwa jina la Ghalib Said Muhamed, na unapofanya maombi ya kibali lazima mamlaka ijiridhishe kuwa wewe ndiye mmiliki na kama jina litakuwa tofauti hutapata kibali.

Na kwa kuwa mamlaka ya Ardhi Kinondoni ilijiridhisha na kumpa kibali, Mkandarasi akaanza ujenzi na Mteja wangu alilipa fedha zote na hadaiwi na Mkandarasi na kuna Risiti za TRA ili kuonesha kuwa mteja wangu ndiye mmiliki na alianza kumili kiwanja mwaka 2016, na alifuata taratibu zote za kumiliki na kujenga na kwamba ana vibali vyote.

Anamalizia:
Kwa kumalizia, upo upotoshaji wa kidhana ambao sio sahihi kwamba ardhi mnaweza mkamilikishana watu wawili kama mtakavyotaka. Hii sio sawa na haiko kisheria, kwanza mmliki wa Ardhi ni Rais na sisi tunafanya upangishaji ambao utatajwa muda kama ni miaka 30, 100 nk. Hivyo ili umiliki Ardhi ni lazima mauziano hayo ya ardhi mamlaka ithibitishe.

Sisi kama wanasheria, mteja wetu ametuagiza kutoa vielelezo vyote ili kuonesha kuwa yeye ndio mmiliki halali wa ardhi hiyo na kwamba mtu yeyote anayedai kuwa ni mmiliki wa Ardhi hiyo atoe hadharani vithibitisho vya kisheria vilivyothibitishwa na mamlaka husika kuwa yeye ni mmiliki.

Pili, Mteja wangu ametuelekeza kulinda heshima yake ya kibiashara kwa kuchukua hatua za kisheria kwa mtu yeyote anayefanya upotoshaji wowote.

Pia, soma: Video: Makonda yamkuta makubwa, Ghalib wa GSM adai nyumba yake

KATIKA HABARI:

MFANYABISHARA Ghalib Said Mohamed maarufu GSM, ametoa vielelezo kadhaa vinavyoonesha kuhusika katika umiliki wa eneo lenye mgogoro baina yake na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya kusambaa kwa video ambayo Makonda alionekana akidai kuwa eneo hilo ni la kwake huku akiwa amezingirwa na watu akiwemo askari aliyevalia sare za jeshi la polisi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi tarehe 12 Machi 2022, Mwanasheria wa GSM, Alex Mgongolwa, amesema mteja wake amempa maelekezo ya kukanusha umiliki wa Makonda na kuchukua hatua zaidi ikwemo kwenda mahakamani endapo ataendelea kudai eneo hilo ni lake.

“Leo tumewaita hapa ili kuwapa taarifa fupi ya uhalali wa umiliki wa eneo lenye Plot namba 60 lililopo Regent Estate Manispaa ya Kinondoni, Dar Es Salaam,” amesema Mgongolwa.

Mgongolwa amesema Mohammed alinunua ardhi hiyo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya makazi tarehe 21 Novemba 2006 na kuonyesha waandishi wa habari nyaraka za udhibitisho.

271608744_467718128056333_5940805006310550358_n-300x189.jpg

Amesema Tarehe 19 Septemba 2017, Mohammed aliingia Mkataba na Kampuni ya ujenzi iitwayo Group Six International wenye thamani ya Sh 640 milioni “na hii ni nakala ya Mkataba huo.”

Aidha, ameongeza kuwa mteja wake aliomba kibali cha ujenzi na Manispaa ya Kinondoni walitoa kibali cha ujenzi tarehe 16 Oktoba 2017 chenye kumbukumbu namba 00020032 kwa Ghalib Said Mohammed kwa ajili ya kuanza ujenzi wa eneo hilo.

“Baada ya kibali kutolewa, Group Six walianza ujenzi na walipeleka maombi ya malipo ya awali ya ujenzi tarehe 31 Januari 2018 na Ghalib Said Mohammed alitekeleza sehemu ya Mkataba kwa kulipa kiasi cha Sh 51.9 milioni na kuna kithibitisho cha risiti ya TRA,” amesema.
Lakini kuna vitu vinachanganywa kwenye hii habari.Mfano naona mara wameingia mkataba na Group 6 mwaka 2019, mara3 nyuma zaidi,mara GSM alimiliki kiwanja hicho kuanzia 2016 , kwingine 2006.Mbona lugha gongana?

Hlf kwamba ardhi ni ya rais na mtu anapewa lease ya miaka 30 au 100 nk, je haizuii kuuziana?

Na mbona suala la disposition ya land kati ya watu lipo kisheria na lina taratibu zake?

Mbona kamkataba kameoneshwa? Labda ishu iwe kwamba taratibu za disposition hazikukamilika ndio maana details za mmiliki wa zamani bado zinasoma.Sasa hiyo issue si curable?

Au GSM anatumia loopehole hiyo ku reclaim kiwanja chake? Bs story inyooke.

Am just trying to be objective sina nasaba yoyote na Makonda wala GSM.
 
Ni lazima akomae sababu akishindwa na mmoja wengine wataibuka kumnyanganya.
 
Magufuli alijuw anapenda kufanya kazi na watu wenye haiba yake. Yote waliyotenda akina Aanaya, Makonda, Chalamila, Luhaga Mpina, Mnyeti, Mrisho Gambo, yalikuwa na Baraka zake. Alipenda mijitu isiyotumia akili kwa vile mwenyewe alikuwa katili
Lete ushahidi kwamba yote waliyofanya akina Mpina nk.yalikuwa na baraka zake.Short of that haya yatabaki kuwa majungu,uzushi, uongo na chuki binafsi.
 
Wwfanyabiashara huwa wanaonewa sana na kutishwa kwa kutoa bakhshish kila wakati
Vijana muwe mnaridhika na kazi na majukumu mliopewa na kujali maisha yenu

Hata wakubwa pia ridhikeni na maisha yenu msilazimishe kuwa na maisha ambayo hamjayatolea jasho

Sasa huyo dogo kama alikuwa na maisha ya raha kuliko sisi wote vipi tena analilia mali za wanaume?

Get a life boy
 
Possibly Makonda hakufanya transfer kwa kua labda alikua anatafuta wasaa mzuri wa kulipa capital gain tax (labda) ingawa muuzaji ndio anapaswa kulipia CG.

So jamaa baaada ya kuchungulia na kugundua kuwa bado hajafanya transfer wakaamua kulianzisha maana wana support kubwa toka kule mkoa wa pwani.
 
Inawezekana kutokana na changamoto za awamu ya tano ilibidi kweli GSM wamkabidhi kiwanja Paul Makonda wakakubaliana wa backdate tarehe isomeke 2013 kabla ya Makonda kupata Presidential appointment ambayo inamlazimu ku declare kila mali anayomiliki


Inawezekana pia baada ya JPM kutokuwepo na baada ya kupata baraka za Mamlaka mpya imebidi arudishiwe plot yake

Maana naskia za chinichini wale wote walioporwa mali zao kwa dhulma au kufungwa kwa uhujumu uchumi wanaendelea kuachiwa

Kwanini GSM hataki kueleza mazingira yoyote yaliyosababisha Makonda alazimishe kuwa hicho kiwanja no chake

Kwanini wote Makonda na GSM hawataki kwenda Mahakamani badala yale wote wanashinda kwny mitandao kutulisha story za uongo na kweli

Wote Gharib na Paul kuna ka sehemu muhimu wana ki skip kwny story yao ni sawa na ile story ya Mama Mkwe na Mka mwana kutuhumiana uchawi kwa kuwa walikutana kwa Mgang na kila mmoja hataki ijulikane
Huwa matajiri wa afrika hawaheshimiwi huko nje hata siku moja. Utajiri wao hutegemea nani yupo ikulu na wanaiva vipi nae.

Afrika ni bara limejaa matajiri wa misimu, wengi wao wana mambo mengi ya chini kwa chini na hujulikana inapotokea kiongozi mpya anapokuwa kakalia kiti cha ikulu.
 
Tena wamemtumia Ridhiwani kama waziri wa wizara ya ardhi.

Ina maana Ridhiwani alipelekwa pale maksudi ili kumkomoa Makonda.

Bila Kikwete hakuna GSM....hawa ndio wale Home Shopping Center.

Walikuwa wakinyanyasa wafanyakazi mbaya kabisa ile enzi ya JK...na sasa wamerudi ulingoni upya.

Ni wahuni kuanzia usitishaji mkataba wa TFF mpaka kufukuza waajiriwa wao wa kihindi usiku kinyemela.

Time....will....tell....
Maanina walitaka kuleta uhuni kwenye mpira wakakutana na Barbara Gonzalez akawaharibia mazima.

Huyo Gharib anaonekana mhuni fulani wa chini chini. Hana spirit ya mtu mstaarabu.
 
K
Magufuli alijuw anapenda kufanya kazi na watu wenye haiba yake. Yote waliyotenda akina Aanaya, Makonda, Chalamila, Luhaga Mpina, Mnyeti, Mrisho Gambo, yalikuwa na Baraka zake. Alipenda mijitu isiyotumia akili kwa vile mwenyewe alikuwa katili
Kwaiyo sasahivi police wanavyoua watu na kuwanyanganya mali zao Samia anausika? acheni vitu vya kijinga kumuhushisha Magufuli na ujinga,

Nchi hii ni kubwa sana hauwezi futilia kila Mtu,kuna Wakati mlikuwa mnalalamika Wakati anatumbua watu,kuwa Magufuli hafuati utawala wa sheria,amewaacha eti Magufuli amelinda watu wake,bure kabisa wanadamu
 
Back
Top Bottom