Gharama ya kujenga Swimming pool

KAUMZA

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2010
Posts
699
Reaction score
237
Wanajf, Salaam!!
Ninaomba kwa wenye ufahamu, wanisaidie. Nimepata wazo la kujenga swimming pool katika nyumba yangu iliyopo nje kidogo ya mji wa Dodoma.

Ningependa ukubwa wa swimming pool hiyo uwe ni 6m x 8m.

Naomba mchanganuo wa mahitaji ya vifaa, gharama zake na gharama za ufundi.


Karibuni sana
 

Mkuu kama ni la zege kwa size hiyo utanipatia milioni 27 na kama ni la liner utanipatia milion 25 boss
 
Hiyo Tsh 25m/27m ni gharama za ufundi tu au mimi ninakupa hiyo fedha then wewe unanikabidhi bwawa langu tu??
 
Nabaki Africa wao la mita 7 kwa 5 ni milioni 7
 
Nabaki Africa wao la mita 7 kwa 5 ni milioni 7

Hiyo Tsh 7m ni gharama za ufundi tu au unawapa Tsh 7m then wao wanakukabidhi mzigo wako wa swimming pool?
 
Kama una muda wa kusimamia ni nafuu sana ukilijenga mwenyewe kwa mafundi wako, wala si kazi, fundi yeyote anaweza kulijenga ukimnunulia vifaa, akisimamiwa na kufuata mchoro...ningekuwa Dodoma ningekusaidia hiyo kazi mkuu!
 
Hiyo Tsh 25m/27m ni gharama za ufundi tu au mimi ninakupa hiyo fedha then wewe unanikabidhi bwawa langu tu??

Naungana na mdau hapo juu,kama unataka la kisasa hizi ndio bei zake,maana nakumbuka kuna Hotel moja hapa Zanzibar walijenga lao kwa gharama hizo.
Ila kama ni la kawaida tu kama la kuogea bata,basi hata 10m tu unaweza kujenga.Ila mfumo wa maji ndio issue hapo.
La zege ni bora zaidi,kuanzia uimara hadi muonekano na hata kwenye kulipamba linapendeza saaana.

Angalizo:
Haya mabwawa kwa sie waswahili yana records saana za kuuwa,kuna nyumba sita najua vifo vilitokea vya watoto na baadhi ya watu wazima kwa uzembe.
Maana wengi inakuwa ni ugeni,sasa maji ukiyaona kwenye pool unaona kama yapo kwenye glass,sasa ingia uone.Na wengine ni watoto ambao kama hakuna ukingo basi jua utauwa kila siku.Uangalizi ni muhim saana.
 
Swimming pool mita 3 khaa we kweli unautani au we mwen zetu mbilikimo
 
Huku utakutana na madalali tu.....tembelea NABAKI huko ndiko utakutana na wataalamu na watakupa mchanganuo wote wa mahitaji yako ya hilo pool
 
Ukiwa na 55 M tunakukabidhi a complete Swimming pool.
Contact:+255659734925
 
Ukiwa na 55 M tunakukabidhi a complete Swimming pool.
Contact:+255659734925

Acha wizi weeeee.heeeee
Yaani ume form ID mpya juzi tu 11th Sep then unaanza kutapeli watu.

We umeona wapi Domestic pool likawa pesa hiyo.Nyie ndio mnaofanya kila kitu aone ghali wakati sio sahihi.Mmezoe watu waone Swimming Pool kwenye nyumba za wazungu tuuu na sie waswahili kutufanya watu wa Mabata Pool,yaani mvua ikinyesha Bata Pool formed

Kuna Hotels kibao hapa Zanzibar zimejenga na ninajua hadi wajenzi na bei hiyo haijafikia hapo,tena mbaali sana na hiyo.Itakuwa Dar kwenye karibia vifaa vyote.

Angalia mfano hili hapa ambalo hata 25m haijafika na ni la Hotel yenye uwezo wa vyuma 10.Na Pool linamifumo yoote ya kisasa
 

Attachments

  • 5.jpg
    40.9 KB · Views: 1,437
  • 22.jpg
    57.7 KB · Views: 1,460
  • 29.jpg
    52 KB · Views: 1,380
  • 28.jpg
    51.5 KB · Views: 1,373
  • 24.jpg
    56.3 KB · Views: 1,332
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…