Gharama za bando zitaua creativity, biashara na ndoto nyingi za vijana

Gharama za bando zitaua creativity, biashara na ndoto nyingi za vijana

Mkiambiwa suluhu ni kukiwasha tu je mtajitokeza kupambania haki zenu za msingi! Sema serikali imeshazoea inajua watanzania ni kama misukule iliokatwa ulimi wapo wapo tu 😂
Yeah dawa ni kuanzisha Timbwili tuu, hawa jamaa siku watu waingie pale mjengoni Dom hadi ndani anapokaa Speaker, wang'oe viti na zile Mic ndio akili itawakaa sawa.
 
Yeah dawa ni kuanzisha Timbwili tuu, hawa jamaa siku watu waingie pale mjengoni Dom hadi ndani anapokaa Speaker, wang'oe viti na zile Mic ndio akili itawakaa sawa.
Tatizo tumeruhusu walioshiba ndio watufanyie maamuzi! 😅

Sometime namkumbuka sana mchonga na siasa zake za TV moja Tabata nzima na ole wake mtu ajenge nyumba ya tofali. Tofali ni nyumba za serikali tu! Ole wake afisa hata mmoja atumie madaraka kupiga hela 😂😂😂!Hao wasimamizi wangekuwa na njaa sote tungeongea lugha moja ila wao wanajiamulia watakavyo sababu hawako kwenye kikatio wao wameshikilia kwenye mpini!

Tunabambikwa matozo wao shule,hospitali,usafiri ni kwa gharama ya serikali na bado mamishahara makubwa wanalipana na kulindana kwenye wizi wa hela ya serikali! Mtu kama huyu hawezi kukuthamini.
 
Sure..jamaa wao wameshiba hawatujui wenye njaaa. Lakini shida nyingine kubwa kwa hapa Bongo, watu ni waoga sanaaa. Mkijipanga hata 500 tu hakuna sehemu mtashindwa kuingia kwa mkupuo. Bongo bila kuanzisha mtiti hawa jamaa watakuja kutuingiza vidole puani.
 
Waziri aliekuepo kwa maoni Yangu alikua poa kabisa na Accessible..Wameleta Huyu Mama anaitwa Kijaji hata sidhani kama Anashugulika na haya masuala...Kuna balaa kubwa kwenye bando saiv.bei iko juu sana..Sio tu vijana kwa ufupi maisha karibu yote yanaguswa na Internet siku hizi...lakini kwa Tz imekua anasa...Unapigwa Makonzi ya kutuma hela..Mabando..bei ya mafuta duh
 
Hakika
 
Kuna mtu anakitamba sijui atazindua chuo cha Tehama mara sijui kuboresha mazingira ya Tehama huku anapandisha garama ya bando kimya kimya
 
Hii nchi imeanza kuwa ngumu. Tangu juzi bando silielewi. Licha ya kupandisha gharama lkn bando linapepea km moshi.
Sasa hivi ili uweze kuwasiliana lazima
1. Ujiunge bando la Dakika pekee
2. Sms pekee
3. Bando la internet pekee
Hivyi vyote itakugharimu 30,000 kwa wiki.
Mtandao uwe anasa kweli kwa zama hizi? Huu ni wizi umeanza.
 
Kwa hiyo wakipandisha bando ndo watu watashindwa kushusha spana, wamebugi aisee......
Halafu nilivyoona wamemfukuza Ndugulile kwenye wizara, nikajua wamemtoa mbuzi wa kafara ili watibu majeraha ya raia kumbe ni kinyume chake!

Mambo yanavyokwenda sasa ninashindwa kuelewa jinsi wafanya biashara kufanya watakavyo bila serikali kuingilia kwa vyovyote!

Rais kalisemea hilo lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa, matokeo yake hali ndiyo imekuwa ni mbaya zaidi!

Yaani wafanya biashara wanaipima serikali kwa kupandisha bei bidhaa na serikali haikunjurui makucha ipo tu kimya, maana yake inaridhika!

Ninadhani kuna ka 'sindikate' ka wafanya biashara na mawaziri kameungana kuihujumu serikali.

Mambo yanyokwenda sasahivi ninashindwa hata kuamini yaani!
 
Hizi bando zinavyopanda bei unaweza hisi hata gharama za uzalishaji wa hizo bando huwa zinaongezeka kila mwaka kumbe ni urasimu tu.
 
Kwamba watakuja kuleta suluhisho,ili ionekane kuwa tatizo limetatuliwa, Yani ni mwendo kuleta 'problems' na baada ya malalamiko 'solvings' yake inatoka Yani Kama hesabu vile...
 
wasanii wa Nigeria watakuwa wamefurahi mnoo.

Silaha yetu kuu kimataifa ilikuwa ni bando za bei chee kuwamwagia mamilioni ya views / streams wasanii wetu, hii ilifanya hata watu wa mataifa mengine wawajue maana ni nadea kukuta msanii wa Africa ana views kibao.

Pia na huko instagram na fb wasanii wetu walikuwa na followers wengi sana, ila ni sisi watz ndio tulio wafollow kwa asilimia zaido ya 90.

Tusubirie anguko kubwa mno, saizi kuingie youtube kwa mtu mwenye kipato cha chini ni kwa machale sana, heri adownload kuliko ku stream
 
Hizi bando zinavyopanda bei unaweza hisi hata gharama za uzalishaji wa hizo bando huwa zinaongezeka kila mwaka kumbe ni urasimu tu.
Hahaaha utadhani na wenyewe zinasafirishwa kama diesel.
 
Inabidi tuache upole wa kijinga sisi wa Tanzania, mabadiliko yanahitajika sana. Asante kwa andiko zuri na muhimu kutumia andiko hili na mengine mazuri kufumbua vijana wenzetu.
 
You see? Vitu kama hivi vinahitaji bando ambayo ingewasaidia sana TRA wenyewe
 
Back
Top Bottom