Gharama za kumiliki kifo

Gharama za kumiliki kifo

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Waswahel wa Pwani waliosema pesa mwanaharamu sijui ninini kiliwapa mpaka kuna na huo usemi
Nijuavyo mimi ukiachana na mengine yote.

Kuna kitu kinaitwa kichaa cha pesa! Pesa inachizisha watu na kuwafanya wendawazimu kabisa! Hata wewe ukizipata utawehuka hasa zikishakuwa nyingi na ziada kwa ajili ya kutimiza matamanio ya kimwili na kudhihirisha ukwasi wengi hujikuta wananunua na kumiliki kifo kwa gharama kubwa!

Kumiliki helicopter ni aina mojawapo ya kudhihirisha mapene mengi uliyonayo.. Maana gharama zake si mchezo kuanzia
Manunuzi
Vibali
Mafuta
Rubani
Service
Ruhusa ya kuruka
Maegesho nknk

Pamoja na usafiri wa ndege kutajwa kama usafiri salama zaidi duniani.. Lakini kwa helicopter ni ngumu kuamini sana hayo yanayosemwa.

Helicopter zimekatisha maisha ya watu wengi maarufu na wenye pesa nyingi. Helicopter haina comfortability yoyote. Hata ukipanda hamuwezi kusikilizana na ni lazima mvae headphones.

Hata kama kuna life jackets lakini msaada wake ni mdogo sana kwakuwa ajali za helicopter hutokea ghafla na bila dalili za kukupa muda wa kujiandaa.

Kwa mshangao mkubwa watu wwnamiliki chombo hiki ambacho kimejaa gharama na usumbufu mwingi. Halafu kifo ni njenje.
Kumiliki helicopter ni sawa na kumiliki kifo kwa gharama kubwa!
Kingine ni kumiliki bastola!
 
Vipi kumiliki gari sio kifo? Magari yamekuwa yakigongwa/kugonga na kusababisha vifo. Halafu kuna zile helkopta zenye matairi kama zile black cobra za marekani zenyewe mbona ni nzuri hazina kelele kama hizi chopper. Kuna tajiri mmoja muuza pombe kali huko manyara kanunua helkopta aina ya chopper, ina maana anamiliki kifo?
 
Waswahel wa Pwani waliosema pesa mwanaharamu sijui ninini kiliwapa mpaka kuna na huo usemi
Nijuavyo mimi ukiachana na mengine yote.

Kuna kitu kinaitwa kichaa cha pesa! Pesa inachizisha watu na kuwafanya wendawazimu kabisa! Hata wewe ukizipata utawehuka hasa zikishakuwa nyingi na ziada kwa ajili ya kutimiza matamanio ya kimwili na kudhihirisha ukwasi wengi hujikuta wananunua na kumiliki kifo kwa gharama kubwa!

Kumiliki helicopter ni aina mojawapo ya kudhihirisha mapene mengi uliyonayo.. Maana gharama zake si mchezo kuanzia
Manunuzi
Vibali
Mafuta
Rubani
Service
Ruhusa ya kuruka
Maegesho nknk

Pamoja na usafiri wa ndege kutajwa kama usafiri salama zaidi duniani.. Lakini kwa helicopter ni ngumu kuamini sana hayo yanayosemwa.

Helicopter zimekatisha maisha ya watu wengi maarufu na wenye pesa nyingi. Helicopter haina comfortability yoyote. Hata ukipanda hamuwezi kusikilizana na ni lazima mvae headphones.

Hata kama kuna life jackets lakini msaada wake ni mdogo sana kwakuwa ajali za helicopter hutokea ghafla na bila dalili za kukupa muda wa kujiandaa.

Kwa mshangao mkubwa watu wwnamiliki chombo hiki ambacho kimejaa gharama na usumbufu mwingi. Halafu kifo ni njenje.
Kumiliki helicopter ni sawa na kumiliki kifo kwa gharama kubwa!
Kingine ni kumiliki bastola!
Mhhh.... mshana huwa nakukubali lakini hii mbona ni kama hate speech kwa bil Mulokozi?

Acha watu watumie pesa mkuu, wamezitafuta kwa shida. Halafu kumbuka ni pesa za kuuza pombe hivo usijali sana
 
Ni mwakani tu hapo nakua bilionea ila hata mimi kwenye mipango yangu hizo helicopter hazipo kwenye hesabu zangu.
Sionagi raha yake, ni kama upo vitani vile. Labda mwamba ana vikao na shughuli maeneo mbalimbali ya nchi hivyo anahitaji kuwahi ndio maana kanunua.

Wakijenga viwanja maeneo mengi basi nitafikiria kununua ndege binafsi ya abiria.
 
Mshana bana ..
Wengine walimiliki mtungi mmoja ww gesi ,ukaua familia nzima.
Wengine bodaboda walizomiliki ziliwaua,
Wengine gari ,wengine baiskel,n.k
Suala la mauti na kifo halina kwao.
Halina ukoo,halina matajiri au maskini.
Halibagui wa baiskeli au helicopter.
Umiliki chochote usimiliki chochote mauti ipo pale pale..
Hata kama ni kitoto cha siku moja anaokufa.
Kufa ni hakika na kweli..
Haina uhusiano wowote na kumiliki chochote.
 
Kweli Ila katika bastola hapo ni Kwa ajili ya kujilinda zaidi hasa kutokana hali ya usalama .
Hicho ni kifo mkononi wakati wewe unamaliza mwaka ama zaidi hujanitumia anayekuja kukuvamia anatumia daily.. Nani yuko sharp hapo? Yeye kajiandaa ila wewe kakustukiza
 
Back
Top Bottom