DOKEZO Gharama za kuegesha gari Hospitali ya Muhimbili ni kubwa na zinaumiza

DOKEZO Gharama za kuegesha gari Hospitali ya Muhimbili ni kubwa na zinaumiza

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Yamenikuta juzi na JANA tu 27 Feb 2024. Tayari wamenilamba 10,000/= Ki ukweli niliumia sana. Pale Muhimbili si sehemu ya starehe na hakuna anayependa kwenda Muhimbili tu fo the sake of kwenda. Kwa bahati mbaya sana, hakuna huduma unayoweza kupata kwa muda wa saa 1 au 2. USHAURI. Mtu anayetibiwa pale baada ya matibabu apewe green card ya kutoka bure. Watakaochajiwa tena kwa pesa isiyozidi sh 2000 wawe ni wale waliokuja kwa sababu zisizo za matibabu kama waliokuja kuangalia wagonjwa, watoa huduma nyinginezo n.k

Asante kwa aliyeanzisha huu uzi
 
Una akili sana umeliona hilo

Hata mi nnaona wanajaribu kuwavunja moyo wa watu kupenda kwenda na magari yao Muhimbili....... lakini wamebakia sensitive enough kuwasikiliza wanaopeleka au kufuata mgonjwa chaap na kuondoka (chini ya nusu saa)

Kwa kifupi hawataki pawe kero parking space bali watu waje na kuondoka. Na kama hawataki kuja na kuondoka basi wajilipie gharama za kupaki.

Mi nnaona sahihi tu

Halafu uliyeshauri eti waangalie nani ni mgonjwa na nani ni mgeni. Hivi unawezaje kusimamia utaratibu wa namna hiyo? Sasa wenye magonjwa ya kudumu itakuwaje? Mtu akimwambia mlinzi nnaumwa kichwa mlinzi atajuaje🤨. Bora tu waweke hela mingi halafu hayo mengine watu watajirekebisha wenyewe
Kumjua Mgonjwa rahisi sana. Mgonjwa apewe green card ya kutolipia parking baada ya kumaliza matibabu. Hakuna mgonjwa asiye na doc zza matibabu. Anapewa pale getini, akimaliza matibabu anapewa another card kuonyesha alikuwa kwenye matibabu. Simple, ukitumia brain hicho ni kitu simple sana.
 
Parking fee haifai kuzidi 2,000 Kwa kutwa. Ile ni hospitali ya umma.
 
Kumjua Mgonjwa rahisi sana. Mgonjwa apewe green card ya kutolipia parking baada ya kumaliza matibabu. Hakuna mgonjwa asiye na doc zza matibabu. Anapewa pale getini, akimaliza matibabu anapewa another card kuonyesha alikuwa kwenye matibabu. Simple, ukitumia brain hicho ni kitu simple sana.
Ni sawa inawezekana

Hiyo ni kama lengo ni mgonjwa apaki na asiye mgonjwa asipaki.

Lakini umejiuliza kwamba vipi kama lengo ni hadi huyo mgonjwa mwenyewe asipaki!? Yaani watu waje na kuondoka tu. Waachwe na wafuatwe tu baaas🙅‍♀️

Labda wamepiga hesabu kwamba kama kila mgonjwa atapaki gari yake freely hapatatosha pia? Ndio likaja suluhisho la kuwavunja moyo kuja na magari

NB: Yoote niliyoandika ni speculation tu, nimefikiria mara tatu basi nikaandika
 
Back
Top Bottom