Dah sijui tunaelekea wapi, hizi huduma zilipaswa kutupa unafuu wananchi kufanya miamala bila usumbufu lakini imekua ujambazi hasa hasa.
Niliwahi kuhamisha laki mbili kutoka Benki kwenda mpesa nikakatwa 11,000/= hapo bado sijakutana na Makato ya mpesa, nikajikuta nakatwa karibu 16000/= kupata 194,000 sijui, nikabaki nimeduwa.
Ukitoa hata 40000 wanakata 6000/= Makato ya mpesa/tgopesa/Airtel money utakutana nayo juu kwa juu.
Jana nimenunua vocha ya 2000 kutoka mobile banking naangalia statement wamekataa 700/= anyway sawa tu IPO siku kitaeleweka tu maana washatuona misukule.
Nimefuta app zao zote ila najua hata kwenye atm ni yaleyale.