Gharama mpya za Umeme: BBC Wamkaanga Kikwete

Gharama mpya za Umeme: BBC Wamkaanga Kikwete

Nadhani sometimes JK huwa anasahau anachokizungumza!
 
Uropokaji utamponza maana alipokuwa akiahidi alikuwa bwiii.
 
Kaka ila watu wamemchoka JK, Hata huyu babu ambaye kikwete kampa zawadi kwenye birthday yake amesema anashangaa kwa nini Dowans ilipwe. jamaa ana hali ngumu.

u r right, in his campaign full of usanii aliahidi gharama za umeme zisipande, ila mwenyewe, kasema zipande, mbaya zaidi kawa bubu
kuhusu Dowans meaning anataka ilipwe yy mwenyewe akihusishwa, huyu jamaa kweli si Rais, maisha ya watu si mchezo hivi wala hajali
 
Binafsi nashangaa sana kusikia watu hawamwamini tena jk. Misemo hii inamaanishwa kwamba waliwahi kumwamini. Kwa kweli tangu siku ile alipokataliwa na baba wa Taifa kutogombea uraisi mwaka 1995 ilikuwa wazi kwamba hakuwa mtu wa kujenga nchi hii. Baba yetu wa taifa alikuwa na busara sana, kwani aliona si burasa kusema kwamba huyu mtu hafai kuwa raisi na badala yake alisema bado kijana. Kwa hakika alitumia nahau(idiom). Watu wengi walishindwa kutafsiri maana ya nahau hii, na sasa wanatafsiri kutokana na matatizo wanayoyapata.
Cha ajabu ni mwaka 2005 alipitishwa kuwa mgombea urais. Hakuna hata mmoja aliyesema huyu hastahili, wote wakanyamaza kimya. Wote walikuwa wafu, kwa maana roho zao zilishakufa. Kwangu niligundua kwamba sasa tunatawaliwa na marehemu, hivi ndivyo ilivyo.
Kimsingi watanzania tunapaswa kujua kwamba waliotuangusha ni kamati kuu ya nec(ya CCM). Hii ndiyo chanzo cha majanga yanayoikumba nchi yetu. Kwani kipindi kile nchi ilikuwa bado changa sana katika mtazamo wa vyama vingi, ukizingatia mzee wa kuhama vyama alikuwa ameshatumiwa kuua NCCR, na TLP. Nawalaumu sana viongozi wa NEC kwani walikosa utashi wa kuwasaidia wananchi wao kupata kiongozi bora. Najua walijua kumchagua mtu huyu atatupeleka wapi, kwani wao ndiyo wanakula nae, wanashirikiana kwa kila namna, hivyo walipaswa kuwapatia wananchi waliozoeza chama kimoja mtu atakayeongoza nchi na si mtu atakayebomoa nchi.
Mimi nasema, bila hofu NEC ya ccm italaumiwa kwa vizazi vyote na itafika kipindi wajuukuu zetu watachunguza koo za viongozi waliofanya maamuzi haya kwani wataendelea kulipa madeni, mikataba mibovu na unyanyasaji.
 
Ahsante Safari_ni_Safari kwa hii Document.

Article ndefu lakini very informative ni jinsi gani major projects come to being, na pia shukrani kwa mataifa mengine via World Bank na wengineo kuwa wanaangalia haya mambo yanavyofanyika.

Shukrani pia kwa Transparency International kwa juhudi zao kuwalinda walio wanyonge....

Tunajifunza mengi hapa kuwa ndio humu humu kuna waTZ ambao wako busy kuiibia nchi yao, wawekezaji ambao from word go ndio mstari wa mbele kuangalia wapi (NCHI) wanaweza kwenda kukomba mapesa bila wasiwasi.
IPTL na wengineo ni mipango kabambe ya kuifirisi nchi na kama hatuko makini kama article inavyomaonyesha, sis wenyewe hatuja 'complain ya kutosha, na ndio hapo bei zinaongezeka. Sioni sababu ya kuilaumu serikali ya hii partliament kwani haya mambo wameyakuta, ndio labda viongozi wengine ni wale wale, wapo kazini kuilinda kazi walioitenda hapo awali na sio kwa manufaa my mambo tunayoyaona hivi sasa.

Nauliza tena, tunahitaji umeme kiasi gani in MegaWatts nchi nzima, kama huu mradi wa IPTL ulipangwa kuhitaji around 175Million USD, ni 100 MW kweli hii shughuli yote hatuwezi kuifanisi sis wenyewe?
 
Babu gani Mzee Msuya?
Kaka ila watu wamemchoka JK, Hata huyu babu ambaye kikwete kampa zawadi kwenye birthday yake amesema anashangaa kwa nini Dowans ilipwe. jamaa ana hali ngumu.
 
Kwa kweli nimesikitika sana leo asubuhi watu mbalimbali walivyokuwa wakilalalmika ila BBC wamechelewa kwani walichangia kwa kiasi kikubwa JK kurudi madarakani.

Baada ya 'mwenzao' (Tido) kumwagwa!...
 
Natamani asimalize mwaka huu!! Ee Mwenyenzi Mungu saidia!
 
Back
Top Bottom