Gharama na taratibu za kufungua sanduku la posta

Gharama na taratibu za kufungua sanduku la posta

Jamani humu ndani mna mijitu mijinga na isiyojitambua, hivi mtu kuja humu akauliza swali lake kutaka kupata ufumbuzi likajitokeza jitu likajibu utumbo linamaanisha kitu gani ama kweli kuwa mstaarabu unahitaji ujitume kweli kweli. Mwisho ukiona hauna msaada pita tu silazima ujibu.

penye wengi pana mengi.. hizi ni changamoto hatuna budi kuzikabili!
 
Asanteni sana kwa msaada wakuu wa kazi. Nawatunuku degree ya heshima daraja la pili " Honoris Causa Magna Cum Laude"
A%20S%20crown-2.gif

Mara ya mwisho nafuatilia maswala ya posta nilienda pale UDSM wakaniambia kumejaa.

Nikaenda posta mpya wakataka kunipeleka posta ya zamani ila nikagoma.
 
Sanduku la posta la mtu binafsi linagharimu jumla TShs 54,400 hyo ni gharama imecontain gharama ya ada ya mwaka shs 35400 ufunguo Shs 17000 pamoja na authority card shs 2000 ukifika posta yoyote utajaza fomu then utaambiwa uwe na picha pasport size stamp size yakoymoja na ya mtu wakowwa karibu incase ukipata tatizo yeye ataenda posta na authority card kuchukua mzigo wako
Asante dada
 
Hivi ukitumiwa percel inakuja online:what:

Parcel si lazima uwe na p.o.box.mtumiaji akutumie nakala za kumbukumbu ya mzigo kwa email,nenda pamoja na vitambulisho vyako posta mpya watakupa.kwanza parcel zingine haziingi humo ndani ya box
 
Karne hii bado unategemea p.obox? Labda kama unamiliki gazeti
.

Ukifanya registration Brella wanakutumia Cheti katika sanduku la barua, mpango mkakati unakuja badae sanduku la barua litarudisha hadhi yake....
 
Posta ilikua muhimu huku kwetu wakati wa zama za mawe.kupokea bili za tanesco na nuwa (wakati mwingine haziji).
Shirika la posta linaelekea kufa baada ya mapato haswa ya stempu kushuka sana.
Ili ijikongoje serikali imewapa kazi ya kuwa wakala wa NECTA walau lijikongoje wakati linasubiri kufa.
 
Hvi bado mnaandikianaga barua mpaka karne hii ya 21?

Sanduku la posta lina faida nyingi, Sio kupokea barua tu, unaweza hata kuifadhi document za muhimu ambazo unaona zikikaa nyumban au ofisi hazina usalama bro...
 
sometimes pobox inasaidia sana ukiagiza kitu kutoka nje
 
Sanduku la posta lina faida nyingi, Sio kupokea barua tu, unaweza hata kuifadhi document za muhimu ambazo unaona zikikaa nyumban au ofisi hazina usalama bro...

yani kwa mfano ukahifadhi cheti chako cha chuo au secondary kwenye sanduku la posta,utakua unakipenda kweli hicho cheti?
 
yani kwa mfano ukahifadhi cheti chako cha chuo au secondary kwenye sanduku la posta,utakua unakipenda kweli hicho cheti?

Babu yngu alikuwa na sanduku la barua tangu miaka ya sabini huko, na uwezi amini alivyofariki tumeenda kufungua tumekuta mpaka pesa, Passport ya kusafilia na wosia wa mgawanyo wa mali katika familia..
 
Nlifungua Sanduku La Posta la binafsi hapa Dar essalaam tokea mwezi wa kumi mwaka jana mpaka sasa hivi sijapatiwa funguo. Kila nikienda naambiwa bado zamu yetu kuwekewa, inabidi kama kuna barua au kifurushi wanichukulie huko ndani.

Shirika hili lina nafasi nzuri ya kufanya biashara hasa kipindi hiki ambacho biashara za kuagiza na kuuza vitu kwa njia ya mtandao zinashamiri lakini naona wanashindwa kuchangamkia hiyo fursa kwa kutochangamkia wateja wake.
 
Mkuu hiyo sahau zaidi ya miezi miwili,hao jamaa ni wasumbufu sana mwanzo wanasema baada ya wiki mbili baada ya hapo utasikia fundi ni mmoja hvy anafunguo nyingi na maneno mengi ya kuudhi tu na usiombe ukapelekwa kule Sokoine Drive kuna jamaa mmoja bonge hivi bingwa wa kuahidi.
 
Back
Top Bottom