Gharama za michango ya harusi na sintofahamu ya chakula

Kila mtu akifanya kama wewe itakuaje? 😅
 
Bado tunasikitika chakula kidogo na bia hazikutosha mara tayari maharusi washaachana.....mi sichangii sherehe kwakweli niitwe tu kula ila mchango sitoi
Tatizo kiasi kikubwa cha michango kinaenda kwenye mapambo, ukumbi, mc na mazagazaga mengine ambayo hayana maana. Watu wanahitaji chakula na vinywaji tu, hivyo ndo vitu muhimu
 
Umechangia 50k+ Afu unakwenda kugombania wali + samaki sahani moja kwa mama ntilie ni buku tatu na bia ya 2500 🔥
 
Tatizo kiasi kikubwa cha michango kinaenda kwenye mapambo, ukumbi, mc na mazagazaga mengine ambayo hayana maana. Watu wanahitaji chakula na vinywaji tu, hivyo ndo vitu muhimu
Kabisa raha ya sherehe tuleee tunywee hadi tuzikimbie, mapambo hayana ishu kwanza hata tukikaa kwenye mabenchi sawa tu.
 
Hatichangi ili tukale, maana kwa hela ya mchango unaotoa waweza ingia mgahawa wa maana tu ukala mlo mmoja wa nguvu.
 
Ila mi nipo tofauti sipendagi sherehe, yani sipendi hayo masham sham naonaga naboreka tu.... Hadi niwe na mood sana au mtu nnaempenda sana ndo ntajitahidi nifike ila hivi hivi sipendi siendi
Mie sipendi pilika pilika. Niende nikakae ninywe nile niondoke. Nione watu wakiserebuka ndo furaha yangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…