Ila wakuu kupitia jamvi hli yaani mmenisaidi sana maana kuna fundi alishanipiga kwenye msingi na kunyanyua boma "4mil", sasa iv alitaka kunipiga pesa mingi kwenye rough
Ameniambia kupiga rough nyumba ya vyumba 3 sebule ,Dinning, jiko na stoo 1mil
Lakini kupitia jamvi hili nimepata fundi wa laki 3 na ni fundi mzuri yule wa milion nimempiga chini , nashangaa leo ananifata anaomba hata kazi ya kusimamia nikamwambia ntasimamia mwenyewe.
Nawashukuru sana wakuu .
Nilichojifunza kuna mafundi wengi wazuri lakini hawana Majina "hawajajulikana" tuwatumie hawa tena hawana tamaa wala wizi.