Gharama ya kuweka sakafu ya zege/rough floor

Amekupiga parefu sana, mara mbili yake. We agiza lori kubwa la kokoto, agiza roli la mchanga, nunua mwenyewe mifuko ya sumenti, halafu ahirisha kwenda kazini siku hiyo mwambie fundi leo tutafanya kazi pamoja na wewe.

Halafu uone kama hiyo gharama itafika. Mimi kwenye nyumba yangu siku wanafanya vitu vya maana, kuanzia umwagaji wa zege, nilikuwa siendi kazini, navaa nguo za kazi naenda kushinda hapohapo, wakiwa wanakoroga zege na mimi nakoroga, kubeba zege, kila kitu. Nimekuja kujua mafundi ni wezi sana.
 
Mkuu siku zote usiishie kuzungumza na fundi mmoja, jifanye unataka kumpa dili na fundi mwingine na mwingine, kupitia michanganuo yao utapata bei tofauti tofauti kwa kazi yako, hapo utajua ni bei gani usimamie.

Japo usipende kuwagalaliza sana, fundi anaweza kukupa hesabu nyepesi ili umpe tu kazi apate mkate wake.
Bei za mafundi pia hutegemea na eneo husika, fundi anayejenga site za Masaki, Oysterbay gharama zake hazitakuwa sawa na anayejenga Kwa mfuga Mbwa.

Yote kwa yote,gharama hzo zipo juu sana,kuna mdau ameshauri hapo juu,fundi akupe mchanganuo wa idadi ya mafundi na vibarua watakao ifanya hiyo kazi na siku watakazotumia kuikamilisha hiyo kazi then itakua jukumu lako kuupima huo mchanganuo,ila pia utapaswa kujua kupiga plasta per room ni bei gani? Japo ukubwa wa room unatofautiana ila bei hazitaachana sana,Sio fundi akupe tu bei ya jumla ya kazi.

Nawasilisha...
 
Ngastika machale kundesa
 
Hiyo plasta ni ndani na nje au?kwa bei hiyo?
Hiyo ni bei ya plasta ni ndani tu mkuu.
Nichane uhalisia ili hata nikitafuta fundi mwingine niweze kubargain bei reasonable?
 
Mimi nipo mkoa wa Pwani mkuu.
Ila ushauri wako nauzingatia kabisa.
Hizi hela za ujenzi hata sisi tunadunduliza na kujinyima sana, Ila ndugu zetu mafundi wanataka kutulalia.
 
Kama fundi amebainika kakuibia vifaa, hafai kupewa kazi tena huyo.

Na itapoanza kazi ya plasta, akija kukuulilza "Boss vipi kuhusu kazi?"
Mwambie ukweli kuwa
"Niliacha vyanzo vya taarifa za kiintelijensia na kubaini wizi wa wazi wa vifaa vyangu na hivyo kuharibu kazi yangu,
Hii imekupotezea heshima na uaminifu wako pia"
 
Asante sana mkuu.
Kwenye kipengele cha kuwepo saiti hapo niko vizuri.
Nitakomaa nao liwake jua, inyeshe mvua.
 
Nimekusoma mkuu,
Baada ya kununua mchanga na kokoto,
nitafanya maulizo kwa mafundi kadhaa kabla ya kuanza kazi.
 
Nitakapoanza tu najua atajileta maana ni karibu na eneo la ujenzi ataipata habari yake.

Me huwaga navunga tu mtu akifanya ujinga/wizi nikajua ila akija kujizima data hapo ndio nakua mkali.
 
Asante sana mkuu.
Kwenye kipengele cha kuwepo saiti hapo niko vizuri.
Nitakomaa nao liwake jua, inyeshe mvua.
Uwe makini lakini, unaweza kuwepo hapohapo wakakuibia vilevile, mimi sumenti niliweka kwenye kapikapu kangu, ikatulia, wanachana mfuko mmoja, nawapa mwingine hadi ilivyoisha. Mabaki ya mifuko nakuwa nayo na nahakikisha hawanibambikii. Wanao uwezo ukiwa umeenda washroom wakaleta mfuko uliochanwa wakauweka pale na mfuko mzima wa sumenti wakapeleka nyumba ya jirani.

Unaona kama hela ni ndogondogo lakini wakifanya hivyo kwa watu kadhaa wanapata mifuko mingi tu, same applies kwenye nondo. Mmoja aliwahi kuniletea dili la nondo karibia 20, badala ya 24k kila nondo anataka aniuzie 19. Nilimuuliza umetoa wapi, akasema kuna jamaa zake walikuwa wanajenga ghorofa sehemu sasa zimebaki, ni za kwao wala sio za wizi nisiogope. Nikajiuliza, huyu tajiri mjenga ghorofa wanamuibia huko sijui ni nani?
 
Kwa ufupi plaster chumba kimoja ni kati 50,000-70,000 na rafu 30,000-50,000 kwa ndani. Sebule, dining na jiko hesabu kama chumba kila kimoja.

Korido na vyoo inategemea na ukubwa unaweza vichanganya vikawa chumba kimoja. Pia bei inategemea na eneo na hadhi ya fundi.
 

Weka total square meter za floor
Weka total square meter za ukuta wa ndani tukusaidie
 
Mimi wameniambia mifuko 20,
Yawezekana ni sahihi.

Nitachokifanya ni kutoondoka saiti mpaka wamalize mifuko yote.

Agizia chakula kije hapo hapo site [emoji4][emoji4]
 
Hiyo ni bei ya plasta ni ndani tu mkuu.
Nichane uhalisia ili hata nikitafuta fundi mwingine niweze kubargain bei reasonable?

Achana na huyo fundi tafuta mwengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…