Yuko sawa nje ya hapo utatengenezewa zege bovu.Nyumba ina ukubwa wa mita 14 kwa 12.5,
Ina vyumba 3, Sebule 1, Dinning room na jiko.
Fundi ameniambia labor charge ya kuweka zege/rough flow ya inchi mbili nyumba nzima ni 500,000/-.
Kwa uzoefu wenu, ni bei stahiki au anataka kunipiga?
Kama kawaida, ni lazima nilete kesi na changamoto zote zote za ujenzi katika jukwaa hili mpaka hitimisho lipatikane.
UnapigwaAhsante sana mkuu.
Na vipi kuhusu kupiga plasta (ndani pekee) kwa labor charge ya Sh. 900,000/- IPO sahihi au napigwa?
Mkuu, labda nilikosea kuandika.Yaani rough flour pamoja na skimming ni laki 9 au laki Tisa kwa hiyo kazi moja tu?
Note: Bei ya ufundi itatokana na njaa ya fundi au jinsi alivyo maarufu na si ubora wa kazi...
Na kwani wewe huwezi piga hesabu zako ukaona mpaka upigiwe na fundi mbona simple tu..???Mkuu, labda nilikosea kuandika.
Fundi kasema
1) Kuweka rough floor @ 500,000/-,
2) Kupiga plasta @ 900,000/-,
Hivyo kwa kazi hizo mbili, niandae labour charge ya 1,4000,000/-.
Daaaaaaah!!!Kama ni labour charge kwa hivyo vyumba vitatu ni siku moja tu anamaliza kwa hiyo hapo mafundi hawatazidi 3 na wasaidizi wao hawatazidi 5 kwa hesabu za haraka haraka kwa siku fundi analipwa elfu 20 na msaidizi elfu 10
Hesabu
Mafundi 4 × 20000= Tsh 80,000/=
Wasaidizi 5× 10000= Tsh 50,000/=
Jumla= 130,000/=
Cheki ulivyopigwa.
Muulizie atatumia mafundi wangapi na vibarua wangapi kwa hiyo kazi uone Kama hajakimbia na akikujibu piga hesabu mwenyewe uone na mafundi wengine huwa wanaangalia na watu wa kuwapiga kuweni makini.Daaaaaaah!!!
Inasikitisha sana mkuu.
Huyu fundi akiendekeza tamaa, anakosa kazi.
Hawa jamaa wanataka kunifanya mimi babu yao.Muulizie atatumia mafundi wangapi na vibarua wangapi kwa hiyo kazi uone Kama hajakimbia na akikujibu piga hesabu mwenyewe uone.
Me inafanana ya yako ingawa kwenye dimensions yako kubwa yangu ni 12.5m× 11mNyumba ina ukubwa wa mita 14 kwa 12.5,
Ina vyumba 3, Sebule 1, Dinning room na jiko...
Aiseeeee!!!Me inafanana ya yako ingawa kwenye dimensions yako kubwa yangu ni 12.5m× 11m
Jamaa kanipigia Rough Floor kwa 300k...
Ilikua 21 mkuu ila ndio hivyo walichapa sasa hata nashindwa kujua ilitumika mingapi ndugu yanguAiseeeee!!!
Hapa kwenye wizi hapa nd'o panaumiza sana, kwani hupelekea kazi kuwa chini ya kiwango.
Jumla walikwambia ununue mifuko mingapi kwa ajili ya rough floor?
Mimi alinichana jamaa kuwa mzee ulivyochomoka kula wamepita na mifuko hapa nimeoma miwili me ilinikata moto kweliMimi wameniambia mifuko 20,
Yawezekana ni sahihi.
Nitachokifanya ni kutoondoka saiti mpaka wamalize mifuko yote.
Hizo hesabu umepiga kwa vigezo gani? Vyumba vitatu vya aina gani?Kama ni labour charge kwa hivyo vyumba vitatu ni siku moja tu anamaliza kwa hiyo hapo mafundi hawatazidi 4 na wasaidizi wao hawatazidi 5 kwa hesabu za haraka haraka kwa siku fundi analipwa elfu 20 na msaidizi elfu 10
Hesabu
Mafundi 4 × 20000= Tsh 80,000/=
Wasaidizi 5× 10000= Tsh 50,000/=
Jumla= 130,000/=
Cheki ulivyopigwa.
Hiyo plasta ni ndani na nje au? Kwa bei hiyo?Nyumba ina ukubwa wa mita 14 kwa 12.5,
Ina vyumba 3, Sebule 1, Dinning room na jiko...