Gharama za kumuuguza Mzee zinaongezeka. Sisi tumeshachoka kwa kweli. Bora tu achukuliwe

Gharama za kumuuguza Mzee zinaongezeka. Sisi tumeshachoka kwa kweli. Bora tu achukuliwe

Pole kwa kuuguza kaka , hamna jinsi kama yeye aliwajibika ipasavyo wakati mnakua pengine mlikua hata zaidi ya watoto watatu !! Uwajibikaji umehamia kwenu hamna jinsi pambaneni mkishirikiana na madaktari wawaeleze hali halisi !!! Ingekua kwa wenzetu kuna "Mercy killing"
Hakuna cha "mercy killing" uuwaji ni uuwaji tu kuondoa uhai wa mtu unasema ni mercy?
 
Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa hishima



hii ni Qur'an inatuamrisha haya
kumbuka ww ulivokua mtoto huenda ulikua msumbufu sana ila wazazi wako walikuvumilia iweje leo ww huwezi kumvumilia mzazi wako?
Yawezekana angekua tajiri mkubwa tu lkn alisacrifice akakulea ww kwa pesa zake leo hii iweje yy ndio sababu ya ww kupatikana lkn unamdhalilisha kiasi hichi

Najivunia kua Muislamu kwani Uislamu umetufunza yte hya
Neno la Muumba wetu ni amri hivyo ni amri kuwalea wazazi wawili kwa heshima na kuwajali.
 
Niliwahi sikia baadhi ya makabila kuna dawa huwa wanameza..sasa wakifikia hatua ya uzee hawafi haraka..yaani mpaka kuna dua maalumu wanasomewa ndio wanakufa..inaweza kufikia mtu ni mzee mpaka baadhi ya sehemu za mwili kama zinaoza ila bado hakati moto..

Binafsi naamini kila mtu anakufa kwa siku zake..kama siku zake bado msitake kumuwahisha..unless mfanye kama baadhi ya nchi za ulaya kumchoma sindano..kitu ambacho sio sawa.
 
Wewe yasikie tu hawa wanaosem vumilia hawajui eti wanakupa mistari ya Qoran hyo ni theory ukija kweny uhalisia utajua hujui. Sisi kwetu wazee walifikia hatua wakataka wamuwekee baba yao sumu afe lkn ikashindn coz kila mtu alipata ugumu wa kummywesha hyo sumu, mzee akafa kwa wakati wake na watu wakapata ahueni
 
Juz. Nilikuwa Happ seliani hospital kumuona mam ake na jamaa angu ambaye aamelzwa hapo aisee had nikawaonea huruma mnk walimtoa pale na kumpeleka ktk kipimo Cha CT scan ya hospital ya nsk huku nikiona kbsa kuwa mgonjwa huyu awezi kukatisha usiku hajaondoka nilitaka niwaambie kuwa watulie tu mnk sioni dalili ya mam huyu kusurvive kwa jins alivyo kuwa mnk alishindwa had kula kwa takribani week nzima.

Ajabu ilipoa fika saa nane usku yule mgonjwa akafariki nikakumbua ule usumbufu wa kumuamisha amisha na kuanagika nae aisee kuuguza sikia kwa mwinginee tu bi pesa zinatoka jamani.
 
mkuu.. wewe huujui uislamu kuliko mimi . ungenyamaza tu ili usije leta mjadala wa kidini hapa. mimi toka babu yangu alikuwa sheikh,mufti na alhaj... wewe maamuma tu unataka jifanya unaifahamu dini na mistari ya kukariri kuliko watu wenye uelewa wa dini? acha huo upuuzi hapa tunaongea kisomi siyo kimaamuma.
Hoja hupingwa na hoja lete aya inayopinga aliyoyatoa huyo member ikiwa wewe unaijua dini kuliko yeye.

Mtu yeyote anweza kuwa alhaji akishaenda ku hiji makka ,mtu yeyote anaweza pia kuwa mufti maana ni nafasi ya uteuzi wa kiserikali na haizingatii elimu ya dini .

So usitumie hayo kama chaka la kujifichia pinga hoja kwa hoja
 
Kuna tofauti kubwa ya kuzungumza na kufikiria mambo kichwani. Haya mambo ungeyetafakari kichwani tu kwa kuwa ndio ulivyo ila kwa kudiriki kuyatamka umeyapa uhai. Yatakusumbua maisha yako yatakuwa na mwisho mbaya tema mate chini piga magoti omba msamaha. .

Nakuombea Mungu akutie nguvu kipindi hiki kigumu unachopitia ili huu mtihani uweze kuuvuka salama. Pole sana ndugu. .
 
Unataka tukushauri umuwekee sumu Mzee ili afe? Aisee hapana.Kumbuka kuwa Mzee hakuomba mwisho wake uwe wa kuanikwa kama mjusi(kama unavyosema).

Hakuna ayuaje mwisho wake. Siku ya mauti yake itakapifika,atakufa.Kikubwa ni kumtanguliza Mungu Kwa kila jambo na kuwa na subra.Pesa inatafutwa.
 
Kuna kipindi pia aliumwaaaaaa.... tukafikia hatua tukasema bora tu arudishe number maana sasa inakuwa changamoto kwetu. akaja akapona.. shida ikawa pale pale. hakuna afadhali akiwa mzima shida akiugua shida. ni msumbufu sana....

sasa this time anaumwa tena. mwezi wa 3 huu amelala tumehamisha hosp zote... tunagharamia ukimwangalia age yake nayo imeenda sana. 90 plus. anataka aendelee kuishi kufanya nini hapa duniani? sasa tunatumia pesa ambazo zingesaidia wajukuu wake kumtibu mgonjwa mbaye kwa kweli ameshakula chumvi ya kutosha hapa duniani. mwisho wa siku tunamwona tu kama chuma ulete. maana kila pesa zetu zinaenda kwenye matibabu yake. meno yake yameshatoka, anaishi kwa shida... anaanikwa tu juani kama mjusi ila bado anataka aendelee kuishi. unajiuliza aishi kufanya nini hapa duniani? mbona alishamaliza kila kitu?

Sasa inafikia kipindi tunasema bora tu akapumzike nasi tupumzike kidogo maana atatufilisi kwa kweli. mimi nimeshauza gari moja. nimechukua mkopo, nimekuwa sasa nina madeni ile mbaya. kwa mabro wengine nao.. ishakuwa shida. maana tulishampeleka mpaka india kipindi flani... wakatwambia kwa huu umri asifanyiwe hayo matibabu maana kinga zake nazo zimekosa nguvu. so alilazwa tu akipewa madawa miezi mitatu. gharama kubwa ilikuja kwetu. akarudi amekuwa tia maji tia maji . kama gari la mkaa trio moja shamba nyingine gereji.

Ila bado mbishi sana, bado anataka atibiwe na kupelekwa hosp za gharama, sasa mzee si atatuacha watoto wake tumefilisika halafu ndo afe? hapo tutakuwa tumefanya nini? nahitaji ushauri wenu kwa kweli hili jambo limenifika hatua nimechoka sana.sipendi unafiki... hii hali ni ngumu sana. maana sasa hata ukiona simu toka kwa ndugu unashindwa kupokea maana huchelewi kuambiwa sasa tuchangie kila mtu atoe 700,000 kuna vipimo na maibabu flani tena yanatakiwa.
Kiukweli vizazi vya sasa hivi ni kama watoto wamepoteza kabisa mapenzi kwa wazazi wao.. yani kupoteza gari inakuuma kuliko afya ya mzee wako??

Ukute yeye alijima sana kukusomesha akitegemea siku moja na wewe utajitoa vile alijitoa kwako.. kimsingi punguza upendo kwenye material things kuliko utu

Hiyo itakusaidia kuishi maisha yenye furaha zaidi.. hata mzee akiondoka nafsi haito kusuta isipokuwa itakuwa baraka kwako mkuu
 
Back
Top Bottom