Ghalib wa GSM atoa vielelezo kuthibitisha Umiliki wa Kiwanja na Nyumba. Aagiza wanasheria kumchukulia hatua anayepotosha umma

Ghalib wa GSM atoa vielelezo kuthibitisha Umiliki wa Kiwanja na Nyumba. Aagiza wanasheria kumchukulia hatua anayepotosha umma

Possibly Makonda hakufanya transfer kwa kua labda alikua anatafuta wasaa mzuri wa kulipa capital gain tax (labda) ingawa muuzaji ndio anapaswa kulipia CG.

So jamaa baaada ya kuchungulia na kugundua kuwa bado hajafanya transfer wakaamua kulianzisha maana wana support kubwa toka kule mkoa wa pwani.
Kama uliishi kimagumashi kujipatia mali basi, zitarudi kwa style hiyo
Watajuana wenyewe wote wazee wa rafu

Ova
 
Possibly Makonda hakufanya transfer kwa kua labda alikua anatafuta wasaa mzuri wa kulipa capital gain tax (labda) ingawa muuzaji ndio anapaswa kulipia CG.

So jamaa baaada ya kuchungulia na kugundua kuwa bado hajafanya transfer wakaamua kulianzisha maana wana support kubwa toka kule mkoa wa pwani.

Usihalalishe dhulma mkuu

Hapo inajulikana watu huwa wanadhulumiwa sana na viongozi kwa simu moja tu

Africa ni njaa za viongozi kutaka kuendesha V8 kisa tajiri analo

Watu wanapambana miaka na miaka kazi za siku 7 halafu mtu anapata kazi serikalini anataka awe sawa nae kwa mwaka wa kwanza tu

Tukemee hawa watu wanaopata madaraka na vyeo na kuanza kuonea watu
 
Gharibu naye Aache ujanja ujanja wa kujipendejeza kwa viongozi Ili Mambo yake yafanikiwe,,Makonda sawa anayomakosa yake Lakini Gharibu Naye SI mtu mzuri...
 
Gharibu naye Aache ujanja ujanja wa kujipendejeza kwa viongozi Ili Mambo yake yafanikiwe,,Makonda sawa anayomakosa yake Lakini Gharibu Naye SI mtu mzuri...

Gharibu ni mtu mzuri ndio maana rafiki yake Jakaya Kikwete!!

Makonda anasema wana apartments zao wako ubia huko Masaki!!!

Ameisha anza kumwaga mboga kabla hata hakujakuchwa!!
 
Leo Machi 12, 2022 Wakili wa Kampuni ya GSM, Alex Mgongolwa amefanya mkutano na Waandishi wa habari kuanzia saa 6 kamili Mchana, GSM HQ Salamander Tower Samora Avenue.

====

Kilichojiri, full text:

======

Mwanasheria:
Huu hapa ndiyo uthibitisho, nimesema ni kielelezo namba moja, mteja wangu aliponambia nilichukua hatua ya kwenda kukithibitisha Wizara ya Ardhi nao walithibitisha na kithibitisho hiki hakijapatikana mtaani, kimepatikana katika mamlaka ambayo inatambulika.

Ukichukua namba ya kiwanja ukaenda Masjala ya Ardhi matokeao yatakuja mmiliki wa kiwanja hiki ni Ghalib Said Muhamed, na ukifikia Masjala ya Ardhi ukaonesha kiwanja namba ngapi, hati namba ngapi utapata matokeo hayo ambayo nimekueleza, hata hao ambao wanaodai kwamba hiki kiwanja ni cha kwao wakienda watapata matokeao hayo.

Baada ya umilikishwaji huu, mteja wangu alidhamiria kufanya maendelezo kwa kuwa alikuwa na nia ya kufanya maendelezo ambayo ni ya kimsingi yana gharama kubwa, aliamua mnamo tarehe 19, Septemba 2019 kuingia kwenye mkataba wa ujenzi na kampuni ya ujenzi inayoitwa Group 6 Internatinal, na huu ndio mkataba wa ujenzi na unajieleza. Kwa hiyo huingii mkataba wa kuendeleza ujenzi kama kiwanja hicho hakipo kwa jina lako, naomba mziangalie hizo tarehe vizuri nitazieleza baadaye kutokana na upotoshaji wa tarehe ambazo kimsingi hazihusiani kabisa na kiwanja hiki.

Anaendelea:
Kwa kuwa sheria ya nchi hii hazikuruhusu wewe kufanya maendelezo bila kibali, mteja wangu alifuata taratibu za kuomba kibali na kibali kilitoka kuwa ana ruhusa ya kufanya maendelezo na kilitoka 16, Oktoba 2017 na kilitoka kwa jina la Ghalib Said Muhamed, na unapofanya maombi ya kibali lazima mamlaka ijiridhishe kuwa wewe ndiye mmiliki na kama jina litakuwa tofauti hutapata kibali.

Na kwa kuwa mamlaka ya Ardhi Kinondoni ilijiridhisha na kumpa kibali, Mkandarasi akaanza ujenzi na Mteja wangu alilipa fedha zote na hadaiwi na Mkandarasi na kuna Risiti za TRA ili kuonesha kuwa mteja wangu ndiye mmiliki na alianza kumili kiwanja mwaka 2016, alifuata taratibu zote za kumiliki na kujenga na kwamba ana vibali vyote.

Anamalizia:
Kwa kumalizia, upo upotoshaji wa kidhana ambao sio sahihi kwamba ardhi mnaweza mkamilikishana watu wawili kama mtakavyotaka. Hii sio sawa na haiko kisheria, kwanza mmliki wa Ardhi ni Rais na sisi tunafanya upangishaji ambao utatajwa muda kama ni miaka 30, 100 nk. Hivyo ili umiliki Ardhi ni lazima mauziano hayo ya ardhi mamlaka ithibitishe.

Sisi kama wanasheria, mteja wetu ametuagiza kutoa vielelezo vyote ili kuonesha kuwa yeye ndiye mmiliki halali wa ardhi hiyo na kwamba mtu yeyote anayedai kuwa ni mmiliki wa ardhi hiyo atoe hadharani vithibitisho vya kisheria vilivyothibitishwa na mamlaka husika kuwa yeye ni mmiliki.

Pili, Mteja wangu ametuelekeza kulinda heshima yake ya kibiashara kwa kuchukua hatua za kisheria kwa mtu yeyote anayefanya upotoshaji wowote.

Pia, soma: Video: Makonda yamkuta makubwa, Ghalib wa GSM adai nyumba yake

KATIKA HABARI:

MFANYABISHARA Ghalib Said Mohamed maarufu GSM, ametoa vielelezo kadhaa vinavyoonesha kuhusika katika umiliki wa eneo lenye mgogoro baina yake na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya kusambaa kwa video ambayo Makonda alionekana akidai kuwa eneo hilo ni la kwake huku akiwa amezingirwa na watu akiwemo askari aliyevalia sare za jeshi la polisi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi tarehe 12 Machi 2022, Mwanasheria wa GSM, Alex Mgongolwa, amesema mteja wake amempa maelekezo ya kukanusha umiliki wa Makonda na kuchukua hatua zaidi ikwemo kwenda mahakamani endapo ataendelea kudai eneo hilo ni lake.

“Leo tumewaita hapa ili kuwapa taarifa fupi ya uhalali wa umiliki wa eneo lenye Plot namba 60 lililopo Regent Estate Manispaa ya Kinondoni, Dar Es Salaam,” amesema Mgongolwa.

Mgongolwa amesema Mohammed alinunua ardhi hiyo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya makazi tarehe 21 Novemba 2006 na kuonyesha waandishi wa habari nyaraka za udhibitisho.

271608744_467718128056333_5940805006310550358_n-300x189.jpg

Amesema Tarehe 19 Septemba 2017, Mohammed aliingia Mkataba na Kampuni ya ujenzi iitwayo Group Six International wenye thamani ya Sh 640 milioni “na hii ni nakala ya Mkataba huo.”

Aidha, ameongeza kuwa mteja wake aliomba kibali cha ujenzi na Manispaa ya Kinondoni walitoa kibali cha ujenzi tarehe 16 Oktoba 2017 chenye kumbukumbu namba 00020032 kwa Ghalib Said Mohammed kwa ajili ya kuanza ujenzi wa eneo hilo.

“Baada ya kibali kutolewa, Group Six walianza ujenzi na walipeleka maombi ya malipo ya awali ya ujenzi tarehe 31 Januari 2018 na Ghalib Said Mohammed alitekeleza sehemu ya Mkataba kwa kulipa kiasi cha Sh 51.9 milioni na kuna kithibitisho cha risiti ya TRA,” amesema.
Hili suala ni Kama linataka kummaliza kijana wetu.
 
Bashite na Sabaya sio Maguli na hawakufanya waliyofanya kwa maelekezo ya Magufuli.Pia kumbuka kwamba no President can be everywhere at the same time.Zako Ni accusations za kijinga zinazochangiwa na chuki zinazoambatana na uovu.
Mwambie mheshimiwa Jaji unamzungua Magufuli yupi? Yule ambae aliapa kupambana na mafisadi wote? Akaweza kutatua mpaka kesi za viwanja vya kina mama Igunga asione kiwanja cha mamilioni Dar? Unazungumzia Magu ambaye alikuwa na kamati na ulinzi na usalama kila wilaya? Unamzungumzia Magufuli ambaye alimwaga usalama kila kona kupata info?

Mwambie mheshimiwa Jaji kama hatukuwahi kupiga kelele juu ya uovu wa Bashite kisha akatujibu hadharani Yeye ndio Rais hatuwezi kumpangia
 
GSM ana akili kama za ndugu yangu Riziwani. Dkt Magufuli aliwaheshimu, Riziwani pamoja na kashfa zake zote Dkt Magufuli hakuwa kumdhalilisha, bali yeye alisimamia misingi ya ukweli ya uzalendo, akawabana ili marafiki zao wasikwepe kodi, leo hii Riziwani ni mtu wa kufoji document ili kufanikisha jambo la kisiasa, hivi hawajui timu ya walinzi wa taifa inawaangalia tu???? Just the matter of time watalia na kusaga meno
Hiyo timu ya walinzi wa taifa ilikuwa wapi katika awamu ya 6 kufanya kazi ili kuzuia ujambazi wa hao akina sabaya na makonda, na yule baba yao mwendazake?
 
Hahah watetezi wa Bashite mmebaki uchi kama bata.
Mwambie Bashite kama anaona amedhulumiwa aje na hizo documents na asithubutu tena kukanyaga pale site maana safari hii watamtia viboko vya kwenye yale makalio.


🤣🤣🤣Ona hizi forgery za mtoto wa darasa la tatu kabisa:
View attachment 2147993
Daah makonda hakika hana akili
 
GSM ana akili kama za ndugu yangu Riziwani. Dkt Magufuli aliwaheshimu, Riziwani pamoja na kashfa zake zote Dkt Magufuli hakuwa kumdhalilisha, bali yeye alisimamia misingi ya ukweli ya uzalendo, akawabana ili marafiki zao wasikwepe kodi, leo hii Riziwani ni mtu wa kufoji document ili kufanikisha jambo la kisiasa, hivi hawajui timu ya walinzi wa taifa inawaangalia tu???? Just the matter of time watalia na kusaga meno
Bashite!!!
 
Alafu ndo utasikia serikali ya JEIII PII EMM ilikua haina mafisadi hasa sasa huyo mende wa Chooni kweni Paulo Makondakta uozo wake mmeshaujua kundi zima la MATAGA na SUKUMA GANG[emoji57][emoji57]MamaQe
 
These are stupid dots.Tuambie unayojua maovu aliyofanya Hayati Magufuli.Hamchoki tu,mnapaka matope hata marehemu!You are so evil.Ni uzuchi tu na kusingizia watu.
Muulize ben saanane
 
Haya magenge ya kimafia yana mtandao mpana, kuwa na polisi wao, mawakili wao, mahakimu wao.

Ni kitu cha kawaida sana, waziri mastermind anacheza na akili za watanzania aombe mungu ampe maisha marefu.

Ili aje kuona rewind ya haya mapichapicha. Sasa hawezi kuona maana yeye ni mungu mtu.
 
Huyu mwanasheria ni poyoyo, huo ushahidi wa GSM ni wa kubumba maana mwenzake kaleta ushahidi wa tangu 2013. Pamoja na udhaifu wa Makonda hapo Riziwani Kikwete anahusika na hii kitu nawahakikishia itakuja kumgharimu yeye na huyo GSM.
Huu ndiyo uharisia GSM wasjione wako juu ya WATANZANIA kabisaaaa ndiyo makonda anamadhambi yake basi ahukumiwe kwa madhambi yake ila Riz1 kama kahusika juu ya hili basi hana budi ajitathimini.

Huu ukoo wa GSM ni laana unapaswa kufutiliwa mbali sivyo utatuendesha WATANZANIA kila uongozi unapobadirika.

Wao ni kina nani kila UTAWALA uwe mifukoni mwao????

Tutatetea TANZANIA siyo waharifu kama GSM au MAKONDA.

Kila mtu apate HAKI yake,GSM chunga sana umafia ulio nao watu wanaujua hivyo kukuondosha kwa heshima ya NCHI hii inawezekana,utakimbia tena nchi hii!!!
 
Huyu mwanasheria ni poyoyo, huo ushahidi wa GSM ni wa kubumba maana mwenzake kaleta ushahidi wa tangu 2013. Pamoja na udhaifu wa Makonda hapo Riziwani Kikwete anahusika na hii kitu nawahakikishia itakuja kumgharimu yeye na huyo GSM.
Huyu kaleta ushahidi wa 2006, wewe unasema w 2013

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom