DOKEZO Gharama za Lipa namba ziwekwe wazi kama miamala mingine

DOKEZO Gharama za Lipa namba ziwekwe wazi kama miamala mingine

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mtandao ya simu imerahisisha huduma ya kulipa vitu mbalimbali ikiwemo malipo ya serikali na biashara binafsi. Ni kawaida kwa sasa kukuta biashara ina LIPA NAMBA ambapo mtu anaweza kulipa kwa namba hiyo.

Hata hivyo katika kutumia lipa namba, kuna gharama ambayo mteja anakatwa, lakini gharama hizi haziko wazi kama gharama za kutuma, kupokea na kutoa fedha, ambazo makato yake utaona yameandikwa.

Naona ni muhimu mitandao yote inayosapoti lipa namba iweke gharama za kila muamala wazi ili mteja achague kutumia lipa namba au kulipa kwa fedha taslimu.

Nawasilisha, nikiwa nimekasirika kwa kukatwa 800Tsh kwa kufanya malipo ya Tsh 15,000

Kwa wenzetu wa Kenya gharama za Lipa Namba ziko wazi, angalia hapa https://www.safaricom.co.ke/images/Downloads/paybill-standard-tariff.pdf

View attachment 2888087
Umelipia bidhaa gani mkuu
 
Hii kitu siipendi hata kidogo, siku hizi pia imewafanya mawakala kuhamia huku na kuzitelekeza till zao, unaenda kwa wakala unamweleza naomba kutoa anakulazimisha utoe kwa lipa ambapo kule kwenye mtandao husika unakatwa halafu na wakala nae anakukata(kwa makubaliano) wizi mtupu!
 
Ukitumia App inaonyesha makato
Yeah App ni nzuri zaidi inaonyesha makato lkn watu wengi hawatumii App wanatumia njia ya kawaida sasa kuna baadhi ya mitandao ukilipa kwenda mtandao mwingine hawaonyeshi makato ila utayaona tu ujumbe mfupi wa sms
 
Hakuna sababu ya mteja kununua bidhaa kwa lipa namba na kukatwa hela. Huu ni upuuzi. Lakini pia hakuna sababu ya wateja kutoa hela kwa kutumia lipa, na wakati kuna ule mfumo wa kawaida.
 
Sahivi voda wanamkata mwenye Line ya Lipa akitaka kutoa kwa Wakala
 
Sahivi voda wanamkata mwenye Line ya Lipa akitaka kutoa kwa Wakala
Navyo jua ni ndani ya 24 hours ukitoa mala moja ukatwi ila uki toa mala ya pili ndani ya hizo 24 hrs ndio una katwa ..au wame badili ? Na kuna lipa no. Ambazo mteja aki lipa hakatwi hata tzsh 1
 
Navyo jua ni ndani ya 24 hours ukitoa mala moja ukatwi ila uki toa mala ya pili ndani ya hizo 24 hrs ndio una katwa ..au wame badili ? Na kuna lipa no. Ambazo mteja aki lipa hakatwi hata tzsh 1
Sahivi hata utoe mara1 unachinjwa
 
Mbona nimetoa 5M na sijakatwa? voda au wanaangalia watu na watu
Voda hawakati kabisa mchezo wa kukata wanao Airtel,hao jamaa lipa namba yao niliitumia mara moja sijaja kurudia tena.
 
BINASFI NAPENDEKEZA LIPA IFUTWE AU IWE KWA WAFANYABIASHARA PEKEE NA IFUNGIWE KWA MAWAKALA WOTE YAANI IWE KAMA MWANZO MFUMO WA LIPA UNA CHANGAMOTO SANA KWA MAWAKALA
 
BINASFI NAPENDEKEZA LIPA IFUTWE AU IWE KWA WAFANYABIASHARA PEKEE NA IFUNGIWE KWA MAWAKALA WOTE YAANI IWE KAMA MWANZO MFUMO WA LIPA UNA CHANGAMOTO SANA KWA

BINASFI NAPENDEKEZA LIPA IFUTWE AU IWE KWA WAFANYABIASHARA PEKEE NA IFUNGIWE KWA MAWAKALA WOTE YAANI IWE KAMA MWANZO MFUMO WA LIPA UNA CHANGAMOTO SANA KWA MAWAKALA
Shida ni kwamba hao wafanyabiashara ni mawakala pia, mawakala wengi sikuhizi wanakuwa na biashara nyingine so inakuwa ngumu kuzitenganisha. Halafu kumbuka wateja ndio wanachochea mawakala kutafuta line za Lipa, maana kwa sasa wateja wengi wamehamia huko, wakala ukiwa hauna line ya lipa utakuwa unapishana na pesa
 
Mimi pia nakazia. Kama mtoa mada alivyosema, huduma ya LIPA NAMBA ni wizi tu, kwani wakala anakukadiria gharama atakayokutoza huyu ni tofauti na wakala mwingine. Sasa mteja, unatafuta wapi wakala mzuri ambaye hana makato makubwa? Nyakati nyingine mnakubaliana kwenye pesa yako.

Na patwa na gazabu pindi wakala unapofika ofisini kwake anakwambia utumie LIPA NAMBA. Unamwambia, "Mimi LIPA, sitaki kutumia." Unajibiwa, "Huduma hiyo haipo."

Issue ya LIPA NAMBA ipo shida sehemu, ila mtu ukiwa na haraka zako huwezi kuelewa. Mimi LIPA NAMBA nimeikataa kutumia. Bora pesa yangu nigawane na wenye mtandao wao na nchi yangu.
😂😂😂HAO UNAOWAGAWIA NDIO WALIOLETA SHIDA ZOTE HIZI. BURGAIN NA WAKALA ILI VIJANA WAPATE KULA MKUU KWASABABU BAADA YA SERIKALI KULETA TOZO BIASHARA YA UWAKALA WA MITANDAO YA SIMU IMEKUWA NGUMU SANA. WABARIKIKIWE WALIOLETA LIPA NAMBA NDIO IMELETA AHUENI KWENYE HII BUSINESS
 
Shida ni kwamba hao wafanyabiashara ni mawakala pia, mawakala wengi sikuhizi wanakuwa na biashara nyingine so inakuwa ngumu kuzitenganisha. Halafu kumbuka wateja ndio wanachochea mawakala kutafuta line za Lipa, maana kwa sasa wateja wengi wamehamia huko, wakala ukiwa hauna line ya lipa utakuwa unapishana na pesa
Kweli kabisa mkuu. Mteja anakuwa hakatei pesa nyingi hata wakala nae kale kakamisheni kanaongezeka halafu hakuna masuala ya kusubiri mwisho wa mwezi ni papo kwa papo unachukukua chako mapema.
 
Cashless economy ngumu kwa Tz sababu ya tozo na makato yasiyo na kivhwa na mkia
 
Back
Top Bottom