Gharama za bima kupanda

crabat

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2012
Posts
4,323
Reaction score
2,207
Mamlaka ya shughuli za bima TIRA kwa barua ya Commissioner wake Bw Kamuzora imekubali maombi ya makampuni

ya bima kuongeza gharama za bima za magari kwa zaidi ya asilimia 500%.

kwa mujibu wa barua ya TIRA gharama hizo zitaanza kutumika rasmi kuanzia tarehe 01 March 2013.
Insurance premium hizo zimeongezwa na jumuia ya makampuni ya bima yaani Association of Tanzania Insurers-ATI ambapo habari za ndani kabisa ya kikao hicho ni kwamba ongezeko hilo halikuzingatia hali halisi ya kipato cha wana nchi wala Uchumi wa nchi au gharama za madai zitokanazo na bima za magari bali kimeangalia zaidi faida kwa kampuni hayo

gharama za chini kwa bima ya kawaida yaani third party kwa magari ya mizigo yaani Trucks yamepanda kutoka Tshs 100,000/- mpaka Ths 750,000/-
magari ya mafuta yaani tankers kutoka Tshs 150,000/= mpaka Tshs 1,000,000/-
GHARAMA HIZO NI KWA GARI ZOTE ZA MIZIGO IKIWA NI PICK UP AU CANTERS AU TRAILERS AMA TRUCKS.
UKIANGALIA GHARAMA HIZO NI ZA JUU SANA NA WATU WENGI SASA WANAWEZA KUENDESHA MAGARI BILA YA INSURANCE.
HABARI ZA NDANI NI KUWA MASHIRIKA YA BIMA YA SERIKALI ZIC NA NIC YALIKATAA ONGEZEKO HILO LAKINI kutokana na WINGI WA MAKAMPUNI YA PRIVATE HIVYo IKALAZIMIKA KUPITISHWA.
PIA HABARI ZA NDANI YA KIKAO CHA "ATI" NI KUWA MAKAMPUNI MENGI HAYATAKI KUTOA BIMA ZA MAGARI HIVYO NI KAMA KUWAKOMOA WATANZANIA.
UPANDE WA DALA DALA ZIMEPANDA KUTOKA Tshs 7,500/- kwa kila seat moja mpaka Tshs 15,000/-
mabasi ya mikoani kutoka Tshs 10,000/- kwa seat moja hadi Tshs 25,000/-
taxis kutoka Tshs 60,0000/- hadi Tshs 150,000/-
magari binafsi Tshs 40,000/- mpaka Tshs 100,000/-
magari ya school ya wanafunzi kutoka Tshs 5,000/- kwa seat hadi Tshs 15,000/- kwa seat moja.
gharama hizi bila shaka zitaathiri gharama za uchukuzi na kugharimu shughuli za uchumi.
mfano ubebaji wa mafuta na abiria , mizigo na mafuta.
Pia katika gharama hizo kuna ongezeko kubwa la bima kubwa yaani comprehensive
mfano tankers imepanda kutoka 4% ya thamani ya gari mpaka 9%
kwa hio gari mpya ya gari ya scania inayofikia USD 300,000 bima yake itakuwa ni USD 27,000/- hii ni sawa na akufukuzae hakwambii toka.
cha ajabu ni kwa nini TIRA imekubali kila kitu kama ili vo pendekezwa na ATI bila ya kulinda maslahi ya walaji, uchumi wa nchi na wao TIRA wameangalia zaidi maslahi ya makampuni katika kupata faida.
nchi nyingi Regulators ndio wanahusikaa kupandisha ama kushusha gharama za bima ya magari kwa sababu bima hizo ni lazima kwa mujubu wa sheria. Na uwezo wa kupandisha kitaalam TIRA Wanao kwani wanazo data zote za makampuni ya bima na wana jua loss ratio iliopo kwenye soko.
lakini hili la kupandisha bima ya third party kwa pick up ya tani moja kuwa Tshs 750,000 kweli TIRA wamechemsha
sasa nusura yetu ipo kwa fair competion commision kuangalia suala hili


Gharama za uendeshaji wa magari ya abiria kama Dala dala, Taxis, Magari ya mizigo na mafuta yataongezeka maradufu kuazia March 2013.
 
Aisee hii ni kali ya mwaka!
Mlaji halindwi Fair Competion Commission nao wakifumba macho kwishnii.
Tutapaki magari juu ya mawe! LOL
 
Mkuu nilienda kulipa bima ya gari ambayo inaisha mwezi wa tatu.. Kilichotokea niliambiwa gharama zimepanda na kuwa bado muda wake haujamalizika hawapokei hela mpaka iishe.. Nilichoambiwa Viwango vipya vinaanza mwezi wa March.. Nikaweka ligi ya nguvu pale mpaka boci wa sehemu ile akawaambie wanikatie hiyo bima.. Ndo nikapata hizi habari kwa mara ya kwanza..! Waitoe sheria ya kuwa na bima ya magari waone watanzania walio wengi kama watakata hizo bima zao.. Inakera..
 

Tukijitahidi sana wote tutakata third party......
 
Tukijitahidi sana wote tutakata third party......

Na hiyo Dina ni kwa vile tunalazimishwa na sheria.. Vinginevyo hamna hata haja ya kukata hiyo third party.. Haya makampuni ya bima kwanza yanapunja malipo ya fidia kwa waathirika.. Yaani wao slogan zao ni kutolipa fidia.. maana ukiwa unafuatilia madai ukiwa wa kukata tamaa.. mapema tu unawasusia..
 
Tukijitahidi sana wote tutakata third party......

Na haya ndiyo malengo yao ili wapate bila kufidia kwani 3rd party ni wangapi wanafuatilia....But real inaumiza sana.
 
Na haya ndiyo malengo yao ili wapate bila kufidia kwani 3rd party ni wangapi wanafuatilia....But real inaumiza sana.

Na inakera haswa, ni basi tu kuwa sheria inabana, vinginevyo wangetusikia redioni tu....
 

Mkuu umenifurahisha ati uliweka Ligi ya Nguvu...
 
Wenye nyumba za kupangisha wataanza kulipa kodi gharama za bima kupanda ada za shule ni ndoto kushuka mishahara ipo pale pale bado wanasema maisha bora kwa kila mtanzania,
 
Mkuu umenifurahisha ati uliweka Ligi ya Nguvu...

Ha ha ha.. Mkuu Duduwasha bajeti yenyewe ya kuunga unga.. Nimeshapiga kadili kangu nikapanga kabisa hii ni ya bima.. Halafu wao wananikatalia.. Ukifika huo mwezi wa tatu kama cina hela ndo nipaki gari home..?
 

Kanuni mojawapo ya bima ni: A good insurer is he who does not pay promptly. Ndo maana ukipata tatizo la fidia utazungushwa sana mpaka ukate tamaa ...ile kwako.
 
Nchi hii inaongozwa na vichaa. huwezi kwa mfano toka Tzs.40,000 mpaka Tzs.100,000/=. yaani ukaruka 50k,60k,70,89k,90k ukaweka Tzs.100k. ni vema wangeacha kabisa kugusa magari ya wanafunzi. Huko kwa wenzetu shughuli zote za wanafunzi huwa na bure hapa kwetu kama mataahira tu!! Bungeni mtusaidie kupiga kelele huku kuna vibaka wanaitwa TIRA. Makampuni mengi hapa ya Insurance yameshikiliwa na waasia na hawa jamaa kwa kuhonga ni mwisho. Pls they must stop this new rate. Ina maana hawa wakora hawana watu wa kuwahoji wao ni kuibuka tu kama mzee wa makilomita ( makuguri) alivyokuja na rate za Kigamboni ferry??
 


Hii inatakiwa ikomalie kama ile ya mafao maana athali zake ni kwa kila mtu, hakuna atakaebaki salama bila kuguswa na hili kwa njia moja au nyingine.
 
Kama hutaki bima, tembelea mitaa ya mkwepu pale kuna vijana wanauza stika za bima yeyote unayoitaka kwa buku tano tuu.
 
Aisee hii ni kali ya mwaka!
Mlaji halindwi Fair Competion Commission nao wakifumba macho kwishnii.
Tutapaki magari juu ya mawe! LOL

Na sio kupaki tu....sasa ndio hakun abima mjini kuna fake tu
 

sasa hio third party mfani ka gari chako ni pick up tani mbile insurance yake ni Tshs 750, 000
mkuu hapa its crazy kwa TIRA...Basi hawajui hata viwango....vipi wamewakubalia hawa jamaa ?
yaani pick hio ulikua unalipa Tshs 40,000 sasa ni 750,000
dah.....bora turudi tu enzi za NIC peke yake
 

Kinachofuatia ni TRA kupandisha kodi ya road licence.. Utacikia bunge la bajeti la June.. Mwisho wa ciku kuiweka gari barabarani itakuwa ni anasa kubwa.. Kweli ule msemo wa mwenye nacho ataongezewa bali asie nacho atanyang'anywa hata kile kidogo alicho nacho umeswihi sawia hapa..
 
huu ndio unaitwa uku**nina wa tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…