DOKEZO Gharama za kuegesha gari Hospitali ya Muhimbili ni kubwa na zinaumiza

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Yamenikuta juzi na JANA tu 27 Feb 2024. Tayari wamenilamba 10,000/= Ki ukweli niliumia sana. Pale Muhimbili si sehemu ya starehe na hakuna anayependa kwenda Muhimbili tu fo the sake of kwenda. Kwa bahati mbaya sana, hakuna huduma unayoweza kupata kwa muda wa saa 1 au 2. USHAURI. Mtu anayetibiwa pale baada ya matibabu apewe green card ya kutoka bure. Watakaochajiwa tena kwa pesa isiyozidi sh 2000 wawe ni wale waliokuja kwa sababu zisizo za matibabu kama waliokuja kuangalia wagonjwa, watoa huduma nyinginezo n.k

Asante kwa aliyeanzisha huu uzi
 
Kumjua Mgonjwa rahisi sana. Mgonjwa apewe green card ya kutolipia parking baada ya kumaliza matibabu. Hakuna mgonjwa asiye na doc zza matibabu. Anapewa pale getini, akimaliza matibabu anapewa another card kuonyesha alikuwa kwenye matibabu. Simple, ukitumia brain hicho ni kitu simple sana.
 
Parking fee haifai kuzidi 2,000 Kwa kutwa. Ile ni hospitali ya umma.
 
Ni sawa inawezekana

Hiyo ni kama lengo ni mgonjwa apaki na asiye mgonjwa asipaki.

Lakini umejiuliza kwamba vipi kama lengo ni hadi huyo mgonjwa mwenyewe asipaki!? Yaani watu waje na kuondoka tu. Waachwe na wafuatwe tu baaas🙅‍♀️

Labda wamepiga hesabu kwamba kama kila mgonjwa atapaki gari yake freely hapatatosha pia? Ndio likaja suluhisho la kuwavunja moyo kuja na magari

NB: Yoote niliyoandika ni speculation tu, nimefikiria mara tatu basi nikaandika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…