Gharama ya kusoma CPA

Gharama ya kusoma CPA

Leyman98

New Member
Joined
Jan 12, 2023
Posts
1
Reaction score
3
Habari za sasa hivi.

Nimemaliza chuo degree ya uhasibu nataka niende kusoma CPA kwahiyo nilikuwa nauliza gharama ya kusoma hiyo CPA kwenye intermediate level itacost sh ngapi?

Natanguliza shukrani za dhati kwenu wote
 
Ewe msomi hewa... mambo mengine hayana haja ya kuleta matangazo uonekane unatangaza nia ya kwenda kuongeza usomi hewa. Tovuti maalum ya "NBAA" wewe huifahamu?! Sasa muhasibu wewe ni muhasibu gani?! 🤔
 
Umemsononesha na umemfedhehesha huyu ndg. Punguza makasiriko umshauri tena.

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
Hakuna makasiriko wala mifedhehesho na misononeko hapo... msiendekeze ujinga. Watoto wa siku hizi wanamaliza shule ila wana-graduate kwenye ujingaujinga tu na upumbavu. Sasa mtu usome uhasibu miaka mitatu lakini hujui kuhusu NBAA wewe unaona ni akili ya sawasawa hiyo?! Au wanasoma kukariri DR na CR.. expenses na liabilities basi!?!... Sanasana kujua aina ya iPhones na bei zake, Club zinazobamba sana, fashion mpya zinazo-trend na mademu wakali. Ongezea habari za wasanii pia na vioja vyao.

Usomi si kujua na kukariri ulichosomea tu na kuwa smart unukie, ununue gari na udharau watu au ukakae masaki na uwe na lifestyle ya kizungu. HAPANA! Usomi ni uwezo wa hali ya juu wa kujua, kufahamu, kufuatilia tena kwa kina!..., kuchambua na kupambanua mambo katika nyanja mbalimbali.


Msipende kulea ugonjwa. Mkubali matoto yetu yanamaliza shule ila ni ma-bogus tu kichwani.
 
Back
Top Bottom