Gharama za hospital ni kubwa. Jitahidini muwe na bima

Gharama za hospital ni kubwa. Jitahidini muwe na bima

Yaani unaumwa mgongo halafu umeanfikiwa ufanye ultrasound,arooo mbona majanga
Ili mradi pesa iingie kutunisha mfuko wa hospital,

Siku hizi ukienda hospital usipokuwa mtu wa kuhoji utatapunwa pesa mpaka senti ya mwisho hospital nyingi zimekaa kiupigaji sana .

Ushauri: unapokwenda hospital Dr akikuandikia vipimo muulize Kila kipimo na maana yake na hata akikuandikia dawa pia muulize Kila dawa na kazi yake, ukimuona kapaniki na hakupi majibu ya kuridhisha basi jua kwamba hakuna Dr hapo.
 
MadKtari wa Kitanzania haijalishi ni bingwa au sio bingwa ni wa kuwa nao makini sana,most of them hawapo serious na kazi.tuwe tunajaribu hata ku Google ambacho wanatueleza kama vina endana na hali tunazo zisikia miilini mwetu.
Juzi hospitali ya rufaa nimechanganyiwa dawa,isingekuwa tabia zangu za udadisi dadisi na kuumuliza dkt labda ningekuwa nisha kufa.
 
Pamoja na kuwa na Bima kubwa ya Watumishi ile ya kuongezea malipo,kuna dawa inauzwa 240K bima haikuweza ku cover.
Ukiwa huna hela utakufa unajiona tujitahidi tutafute pesa.
 
Wengine unaweza Kua nabima mpaka yaExpire hujaitumia
 
Pole sana mkuu

Labda kama haukuwahi kuugua au kuuguza ile serious

Ila gharama za hospitali hazijawahi kuwa ndogo au nafuu hapa Tanzania
 
Bima za nini sasa? Huku mtaani huwa tunaenda maabara kupima tukiugua MARALIA buku, UTI buku, TYPHOID buku nne ukipewa majibu unaenda kununua dawa unakunywa unapona life linasonga . Unapona kwa buku tano, kipimo buku, mseto buku tatu paracetamol buku. Kwenda hospitali mpaka tuzidiwe tuwe mahtuti maana ukienda huko kwa malaria hiyo hiyo unstoboka kuanzia elfu arobaini mpaka hamsini plus kukaa kwenye foleni
 
Bima yenyewe kwa kifurushi kinachoeleweka ujipange haswa tofauti na hapo utaangukia kwenye hivi vya Panadol tu.

Kikubwa ni kujitahidi kuepuka magonjwa ambayo yanaepukika kwa 100%.

BTW:Unakimbia X-ray,ungeandikiwa CT Scan ama MRI ingekuwaje sasa?
 
Mpaka sasa nimetumia 133,000/= kwa ajili ya vipimo. Na kuna kipimo ki1 nimeacha sababu ya kukosa pesa. Nina maumivu mgongoni. Kuanzia usawa wa mbavu kuja juu.

Nimekuja kumwona dr baada ya kumpa maelezo kaniandikia kufanya vipimo vya ultrasound, xray, na vipimo v3 vingine kutoka kwenye damu. Ambavyo ni kwa ajili ya kuangalia mafuta. Yaani chollestral. Nimeacha kufanya xray ambayo nitaifanya j3.

Dah gharama za matibabu ni kubwa. Ambao hamjaajiriwa kama mimi, bima ya afya ni muhimu. Tujitahidi kuwa nayo itakusaidia kwa kweli.
Halafu huku kitaa tatizo kama hilo watu huwa wanapiga mitishamba maisha yanaendelea mkuu

Usije kushangaa ultra sound ikatoa majibu kuwa huna tatizo lolote, x ray ikatoa majibu huna shida yoyote, cholesterol huna pia. Ila ukijiangalia unajiona unaumwa kitakachofata daktari atakutandika dozi za neuroton, ibuprofen au diclofenac na tatizo likabaki pale na umechoma laki na nusu.
 
Unanikumbusha Kuna mwaka nimeumia mpirani nimepata maumivu makali kifuani. Nimefika zahati binafsi Daktari ananiambia nina UTI. Nikamwambie nipe NHIF yangu niondoke.

Ninachotaka kusema kama huna uelewa wa matibabu hospitali binafsi zinatumia njia chafu ili utoe hela nyingi pasipo na uhitaji wa msingi.
kuna madaktari wakikutibia ni km wahuni tu wa mtaani mambo yao.
 
Kwenye H. Pylori hapo hata mimi nakazia
Hata vitamin d kaka watu siku hizi hawaoti jua ni ndani gari kiyoyozi ofisini ..... rudi kusoma zile kazi za vitamin d mwilini na uhusiano wake na calcium na madini mengine .... then kasome namna misuli inavyo takiwa kufanya kazi .....


Nmetibu mgonjwa siku 14 sio kawaida asipate matokeo kafanya vipimo vyote

Nikamrudisha kwa orthopedic specialist hola kaenda moi kaonana super specialists wote kafanya MRI, CT SCAN, EKG ECHO ECG na kila kipimo unacho kijua wewe kuweza kiangalia kama visceral organ ndio source ya maumivu wapi .....

Ndio katokea Dr wakihindi aga khan kasema apime vitamin D na h_pyroli

Baada ya dawa ndio kupona
 
Back
Top Bottom