Binafsi nashangaa sana kusikia watu hawamwamini tena jk. Misemo hii inamaanishwa kwamba waliwahi kumwamini. Kwa kweli tangu siku ile alipokataliwa na baba wa Taifa kutogombea uraisi mwaka 1995 ilikuwa wazi kwamba hakuwa mtu wa kujenga nchi hii. Baba yetu wa taifa alikuwa na busara sana, kwani aliona si burasa kusema kwamba huyu mtu hafai kuwa raisi na badala yake alisema bado kijana. Kwa hakika alitumia nahau(idiom). Watu wengi walishindwa kutafsiri maana ya nahau hii, na sasa wanatafsiri kutokana na matatizo wanayoyapata.
Cha ajabu ni mwaka 2005 alipitishwa kuwa mgombea urais. Hakuna hata mmoja aliyesema huyu hastahili, wote wakanyamaza kimya. Wote walikuwa wafu, kwa maana roho zao zilishakufa. Kwangu niligundua kwamba sasa tunatawaliwa na marehemu, hivi ndivyo ilivyo.
Kimsingi watanzania tunapaswa kujua kwamba waliotuangusha ni kamati kuu ya nec(ya CCM). Hii ndiyo chanzo cha majanga yanayoikumba nchi yetu. Kwani kipindi kile nchi ilikuwa bado changa sana katika mtazamo wa vyama vingi, ukizingatia mzee wa kuhama vyama alikuwa ameshatumiwa kuua NCCR, na TLP. Nawalaumu sana viongozi wa NEC kwani walikosa utashi wa kuwasaidia wananchi wao kupata kiongozi bora. Najua walijua kumchagua mtu huyu atatupeleka wapi, kwani wao ndiyo wanakula nae, wanashirikiana kwa kila namna, hivyo walipaswa kuwapatia wananchi waliozoeza chama kimoja mtu atakayeongoza nchi na si mtu atakayebomoa nchi.
Mimi nasema, bila hofu NEC ya ccm italaumiwa kwa vizazi vyote na itafika kipindi wajuukuu zetu watachunguza koo za viongozi waliofanya maamuzi haya kwani wataendelea kulipa madeni, mikataba mibovu na unyanyasaji.