Gharama za kumuuguza Mzee zinaongezeka. Sisi tumeshachoka kwa kweli. Bora tu achukuliwe

Kuna kipindi pia aliumwaaa.... tukafikia hatua tukasema bora tu arudishe number maana sasa inakuwa changamoto kwetu. Akaja akapona. Shida ikawa pale pale. Hakuna afadhali akiwa mzima shida akiugua shida. Ni msumbufu sana.

Sasa this time anaumwa tena. mwezi wa 3 huu amelala tumehamisha hosp zote. Tunagharamia ukimwangalia age yake nayo imeenda sana. 90 plus. Anataka aendelee kuishi kufanya nini hapa duniani? Sasa tunatumia pesa ambazo zingesaidia wajukuu wake kumtibu mgonjwa mbaye kwa kweli ameshakula chumvi ya kutosha hapa duniani. Mwisho wa siku tunamuona tu kama chuma ulete. Maana kila pesa zetu zinaenda kwenye matibabu yake. Meno yake yameshatoka, anaishi kwa shida. Anaanikwa tu juani kama mjusi ila bado anataka aendelee kuishi. Unajiuliza aishi kufanya nini hapa duniani? Mbona alishamaliza kila kitu?

Sasa inafikia kipindi tunasema bora tu akapumzike nasi tupumzike kidogo maana atatufilisi kwa kweli. Mimi nimeshauza gari moja, nimechukua mkopo, nimekuwa sasa nina madeni ile mbaya. Kwa mabro wengine nao.. ishakuwa shida. Maana tulishampeleka mpaka India kipindi fulani. Wakatwambia kwa huu umri asifanyiwe hayo matibabu maana kinga zake nazo zimekosa nguvu. So alilazwa tu akipewa madawa miezi mitatu. Gharama kubwa ilikuja kwetu. Akarudi amekuwa tia maji tia maji kama gari la mkaa trip moja shamba nyingine gereji.

Ila bado mbishi sana, bado anataka atibiwe na kupelekwa hosp za gharama, sasa mzee si atatuacha watoto wake tumefilisika halafu ndo afe? Hapo tutakuwa tumefanya nini? Nahitaji ushauri wenu kwa kweli hili jambo limenifika hatua nimechoka sana. Sipendi unafiki... hii hali ni ngumu sana maana sasa hata ukiona simu toka kwa ndugu unashindwa kupokea maana huchelewi kuambiwa sasa tuchangie kila mtu atoe 700,000 kuna vipimo na matibabu flani tena yanatakiwa.
Hahahaha
Mkuu naona laana imeanza kazi kabla haijasomwa.kwako.

Jinsi ya khiepuka toa hiyo 709k akatibiwe
 
utahudhunika? ndo lugha gani hiyo? acha unafiq... mzee wa miaka 97 amelazwa ICU anatumia gaskwa week 3 unajua gharama yake kwa siku? bado alikuwa ameshazeeka hajitambui, hana kumbukumbu yoyote. ulitaka aendelee kuishi akiteseka? anatumia mtungi wakati wote kupumua, anatumia mirija kula na kukojoa? wewe una akili au unajitia unafiq tu?
Kama aliweza kuuza mali zake ili awahudumie...imekuaje mshindwe kuuza mali zenu kumuhudumia...? Hamjamtendea Haki. Kifo kisikie TU ndugu yangu ukitaka habari zake angalia hata documentary za Near-death experience. Mimi nilishawahi kuumwa Hadi nikawa nahisi nitakufa muda sio mrefu lakini Bado maisha nilikuwa nayahitaji.

Kila mtu na mtazamo wake pengine wenzetu wazee amuwapendi.​
 
Ningekukutukana Ila basi tu siyo malezi yangu. Nadhani huyo siyo baba yako mzazi, angekuwa baba yako usingetoa kauli ya kumuacha afe eti umechoka. Vaa huo uhusika km wewe ndo watoto wako wangekuwa wanasema hivyo. Unakera sn bora ungetoa thread ya kuomba ushauri wa maan siyo hii.
 
Unaposema bado anataka kuishi unamaanisha nini[emoji28][emoji28]

Kwani analazimishaje kuishi? Hakuna hila mtafanya ifupishe safari?

Kimsingi sioni sababu ya mtu kuishi umri mrefu kama huo hata mimi sitaki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama aliweza kuuza mali zake ili awahudumie...imekuaje mshindwe kuuza mali zenu kumuhudumia...? Hamjamtendea Haki. Kifo kisikie TU ndugu yangu ukitaka habari zake angalia hata documentary za Near-death experience. Mimi nilishawahi kuumwa Hadi nikawa nahisi nitakufa muda sio mrefu lakini Bado maisha nilikuwa nayahitaji.

Kila mtu na mtazamo wake pengine wenzetu wazee amuwapendi.​
Ndugu kuzaa siyo kupata,Mungu amsamehe tu mleta mada.
 
Usimuache utabarikiwa ushangae. Nilimuuguza babu yangu miaka 2 ilikuwa ameumwa sana na wanaye hawamjali walimchoka kama wewe ulivyochoka!

Baada ya kuumuuguza Hadi kufulia, alipofariki tu nikashangaaa mambo yote yamerudi fasta tena mazuri kuliko mwanzo.
Mleta mada kwa imani ishu humu.
 
Hii thread imenifanya nicheke saana, mleta mada pepo utaisikia.

Ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha
 
So wachina , wahindi,wajapani,Imani za mizimu za kiafrika na sie tujivunie vya asili na sio huyu anajivunia dini aliyoletewa na mashua Mana Hawa jamaa wasingekuja sijui angejivunia Nini na ilhali wakamuachia dini Ila wakamuibia madini na kumuuza utumwani wakampatia Imani ya kumpooza akili yake itulie.
Namie najivunia kuwa mwafrika na dini yangu ya kiafrika Mana tulikuwa na dini zetu kabla ya wageni hawajaja afrika miaka ya 1200 kurudi nyuma.
Najivunia kuwa Muislamu kwani Uislamu umetufunza yote haya.
 
Bora dingi angepiga nye***o.
Mzee, vitu kama hivi hatuleti hadharani. Najua unawaza sana, unaumia mno.
Mambo kama haya unakufa nayo kiume. Ni kama umechapiwa mkeo na huwezi kumuacha (ni mfano tu).
Kuweka hapa habari hizi ni kukosa utu na kutomthamini mzazi wako.

Kama huna guts za kugoma kutoa pesa za matibabu (probably unaogopa kupata radhi ama kuonekana na familia wewe ni wa hovyo) basi ungetulia kimya hivyo hivyo.

Mwenyezimungu akupe subira.
 
Mkuu.. wewe huujui uislamu kuliko mimi. Ungenyamaza tu ili usije leta mjadala wa kidini hapa. Mimi toka babu yangu alikuwa sheikh, mufti na alhaj.

Wewe maamuma tu unataka jifanya unaifahamu dini na mistari ya kukariri kuliko watu wenye uelewa wa dini? Acha huo upuuzi hapa tunaongea kisomi siyo kimaamuma.

Chizi
 
Kuna kipindi pia aliumwaaa.... tukafikia hatua tukasema bora tu arudishe number maana sasa inakuwa changamoto kwetu. Akaja akapona. Shida ikawa pale pale. Hakuna afadhali akiwa mzima shida akiugua shida. Ni msumbufu sana.

Sasa this time anaumwa tena. mwezi wa 3 huu amelala tumehamisha hosp zote. Tunagharamia ukimwangalia age yake nayo imeenda sana. 90 plus. Anataka aendelee kuishi kufanya nini hapa duniani? Sasa tunatumia pesa ambazo zingesaidia wajukuu wake kumtibu mgonjwa mbaye kwa kweli ameshakula chumvi ya kutosha hapa duniani. Mwisho wa siku tunamuona tu kama chuma ulete. Maana kila pesa zetu zinaenda kwenye matibabu yake. Meno yake yameshatoka, anaishi kwa shida. Anaanikwa tu juani kama mjusi ila bado anataka aendelee kuishi. Unajiuliza aishi kufanya nini hapa duniani? Mbona alishamaliza kila kitu?

Sasa inafikia kipindi tunasema bora tu akapumzike nasi tupumzike kidogo maana atatufilisi kwa kweli. Mimi nimeshauza gari moja, nimechukua mkopo, nimekuwa sasa nina madeni ile mbaya. Kwa mabro wengine nao.. ishakuwa shida. Maana tulishampeleka mpaka India kipindi fulani. Wakatwambia kwa huu umri asifanyiwe hayo matibabu maana kinga zake nazo zimekosa nguvu. So alilazwa tu akipewa madawa miezi mitatu. Gharama kubwa ilikuja kwetu. Akarudi amekuwa tia maji tia maji kama gari la mkaa trip moja shamba nyingine gereji.

Ila bado mbishi sana, bado anataka atibiwe na kupelekwa hosp za gharama, sasa mzee si atatuacha watoto wake tumefilisika halafu ndo afe? Hapo tutakuwa tumefanya nini? Nahitaji ushauri wenu kwa kweli hili jambo limenifika hatua nimechoka sana. Sipendi unafiki... hii hali ni ngumu sana maana sasa hata ukiona simu toka kwa ndugu unashindwa kupokea maana huchelewi kuambiwa sasa tuchangie kila mtu atoe 700,000 kuna vipimo na matibabu flani tena yanatakiwa.
Jiweke wewe mahali pake
"Everybody wants to go to heaven but no one wants to die" PETER TOSH ( The Wailers)
 
Back
Top Bottom