Gharama kubwa za uchapishaji wa stika za vinywaji za TRA chanzo bei kubwa za vinywaji nchini

Gharama kubwa za uchapishaji wa stika za vinywaji za TRA chanzo bei kubwa za vinywaji nchini

KING MIDAS

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Posts
8,589
Reaction score
16,936
Wazalishaji wa vinywaji vikali na baridi Tanzania wanalipa zaidi ya shilingi bilioni 100 kwa mwaka kwa hizi stempu.

Kampuni inayolipwa ni kutoka Ulaya (Uswisi) inaitwa SICPA. Hizi gharama ni kubwa ukilinganisha na nchi majirani, mfano Zambia ni robo ya hii bei. TRA wameshauriwa sana kwamba hizi gharama zinarudi kumuumiza mwananchi wa kawaida na ni bora waruhusu kampuni zaidi kuweka stempu ili kushusha bei ila hawasikii.

Hizi pesa wanaiba kwa wananchi zinapelekwa kwa nani? Mheshimiwa Rais Samia tunaomba uchukue hatua. Mambo kama haya yanafanya gharama za maisha kuzidi kuwa juu.
 
Tanzania tuna ma kodi na gharama lukuki alafu walioajiriwa wanashauri vijana wafanye biashara.
 
Duh! Aisee hii kali kwa kweli. Maana tunapigwa mpaka mshono unawaka Moto[emoji2299][emoji2299][emoji2359][emoji2359]
 
Kwanza inakuwaje vistika km hivyo vidogo vinazalishwa na kampuni ya uswisi? Mbona serikali yetu inajikebehi yenyewe? Tumeshindwa kuunda vitu vikubwa vikubwa, hata hizi stika tunashindwa kweli?
 
Back
Top Bottom