Gharama za kumuuguza Mzee zinaongezeka. Sisi tumeshachoka kwa kweli. Bora tu achukuliwe

Gharama za kumuuguza Mzee zinaongezeka. Sisi tumeshachoka kwa kweli. Bora tu achukuliwe

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
10,931
Reaction score
24,816
Kuna kipindi pia aliumwaaa.... tukafikia hatua tukasema bora tu arudishe number maana sasa inakuwa changamoto kwetu. Akaja akapona. Shida ikawa pale pale. Hakuna afadhali akiwa mzima shida akiugua shida. Ni msumbufu sana.

Sasa this time anaumwa tena. mwezi wa 3 huu amelala tumehamisha hosp zote. Tunagharamia ukimwangalia age yake nayo imeenda sana. 90 plus. Anataka aendelee kuishi kufanya nini hapa duniani? Sasa tunatumia pesa ambazo zingesaidia wajukuu wake kumtibu mgonjwa mbaye kwa kweli ameshakula chumvi ya kutosha hapa duniani. Mwisho wa siku tunamuona tu kama chuma ulete. Maana kila pesa zetu zinaenda kwenye matibabu yake. Meno yake yameshatoka, anaishi kwa shida. Anaanikwa tu juani kama mjusi ila bado anataka aendelee kuishi. Unajiuliza aishi kufanya nini hapa duniani? Mbona alishamaliza kila kitu?

Sasa inafikia kipindi tunasema bora tu akapumzike nasi tupumzike kidogo maana atatufilisi kwa kweli. Mimi nimeshauza gari moja, nimechukua mkopo, nimekuwa sasa nina madeni ile mbaya. Kwa mabro wengine nao.. ishakuwa shida. Maana tulishampeleka mpaka India kipindi fulani. Wakatwambia kwa huu umri asifanyiwe hayo matibabu maana kinga zake nazo zimekosa nguvu. So alilazwa tu akipewa madawa miezi mitatu. Gharama kubwa ilikuja kwetu. Akarudi amekuwa tia maji tia maji kama gari la mkaa trip moja shamba nyingine gereji.

Ila bado mbishi sana, bado anataka atibiwe na kupelekwa hosp za gharama, sasa mzee si atatuacha watoto wake tumefilisika halafu ndo afe? Hapo tutakuwa tumefanya nini? Nahitaji ushauri wenu kwa kweli hili jambo limenifika hatua nimechoka sana. Sipendi unafiki... hii hali ni ngumu sana maana sasa hata ukiona simu toka kwa ndugu unashindwa kupokea maana huchelewi kuambiwa sasa tuchangie kila mtu atoe 700,000 kuna vipimo na matibabu flani tena yanatakiwa.
 
Pole kwa kuuguza kaka, hamna jinsi kama yeye aliwajibika ipasavyo wakati mnakua pengine mlikuwa hata zaidi ya watoto watatu!! Uwajibikaji umehamia kwenu hamna jinsi pambaneni mkishirikiana na madaktari wawaeleze hali halisi!!! Ingekuwa kwa wenzetu kuna "Mercy killing"
 
kuna kipindi pia aliumwaaaaaa.... tukafikia hatua tukasema bora tu arudishe number maana sasa inakuwa changamoto kwetu. akaja akapona.. shida ikawa pale pale. hakuna afadhali akiwa mzima shida akiugua shida. ni msumbufu sana....
Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa heshima

Hii ni Qur'an inatuamrisha haya
Kumbuka wewe ulivokuwa mtoto huenda ulikuwa msumbufu sana ila wazazi wako walikuvumilia iweje leo wewe huwezi kumvumilia mzazi wako?

Yawezekana angekuwa tajiri mkubwa tu lakini alisacrifice akakulea wewe kwa pesa zake leo hii iweje yeye ndio sababu ya wewe kupatikana lakini unamdhalilisha kiasi hiki.

Najivunia kuwa Muislamu kwani Uislamu umetufunza yote haya.
 
Do
kuna kipindi pia aliumwaaaaaa.... tukafikia hatua tukasema bora tu arudishe number maana sasa inakuwa changamoto kwetu. akaja akapona.. shida ikawa pale pale. hakuna afadhali akiwa mzima shida akiugua shida. ni msumbufu sana....
Do your best and let God do the rest. Uthamani wa mzazi utauona akishaondoka duniani. Unatamani angalau usikiye sauti yake tu inatosha lakini ndo basi tena hayupo. Mzee wako akiondoka duniani wewe na ndugu ndo mutakuwa next kuondoka duniani. Tayari nyiye ndo munabaki generation yenye umri unaofuata kuondoka hapa duniani. Hivyo unaweza kuona maisha hapa duniani hayana maana kabisa. Uwe na pesa usiwe na pesa kuondoka kuko pale pale. Hivyo pesa siyo kila kitu, mtunze mzee wako mpaka dakika yake ya mwisho.

Pesa si kila kitu pambana mpaka mwisho wake. Unaweza kutoa pesa zote kwa ajili yake. Lakini utashangaa akishaondoka duniani unapata pesa nyingi kuliko hizo ulizotoa.

Pesa ni upepo tu leo zipo kesho hazipo. Tafadhali mtunze baba yako mpaka dakika yake ya mwisho hapa duniani. Mzee akifikisha 90+ brain yake ya kufikiri inashuka hivyo kuwa na hasira na vitu vidogo ni kawaida. Muwe naye karibu tu.
 
Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako...
Mkuu.. wewe huujui uislamu kuliko mimi. Ungenyamaza tu ili usije leta mjadala wa kidini hapa. Mimi toka babu yangu alikuwa sheikh, mufti na alhaj.

Wewe maamuma tu unataka jifanya unaifahamu dini na mistari ya kukariri kuliko watu wenye uelewa wa dini? Acha huo upuuzi hapa tunaongea kisomi siyo kimaamuma.
 
angeyasikia haya maneno nina hakika angekufa leo leo...

huna ustaarabu hata kdg

usisahau na wewe ni mzee mtarajiwa
Mimi mpaka hapo sijaona ustaarabu wako pia. Mimi nimeongea uhalisia ulivyo. Kila mtu ni mzee na marehemu mtarajiwa. So hi haitoi kibali cha mtu kuwa mnafiki na mpuuzi. Kuna haja gani kutumia chakula cha wazima kumpa mtu ambaye hatoweza kuwa mzima? Wafe wote? Miaka 90 plus unadhani ni michache? Na hali yake si nzuri. Unadhani kuna mtu ataishi milele?
 
Kuna kipindi pia aliumwaaaaaa.... tukafikia hatua tukasema bora tu arudishe number maana sasa inakuwa changamoto kwetu. akaja akapona.. shida ikawa pale pale. hakuna afadhali akiwa mzima shida akiugua shida. ni msumbufu sana....

sasa this time anaumwa tena. mwezi wa 3 huu amelala tumehamisha hosp zote... tunagharamia ukimwangalia age yake nayo imeenda sana. 90 plus. anataka aendelee kuishi kufanya nini hapa duniani? sasa tunatumia pesa ambazo zingesaidia wajukuu wake kumtibu mgonjwa mbaye kwa kweli ameshakula chumvi ya kutosha hapa duniani. mwisho wa siku tunamwona tu kama chuma ulete. maana kila pesa zetu zinaenda kwenye matibabu yake. meno yake yameshatoka, anaishi kwa shida... anaanikwa tu juani kama mjusi ila bado anataka aendelee kuishi. unajiuliza aishi kufanya nini hapa duniani? mbona alishamaliza kila kitu?

Sasa inafikia kipindi tunasema bora tu akapumzike nasi tupumzike kidogo maana atatufilisi kwa kweli. mimi nimeshauza gari moja. nimechukua mkopo, nimekuwa sasa nina madeni ile mbaya. kwa mabro wengine nao.. ishakuwa shida. maana tulishampeleka mpaka india kipindi flani... wakatwambia kwa huu umri asifanyiwe hayo matibabu maana kinga zake nazo zimekosa nguvu. so alilazwa tu akipewa madawa miezi mitatu. gharama kubwa ilikuja kwetu. akarudi amekuwa tia maji tia maji . kama gari la mkaa trio moja shamba nyingine gereji.

Ila bado mbishi sana, bado anataka atibiwe na kupelekwa hosp za gharama, sasa mzee si atatuacha watoto wake tumefilisika halafu ndo afe? hapo tutakuwa tumefanya nini? nahitaji ushauri wenu kwa kweli hili jambo limenifika hatua nimechoka sana.sipendi unafiki... hii hali ni ngumu sana. maana sasa hata ukiona simu toka kwa ndugu unashindwa kupokea maana huchelewi kuambiwa sasa tuchangie kila mtu atoe 700,000 kuna vipimo na maibabu flani tena yanatakiwa.
Tatizo ni wanafamilia kuwa masikini
 
Usimuache utabarikiwa ushangae. Nilimuuguza babu yangu miaka 2 ilikuwa ameumwa sana na wanaye hawamjali walimchoka kama wewe ulivyochoka!

Baada ya kuumuuguza Hadi kufulia, alipofariki tu nikashangaaa mambo yote yamerudi fasta tena mazuri kuliko mwanzo.
 
Kuna kipindi pia aliumwaaaaaa.... tukafikia hatua tukasema bora tu arudishe number maana sasa inakuwa changamoto kwetu. akaja akapona.. shida ikawa pale pale. hakuna afadhali akiwa mzima shida akiugua shida. ni msumbufu sana.....
Mambo mengine yafiche moyoni tu, maana unajiaibisha tu unamuanikaje mzazi wako hadharani hivi
 
Back
Top Bottom