Gharama nafuu sio unafuu wa maisha, heri mji wenye gharama kubwa utazoweza kumudu kuliko mji wenye gharama nafuu utazosota kumudu

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
Kigezo cha kusema kwamba sehemu ina maisha nafuu kwasababu vitu vyake ni gharama nafuu ni dhaifu with a few exceptions.

Kila mkoa / nchi ina system yake kwenye matumizi na kipato, ni jambo la kuzingatia sana hasa kwa wale wanaojitafuta.

Unaweza kuwa sehemu kama Mbeya, ni mkoa unaosifika kwa gharama nafuu lakini mzunguko wa pesa ni changamoto, matumizi kwa siku yanaweza kuwa elf 3 lakini kuitafuta hio elf 3 ni mziki na haina uhakika kwasababu ya mzunguko mdogo wa pesa.

Ukienda sehemu kama Dar es Salaam ni kweli maisha yapo juu waweza kutumia elfu 10 daily lakini una uhakika wa kulaza 20 daily, ni sababu ya soko kubwa, mzunguko mkubwa wa pesa, n.k. hoja ya kwamba maisha yapo juu inapozwa kwa kipato utachoingiza

Wanaoweza ku enjoy unafuu wa maisha ni waajiriwa wanaopokea mshahara sawa mikoa yote

Muhimu: kutafuta maisha sio lazima uende mjini, kuna watu wamejipata vijijini lakini wengi zaidi hujipata kwenye mjini, kinachovutia wengi sehem flani ni uwezekano (sio guarantee) wa kuyamudu maisha kiuchumi
 
Usemacho c km kinaukwelii mkuu, Bali ndio ukweli wenyewee ....
 
Mimi naheshimu maoni yako japo SIKUBALIANI nayo....
Huo utafiti wa mzunguko wa pesa kwa watu wa mkoani umeufanya lini?
Hizi mindset za kwamba Dar ndio kila kitu zimesababisha watu wengi kuishi kwa kuunga unga hapa Dar.
Dar usipokua na nidhamu ya pesa utaishia kulipa kodi za nyumba na bill Nyingine za kuendesha Maisha yako lakini kujenga nyumba nzuri ya kisasa itakuchukua muda.
Ewe kijana usikimbilie kuja Dar ukaacha mashamba yako huko mkoani.
Kuna mjomba wangu ana miaka zaidi ya 40 yupo Dar bado mpaka sasa kapanga lakini age mate wenzie waliopo mkoani wana maisha mazuri na wanaitwa baba mwenye nyumba,anko ni wale watu wanaoamini Dar ndio kila kitu.
 
Kigezo cha kusema kwamba sehemu ina maisha nafuu kwasababu vitu vyake ni gharama nafuu ni dhaifu with a few exceptions.

Kila mkoa / nchi ina system yake kwenye matumizi na kipato, ni jambo la kuzingatia sana hasa kwa wale wanaojitafuta.

Unaweza kuwa sehemu kama Mbeya, ni mkoa unaosifika kwa gharama nafuu lakini mzunguko wa pesa ni changamoto, matumizi kwa siku yanaweza kuwa elf 3 lakini kuitafuta hio elf 3 ni mziki na haina uhakika kwasababu ya mzunguko mdogo wa pesa.

Ukienda sehemu kama Dar es Salaam ni kweli maisha yapo juu waweza kutumia elfu 10 daily lakini una uhakika wa kulaza 20 daily, ni sababu ya soko kubwa, mzunguko mkubwa wa pesa, n.k. hoja ya kwamba maisha yapo juu inapozwa kwa kipato utachoingiza

Wanaoweza ku enjoy unafuu wa maisha ni waajiriwa wanaopokea mshahara sawa mikoa yote
Rascal
 
Mimi naheshimu maoni yako japo SIKUBALIANI nayo....
Huo utafiti wa mzunguko wa pesa kwa watu wa mkoani umeufanya lini?
Hizi mindset za kwamba Dar ndio kila kitu zimesababisha watu wengi kuishi kwa kuunga unga hapa Dar.
Dar usipokua na nidhamu ya pesa utaishia kulipa kodi za nyumba na bill Nyingine za kuendesha Maisha yako lakini kujenga nyumba nzuri ya kisasa itakuchukua muda.
Ewe kijana usikimbilie kuja Dar ukaacha mashamba yako huko mkoani.
Kuna mjomba wangu ana miaka zaidi ya 40 yupo Dar bado mpaka sasa kapanga lakini age mate wenzie waliopo mkoani wana maisha mazuri na wanaitwa baba mwenye nyumba,anko ni wale watu wanaoamini Dar ndio kila kitu.
Kwa nchi yetu mgawanyo wa maendeleo umeipendelea sana Dsm tofauti na nchi nyingine, Hii hupelekea Dsm kuwa kitovu cha mzunguko mkubwa wa pesa lakini haimaanishi mikoa mingine hakuna pesa, La Hasha !! Pesa zipo mpaka huko Katavi lakini kuna utofauti mkubwa sana na sehemu nyingine

Nidhamu ya pesa haijalishi upo eneo gani, una utajiri kiasi gani, chanzo cha pesa, n.k. ukikosa nidhamu ya pesa tegemea kuyumba, hata ukiwa mkoani usipokuwa na nidhamu ya fedha anguko linakusubiri.

Huyo mjomba wako moja hawezi kuwa basis ya kuwakilisha watu kibao wanaoenda kutafuta maisha Dsm, ni tone kwenye bahari, Kuna asilimia kubwa ya vijana wanaoyapata maisha Dsm kuzidi vijana wanaofanikiwa mikoani, hili wala halihitaji mjadala.

Nihitimishe kwa kusema kwamba sehemu yoyote mtu anaweza kutoboa lakini watu hupenda kwenda kwenye uwezekano mkubwa zaidi (haimaanishi ni lazima kutoboa)
 
Back
Top Bottom