Ghana yapiga marufuku kuhubiri kwenye Mabasi, Jela Miezi 8 faini Dola 52

Ghana yapiga marufuku kuhubiri kwenye Mabasi, Jela Miezi 8 faini Dola 52

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Ghana ni nchi yenye Wakristo wengi, ambapo kuhubiri injili kwenye vyombo vya usafiri wa umma ni jambo lililozoeleka. Katika mabasi ya masafa marefu, mara nyingi wachungaji huonekana na kusikika wakihubiri injili. Wakati mwingine husimama kwenye ngazi karibu na dereva, huku wengine wakitembea ndani ya basi wakisoma Biblia na kuwataka wenye dhambi watubu kwa sauti kubwa. Wanaendelea kuhubiri hata safari inapochukua saa kadhaa.

Baadhi ya abiria wanaoamini dini hiyo huwapa wahubiri fedha kama msaada wa kuendeleza shughuli zao za kuhubiri.

Hata hivyo, sheria mpya inaweza kukomesha tabia hiyo iliyozoeleka. Mtu yeyote atakayebainika kuhubiri ndani ya vyombo vya usafiri wa umma akiwa safarini anaweza kufungwa hadi miezi minane, kutozwa faini ya hadi dola 52 (takribani pauni 39), au kupewa adhabu zote mbili.

Kanuni hiyo mpya, iliyopitishwa na Bunge mwezi Mei na kuanza kutekelezwa katika wiki za hivi karibuni, inalenga kuzuia mahubiri na biashara ya kutembeza bidhaa ndani ya vyombo vya usafiri vinavyosonga. Vitendo hivyo vimeainishwa kuwa kero, huku mamlaka zikieleza kuwa hatua hiyo inalenga kulinda usalama na kuhakikisha abiria wanasafiri kwa starehe.

Katiba ya Ghana inahakikisha uhuru wa kuabudu, ingawa haki hiyo inazingatia pia masuala mengine, yakiwemo usalama wa umma.

1791107088517.png

============

Before the morning rush begins, the sound of praise and worship fills the Neoplan bus station in Ghana's capital, Accra, as a group of Christians gather to prepare to evangelise on vehicles taking travellers across the country.

Amid drumming and dancing, Boateng Bismark James leads 13 worshippers, nine men and four women, in prayer for drivers and passengers travelling to destinations across Ghana.

Ghana is a predominantly Christian country where preaching on public transport is widespread.

On long-distance buses, pastors can often be seen - and heard - preaching the gospel.

Sometimes they stand in the stairwell next to the driver, at others they walk up and down the aisle reading from the Bible and calling on sinners to repent at the tops of their voices. They do not stop even if the trip lasts for several hours.

The faithful sometimes offer money to the preachers to support their endeavours.

But a new law means this familiar practice could be coming to an end.

Anyone found preaching in public service vehicles faces up to eight months in prison, a fine of up to $52 (£39) or both.

The new regulation, passed by parliament in May, and which has started to be enforced in recent weeks, targets preaching and hawking on vehicles while they are in motion, classifying both as a nuisance and citing the safety and comfort of passengers.

The new rules have divided opinion.

Critics say preaching on moving vehicles is a nuisance and a safety risk, as it could distract the driver, while supporters argue that evangelism is a Christian duty and should be protected under the freedom of religious worship.

But in this devout country, ranked among the most religious in the world, others say evangelism on public transport is an important way of reaching people who may not attend church.

Ghana's constitution guarantees freedom of religion, although those rights are subject to considerations including public safety.


Source: BBC
 
Kwenye usafiri unakuta abiria wengine wanaumwa hivyo wanataka wapumzike wasinzie na wengine pia wamechoka wanataka wapumzike halafu hao wahubiri wanajifanya kuhubiri huku lengo lao kuu likiwa ni kukusanya pesa kutoka kwa hao abiria kwa kisingizio cha sadaka. Bure kabisa.
 
Jitu linatoka kwake saa 12 asubuhi badala kwenda kwenye shughuli za uzalishaji linabeba speaker kwenda kuhubiri vituo vya daladala huku limetega bakuli ya sadaka. Ghana wamefanya vizuri.
Ikifika jioni unapishana nae buchani ananunua nyama kilo 2 na mchele kilo 2 anaenda kujipongeza alivyowapiga hela wajingq
 
Huyo mhubiri na wafuasi wake 13 wanaopiga ngoma na kucheza wakiwaombea hukuitafsiri
Imagine unapigiwa kelele kabla hujaondoka ingawa wengine wanaona ni maombi

Bado sisi maana wamezidi kuuza madawa utafikiri ni soko
Huwa inakera sana ukiwa safarini halafu wanatuhusu watu waingie kwenye bus kupiga makelele mara dini mara anauza dawa bila aibu anataja za kuongeza nguvu ukiwa hata na watoto wako

Ni maamuzi magumu ila naunga mkono hoja
Kila mmoja aombe anavyotaka kwenye safari yake
Kwa sisi hata miziki ni karaha sana
Usafiri hauhitaji karaha
 
Back
Top Bottom