JOHNGERVAS
JF-Expert Member
- Mar 22, 2016
- 1,011
- 1,681
Wakuu Kwema? Bila shaka muko salama.
Mwezi uliopita Nilikuwa Hospitali ya Taifa ya Mloganzila, Baada ya mke wangu Kuhamishiwa hapo baaada ya Kupewa Rufaa kutoka Kituo cha Afya ambapo alienda Kujifungua. Alienda Hospitali ya kawaida baade madaktari wakashauri awahimishwe Hospitali ya Taifa Mloganzila.
Kitu ambacho Nimeona Gharama za pale ni kubwa sana ni kama Hospitali za Watu Binafsi au Taasisi za Dini n.k
Wakati anapokelewa Pale Emergence nilitakiwa Kulipia Laki moja Fedha Taslimu ambayo wanaita ni ya Accomadation na haina maelezo mengine tena unapewa Control number ulipie ndio aanze Kuhudumiwa.
Baada ya Hapo alijifungua salama watoto wawili Mapacha alikaa siku ya Ijumaa hadi Jumatatu yaani Siku tatu Tu nikapewa Bill ya 1.35 yaani (Milioni moja laki tatu na elfu thelathini na tano) Nikasita kulipa nikaenda kwa wahasibu Kugombana nao Kidogo nikitaka Ufafanuzi japo Ilishindikana.
Baadae niliuliza Nikaambiwa Ghrama ya Kulala kwa Siku ni 50,000 lakini gharama ya Kujifungua ni 750,000. Niliambiwa Hiyo ssera ya mama wajawazito wanajifungua Bure haipo ni Siasa na Propaganda Tu.
Nilipambana nikalipia kiasi nikatoka.
Lakini kwa Kifupi Gharama Za Hospitali ya Mloganzila Ni kufuru kule ndani nilikuta akina mama waliojifungua wana Daiwa Wengine Millioni tatu, tano na kuendelea wameshikiliwa wake pale hadi fedha ipatikane.
Kwa kweli jambo hili linaumiza sana watanzania wa hali ya Chini ambao Kimsingi wanaamini Hospitali za Umma zinazoendeshwa naKupata Ruzuku kutoka serikalini ambayo ni kodi za wananchi gharama zake ziwe rafiki ili kila mwananchi aweze Kumudu ila imekuwa ni Tofauti.
Soma Pia: Gharama zinazotozwa Muhimbili Hospital kuwahudumia “Watoto njiti” zinatuumiza tunaouguza
WIZARA YA Afya Aid Inatakiwa ilitazame hili na wawaweke wananchi wazi kwamba ile ni Hospitali ya Kulipia .
Ushahidi wa Nyaraka zote nianzo Mods musifute mukitaka ushahidi wa Receipt na Bill nitawapa.
Pia soma: DOKEZO: Serikali iimulike hospitali ya Mloganzila, Huduma zake ni janga kwa wagonjwa na ndugu wanaouguza pale
===================
Ummy Mwalimu, aliyekuwa Waziri wa Afya akizungumza kuhusu Sera ya huduma bure katika hospitali za Serikali, ilikuwa Januari 10, 2024.
Ema Ngatoluwa Mratibu Wa Afya Ya Uzazi Na Mtoto mkoa wa Manyara akizungumza katika mahojiano, aliulizwa kuhusu gharama za huduma za kujifungua na kusema ni bure. Hii ilikuwa Januari 14, 2024