Gharama ya ujenzi wa vyumba vitatu, sebule, jiko na choo cha ndani

Gharama ya ujenzi wa vyumba vitatu, sebule, jiko na choo cha ndani

Ndugu Lee Swagger ,maoni yako niliya copy ngoja niyabandike hapa kama kumbukumbu[emoji16][emoji16]

Wakulungwa eee! Njooni tumshangae huyu jamaa!
Lee Swagger
______________________________________
Ukiniambia Nyumba itakua na Square Meter ngapi naweza kukupa Makadirio ya Msingi Tu, au Ujenzi mpka finishing.

Kwa Bei Ya Vifaa ya Sasa makadirio inaweza kugharimu million 100. Mpka Finishing. Gharama hyo inaweza Kuongezeka au kupungua Kutokana na Bei ya Vifaa Vya UJENZI na Upatikanaji Wake kwenye eneo Husika.

Hii Hapa ni mfano wa Vyumba 3. Nyumba ya Makazi.

  • Masta 1, Vyumba vya Kawaida 2.
  • Study/ Prayer Room
  • Sebule, Dinning, Open Kitchen na Stoo yake
  • Choo Cha public
  • Bafu Public.

Ina Sqm 217.5. Kitalaamu Gharama ya Ujenzi Mpaka Kukamilka Kila Kitu ni Tsh 108,750,000/=

Huo ndio Ukweli Mchungu, Bila kukuongopea.
_______________________________________
Umeandika maoni kama mtu asiye na kichwa, basi tumia cha chini bhana...

(JOKES)
 
Usiyafuate ili wajukuu wako waje wasome ulivyokuwa unatema shudu in public.
[emoji23][emoji23][emoji23]
Mkuu, nimeamua kuya laminate mawazo yake! Niliyakopi mahali kwa ajili ya kutengenezea uzi wake ili majukwaa yote waone ni jinsi gani Tanzania tunavyopigwa na vitu vizito [emoji23][emoji23]
 
Kakope around 40 M
Si unataka kujenga nyumba nzuri mkeo umnyandue kwa kujiachia na mkweo akija alale na kujisaidia kwa raha zake?
Kama ndio andaa hiyo pesa hapo juu,achana na hao wanao kuambia 15 to 25M hiyo nyumba au double self?
 
[emoji23][emoji23][emoji23]
Mkuu, nimeamua kuya laminate mawazo yake! Niliyakopi mahali kwa ajili ya kutengenezea uzi wake ili majukwaa yote waone ni jinsi gani Tanzania tunavyopigwa na vitu vizito [emoji23][emoji23]
Alikuwa anataka kumkatisha tamaa jamaa tu hana.
 
Lee Swagger [emoji23][emoji23] Milioni 108 ! [emoji23][emoji23]
Ila hii nchi hii,[emoji1787][emoji1787]

Hiyo pesa si ni ya kujenga hekalu! Kanisa letu hapa limejengwa kwa 90m

Akaamua kuweka na kapicha uchwara kutoka facebook ili kuthibitisha!
 
Na ni wapi wataka kujenga?
Maana ujenzi gharama hutegemea na eneo ie mjini au kijijini; Dar au mkoani!
 
Unataka kujenga nyumba gani?
Ya miti au matofari!
So fafanua wajuzi wakupe makadirio!
 
Chukua milioni 50 ya kuanzia, na hapo akili ikuchemka kwelikweli uvute hadi mahali unaweza kuhamia. Changamoto kubwa kwwa sasa material za ujenzi zimepanda bei maradufu....na hali inavyoonyesha zinaendelea kupanda zaidi.
 
Unajenga, unao, bahati mbaya unamkuta na mchepuko, mnaachana, anaenda mahakamani kudai talaka na kugawana mali. Maisha hayana formula
 
Kwa ushauri wangu, usikope kwanza kabla ya kuonana na wataalam wakutengenezee ramani inayoendana na mahitaji yako, hapo ndipo utapata na makadirio halisi ya gharama za ujenzi (material pamoja na ufundi)

Baada ya hapo ndio unaweza kwenda kukopa huku ukijua hiyo nyumba inagharimu kiasi gani,na huo mkopo unaoweza kupata utaweza kumaliza nyumba au unaweza kuishia njiani

Kwa hapo utaepukana na yale mambo yakuchukua mkopo na ukashindwa kumaliza ujenzi.
 
Basi Poa Nafuta Maoni Yangu Endeleeni Kujazana Ujinga.
Usingefuta, unajua nyumba inategemea na vile mtu anataka iwe. Mnaweza kutumia ramani moja, eneo moja, soil structure same, lakini gharama zikatofautiana kwa sababu ya quality kila mmoja anazotaka.

Yes, inawezekana three bedroom house kufika 100 au 150 hadi finishing, inawezekana kabisa na/au isitoshe, lakini pia inawezekana kama wengi wanavyosema hapa nyumba ikajengwa kwa 40-50m na mtu akaishi.

Ndio maana zipo nyumba ukipita unatamani usimame uangalie na macho yanafurahi, na zipo nyumba unapita and you don't notice anything.
 
Back
Top Bottom