Gharama ya kuweka sakafu ya zege/rough floor

Gharama ya kuweka sakafu ya zege/rough floor

Udochi

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2015
Posts
787
Reaction score
1,056
Nyumba ina ukubwa wa mita 14 kwa 12.5,

Ina vyumba 3, Sebule 1, Dinning room na jiko.

Fundi ameniambia labor charge ya kuweka zege/rough flow ya inchi mbili nyumba nzima ni 500,000/-,

Na ya kupiga plasta (ndani tu) ni 900,000/-.

Kwa uzoefu wenu, ni bei stahiki au anataka kunipiga?

Kama kawaida, ni lazima nilete kesi na changamoto zote zote za ujenzi katika jukwaa hili mpaka hitimisho lipatikane.
 
Nyumba ina ukubwa wa mita 14 kwa 12.5,
Ina vyumba 3, Sebule 1, Dinning room na jiko.

Fundi ameniambia labor charge ya kuweka zege/rough flow ya inchi mbili nyumba nzima ni 500,000/-.

Kwa uzoefu wenu, ni bei stahiki au anataka kunipiga?

Kama kawaida, ni lazima nilete kesi na changamoto zote zote za ujenzi katika jukwaa hili mpaka hitimisho lipatikane.
Yuko sawa nje ya hapo utatengenezewa zege bovu.
 
Yaani rough flour pamoja na skimming ni laki 9 au laki Tisa kwa hiyo kazi moja tu?

Note: Bei ya ufundi itatokana na njaa ya fundi au jinsi alivyo maarufu na si ubora wa kazi.

Huyo fundi yuko juu, mtafute mwingine. Kama uko Chanika na viunga vyake nikuunganishe na mafundi bora wenye gharama nafuu.

Kuna fundi kutoka Bunju kaja Chanika kanitajia bei za ajabu, nilimpata fundi aliifanya ile kazi vizuri kwa pesa ambayo ile aliyoitaja za Bunju unazisiaha mara 2 na nusu ndio ifanane.
 
Yaani rough flour pamoja na skimming ni laki 9 au laki Tisa kwa hiyo kazi moja tu?
Note: Bei ya ufundi itatokana na njaa ya fundi au jinsi alivyo maarufu na si ubora wa kazi...
Mkuu, labda nilikosea kuandika.

Fundi kasema
1) Kuweka rough floor @ 500,000/-,
2) Kupiga plasta @ 900,000/-,

Hivyo kwa kazi hizo mbili, niandae labour charge ya 1,4000,000/-.
 
Kama ni labour charge kwa hivyo vyumba vitatu ni siku moja tu anamaliza kwa hiyo hapo mafundi hawatazidi 4 na wasaidizi wao hawatazidi 5 kwa hesabu za haraka haraka kwa siku fundi analipwa elfu 20 na msaidizi elfu 10
Hesabu
Mafundi 4 × 20000= Tsh 80,000/=
Wasaidizi 5× 10000= Tsh 50,000/=

Jumla= 130,000/=

Cheki ulivyopigwa.
 
Mkuu, labda nilikosea kuandika.

Fundi kasema
1) Kuweka rough floor @ 500,000/-,
2) Kupiga plasta @ 900,000/-,

Hivyo kwa kazi hizo mbili, niandae labour charge ya 1,4000,000/-.
Na kwani wewe huwezi piga hesabu zako ukaona mpaka upigiwe na fundi mbona simple tu..???
 
Kama ni labour charge kwa hivyo vyumba vitatu ni siku moja tu anamaliza kwa hiyo hapo mafundi hawatazidi 3 na wasaidizi wao hawatazidi 5 kwa hesabu za haraka haraka kwa siku fundi analipwa elfu 20 na msaidizi elfu 10
Hesabu
Mafundi 4 × 20000= Tsh 80,000/=
Wasaidizi 5× 10000= Tsh 50,000/=

Jumla= 130,000/=

Cheki ulivyopigwa.
Daaaaaaah!!!
Inasikitisha sana mkuu.
Huyu fundi akiendekeza tamaa, anakosa kazi.
 
Na Kwan wewe huwezi piga hesabu zako ukaona mpaka upigiwe na fundi mbona simple tu..???
Mkuu, ugumu wa dili ugeni.
Siku zote kutojua nd'o hutupoteza watu.

Hivyo nd'o maana mimi sifanyi maafikiano mpaka nije huku kupata mwongozo.
 
Daaaaaaah!!!
Inasikitisha sana mkuu.
Huyu fundi akiendekeza tamaa, anakosa kazi.
Muulizie atatumia mafundi wangapi na vibarua wangapi kwa hiyo kazi uone Kama hajakimbia na akikujibu piga hesabu mwenyewe uone na mafundi wengine huwa wanaangalia na watu wa kuwapiga kuweni makini.
 
Muulizie atatumia mafundi wangapi na vibarua wangapi kwa hiyo kazi uone Kama hajakimbia na akikujibu piga hesabu mwenyewe uone.
Hawa jamaa wanataka kunifanya mimi babu yao.

Kwenye upauaji walitaka kunipiga materials, nikakaba mpaka penalt baada ya kupata mwongozo kutoka humu jukwaani.

Sasa hivi nd'o wananiseti ili wanipige upande wa labour charge,
Ni mafundi wazuri kiujenzi, Ila watakosa kazi kwa kuendekeza tamaa.
 
Nyumba ina ukubwa wa mita 14 kwa 12.5,
Ina vyumba 3, Sebule 1, Dinning room na jiko...
Me inafanana ya yako ingawa kwenye dimensions yako kubwa yangu ni 12.5m× 11m
Jamaa kanipigia Rough Floor kwa 300k
Anasema plasta ndani na nje 1.2M
Nilikua nataka yale ya maurembo ya madirishani

Changamoto

1. Siku nimetoka majirani zangu ambao huwa wanalinda wakaniambia kuwa aliiba baadhi ya mifuko ya cement wanasema miwili na kuendelea.

2. Hiyo rough floor hata haikuwa ile nzuri na nahisi imesababishwa na wizi.

Sasa hapo amenikera hiyo kazi ya plasta sitompa tena.
 
Me inafanana ya yako ingawa kwenye dimensions yako kubwa yangu ni 12.5m× 11m
Jamaa kanipigia Rough Floor kwa 300k...
Aiseeeee!!!
Hapa kwenye wizi hapa ndo panaumiza sana, kwani hupelekea kazi kuwa chini ya kiwango.

Jumla walikwambia ununue mifuko mingapi kwa ajili ya rough floor?
 
Aiseeeee!!!
Hapa kwenye wizi hapa nd'o panaumiza sana, kwani hupelekea kazi kuwa chini ya kiwango.

Jumla walikwambia ununue mifuko mingapi kwa ajili ya rough floor?
Ilikua 21 mkuu ila ndio hivyo walichapa sasa hata nashindwa kujua ilitumika mingapi ndugu yangu
 
Mimi wameniambia mifuko 20,
Yawezekana ni sahihi.

Nitachokifanya ni kutoondoka saiti mpaka wamalize mifuko yote.
Mimi alinichana jamaa kuwa mzee ulivyochomoka kula wamepita na mifuko hapa nimeoma miwili me ilinikata moto kweli

Nikawa nasubiri kuona mwisho wa kazi sikuridhishwa

Akaanza kunipa hesabu za plasta na nini nikamwambia respect yourself hatuwezi fanya lazi za kuchungana kama watoto natafuta fundi mwingine

Hakuwa amenielewa ila ataona nitakavyoanza plasta vitu vitapita kwake ila kazi hatoiona
 
Kama ni labour charge kwa hivyo vyumba vitatu ni siku moja tu anamaliza kwa hiyo hapo mafundi hawatazidi 4 na wasaidizi wao hawatazidi 5 kwa hesabu za haraka haraka kwa siku fundi analipwa elfu 20 na msaidizi elfu 10
Hesabu
Mafundi 4 × 20000= Tsh 80,000/=
Wasaidizi 5× 10000= Tsh 50,000/=

Jumla= 130,000/=

Cheki ulivyopigwa.
Hizo hesabu umepiga kwa vigezo gani? Vyumba vitatu vya aina gani?
 
Back
Top Bottom