Gharama za kumuuguza Mzee zinaongezeka. Sisi tumeshachoka kwa kweli. Bora tu achukuliwe

Gharama za kumuuguza Mzee zinaongezeka. Sisi tumeshachoka kwa kweli. Bora tu achukuliwe

mtoto wa Nabii Nuhu ataingia motoni ije kua yy chizi maarifa
Halafu eti anajitapa ni mjukuu wa Mufti. Mjukuu wa Mufti kasahau au hajui kuwa Abu Lahab, ambaye kabashiriwa moto akiwa hai tena katika Qur'an, alikuwa Baba yake mdogo Mtume ﷺ. Baba yake Nabii Ibrahim ('Alayhis Salaam) atakwenda motoni. Ikrima (Radhwiya Allahu 'Anhu) Swahaba Mtukufu huyu baba yake ni Abu Jahl adui mkubwa wa Uislam. Mjukuu wa Mufti kasahau hili. Yeye kuwa Mjukuu wa Sheikh basi kashakuwa Muislam mjuzi na haiwezekani akawa mjinga.

Kumewafaa nini akina Utba bin Rabi'a na akina Abu Jahl kuzaliwa kwao Makkah na wakaishi karibu na al-Ka'aba ilhali walimkataa Mtume ﷺ na wakafa wakiwa ni Washirikina?

Allah atuongoze sisi na yeye mleta uzi katika njia iliyonyooka.
 
Kuna kipindi pia aliumwaaa.... tukafikia hatua tukasema bora tu arudishe number maana sasa inakuwa changamoto kwetu. Akaja akapona. Shida ikawa pale pale. Hakuna afadhali akiwa mzima shida akiugua shida. Ni msumbufu sana.

Sasa this time anaumwa tena. mwezi wa 3 huu amelala tumehamisha hosp zote. Tunagharamia ukimwangalia age yake nayo imeenda sana. 90 plus. Anataka aendelee kuishi kufanya nini hapa duniani? Sasa tunatumia pesa ambazo zingesaidia wajukuu wake kumtibu mgonjwa mbaye kwa kweli ameshakula chumvi ya kutosha hapa duniani. Mwisho wa siku tunamuona tu kama chuma ulete. Maana kila pesa zetu zinaenda kwenye matibabu yake. Meno yake yameshatoka, anaishi kwa shida. Anaanikwa tu juani kama mjusi ila bado anataka aendelee kuishi. Unajiuliza aishi kufanya nini hapa duniani? Mbona alishamaliza kila kitu?

Sasa inafikia kipindi tunasema bora tu akapumzike nasi tupumzike kidogo maana atatufilisi kwa kweli. Mimi nimeshauza gari moja, nimechukua mkopo, nimekuwa sasa nina madeni ile mbaya. Kwa mabro wengine nao.. ishakuwa shida. Maana tulishampeleka mpaka India kipindi fulani. Wakatwambia kwa huu umri asifanyiwe hayo matibabu maana kinga zake nazo zimekosa nguvu. So alilazwa tu akipewa madawa miezi mitatu. Gharama kubwa ilikuja kwetu. Akarudi amekuwa tia maji tia maji kama gari la mkaa trip moja shamba nyingine gereji.

Ila bado mbishi sana, bado anataka atibiwe na kupelekwa hosp za gharama, sasa mzee si atatuacha watoto wake tumefilisika halafu ndo afe? Hapo tutakuwa tumefanya nini? Nahitaji ushauri wenu kwa kweli hili jambo limenifika hatua nimechoka sana. Sipendi unafiki... hii hali ni ngumu sana maana sasa hata ukiona simu toka kwa ndugu unashindwa kupokea maana huchelewi kuambiwa sasa tuchangie kila mtu atoe 700,000 kuna vipimo na matibabu flani tena yanatakiwa.
Umepost JF ili iweje?

Fanya maamuzi magumu (ila kwangu mimi ni mepesi, lakini kwako naona ni magumu).

Miaka 90 inatosha sana. Huyo hata kumbukumbu itakuwa ishapotea kwa hiyo hana cha maana tena cha kufanya duniani. Kwa umri huo itakuwa anaishi kwa madawa. Kwa hiyo cha kufanya ni unaacha tu kumpa hizo dawa. Akifa itaonekana amekufa kwa magonjwa yaliyokuwa yanamsumbua ya uzeeni kwa hiyo hautakuwa na kesi yoyote.
 
Duh hakuna Jambo lolote liwalo laweza kuharalisha kutoa uhai wa binadamu mwenzako, mbaya zaidi mzazi wako,

Mama yangu toka 2013 Ni mgonjwa, Ni wakulisha na kuogesha, maana anajinyea , hivyo Ni wajibu sisi watoto kumswafi, na uzuri zaidi sijawahi sikia hata mtoto mmoja akiwaza kumtoa uhai ili apumzike.

Hayo ni malipo yetu kwa wazazi wetu tungali watoto walikuwa wanatukopesha , Sasa Ni wajibu wetu kulipa,
Pole mkuu,
 
Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa heshima

Hii ni Qur'an inatuamrisha haya
Kumbuka wewe ulivokuwa mtoto huenda ulikuwa msumbufu sana ila wazazi wako walikuvumilia iweje leo wewe huwezi kumvumilia mzazi wako?

Yawezekana angekuwa tajiri mkubwa tu lakini alisacrifice akakulea wewe kwa pesa zake leo hii iweje yeye ndio sababu ya wewe kupatikana lakini unamdhalilisha kiasi hiki.

Najivunia kuwa Muislamu kwani Uislamu umetufunza yote haya.
Mkuu Hapa Muhamedi Aliibia Bibilia

Soma Biblia Takatifu Kitabu Cha Yoshua Mwana Wa Sira Sura ya Tatu Yote.

Chizi Maarifa zingatia Aya ya 12 ya sura hiyo.
 
Umepost JF ili iweje?

Fanya maamuzi magumu (ila kwangu mimi ni mepesi, lakini kwako naona ni magumu).

Miaka 90 inatosha sana. Huyo hata kumbukumbu itakuwa ishapotea kwa hiyo hana cha maana tena cha kufanya duniani. Kwa umri huo itakuwa anaishi kwa madawa. Kwa hiyo cha kufanya ni unaacha tu kumpa hizo dawa. Akifa itaonekana amekufa kwa magonjwa yaliyokuwa yanamsumbua ya uzeeni kwa hiyo hautakuwa na kesi yoyote.
Mmmmh[emoji848][emoji848]

Una watoto?
 
Shukuru Mungu bado unamwona hata kama yote kwenye hali hiyo. Hakika akiondoka utamkumbuka sana. 3 month unalalamika wengine tuliuguza 5 years anafanyiwa kila kitu
walimpeleka mpaka india sasa sijui hela ya kumkatia bima kubwa wanakosa vipi?? kila siku wanachanga helaa.. au ndo wanadhani atakufa soon 😀 😀 😀 mzee nae kagoma kufa
 
Mkuu.. wewe huujui uislamu kuliko mimi. Ungenyamaza tu ili usije leta mjadala wa kidini hapa. Mimi toka babu yangu alikuwa sheikh, mufti na alhaj.

Wewe maamuma tu unataka jifanya unaifahamu dini na mistari ya kukariri kuliko watu wenye uelewa wa dini? Acha huo upuuzi hapa tunaongea kisomi siyo kimaamuma.
Kila mwenye Ilmu yupo mwenye Ilmu zaidi yake. Kama ni mtito wa Sheikh,Alhaji au Mufti HUSTAHILI KUTAMKA MAMENI HAYO KWA MZAZI WAKO ALIYE KUZAA.
 
Angeyasikia haya maneno nina hakika angekufa leo leo...

Huna ustaarabu hata kdg

Usisahau na wewe ni mzee mtarajiwa
Kibinadamu sio rahisi mkuu, haya mambo unaweza kumlaumu lakini likiwa kwako ndio utaelewa anachoongea.

Hawa ni wazee wetu, tunawapenda sana, tunawahudumia kwa dhati ya mioyo yetu na uwezo wetu, lakini kuna sehemu ubinadamu unachukua nafasi yake, madhaifu yetu yanadhihirika pale unapoona kazi unayoifanya haina faida(mzee haponi na rasilimali zinaisha). Achana na kuuguza, ni kazi kuliko kazi ila tummies nguvu, tusimlaani kwa sababu ndio jukumu lake kwa sasa.
 
Pesa inatafutwa na inakuja Tu. Mtendeeni stahili yenu huyo baba kama alivyojitoa katika maisha yake.
Hongera kwa kuwa na mzazi wa MIAKA 90+ wengine waliondoka mapema tunatamani warudi.
Huyu kijana sijajua imani ya dini yake ila nadhani anahitaji kuisoma dini yake sana
 
Back
Top Bottom