Gharama za 'Semina ya Wataalamu wa Nje' wa Mh. Sitta

Gharama za 'Semina ya Wataalamu wa Nje' wa Mh. Sitta

Lupweko

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2009
Posts
23,566
Reaction score
24,891
Wakuu, Mh. SS, pamoja na mambo mengine, amesema kutakuwa na Semina itakayoongozwa na wataalamu wa nje ya nchi yetu kwa wajumbe wa Bunge Maalum. Maswali yangu ni mengi kuliko majibu.
1. Amechaguliwa juzi tu, aliwaarifu lini hao wataalamu kuwa wanatakiwa kutoa semina Tanzania?
2. Alifuata taratibu za zabuni kuwapata wataalamu hao?
3. Gharama za kuwalipa hao wataalamu ni shilingi ngapi?
4. Hakuna mianya ya ufisadi au 10% katika mchakato wa kuwapata na kuwalipa?

Tufanye rejea katika thread hii: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/29351-ni-ufisadi-wa-spika-samwel-sitta-45.html
 
Hahahaaaaa hili la "kufuata taratibu za zabuni kuwapata wataalamu hao" limenipa raha sana mkuu!!!!
 
Uko sahihi mkuu.Hivi kumbe hata hawa wajumbe si wataalam?Kuna haja gani ya kuingia gharama yote hiyo kuwalipa posho yote hiyo ni kwanini hao wataalam wasingefanya hiyo kazi kisha wananchi wapigie kura ya kuipitisha tu?
 
hahaha..
hii nchi inafurahisha kwa mengi
 
Kweli TZ ni kichaka cha waizi.Usishangae ikaanzishwa kodi ya mke.Ukioa tu unaripoti TRA.Tehe tehe!
 
Huyu mzee ataleta tena mada ya kutengenezewa SIWA ili apige pesa juu kwa juu. Ni hatari sana!
 
Semina ya nini? Rasimu ile inahitaji maboresho tu na sio mabadiliko kwani yale ndiyo matakwa na maoni ya Wananchi walio wengi walioyatoa kwa tume. Wasitubabaishe. Labda wawaite tume ya Warioba wawape semina!
 
Hata mimi nimeshangaa wataalamu wa nje kuwaleta Sitta wakati kachaguliwa jana tu,haow wataalamu wa nje sisi watatusaidia kitu gani kipya ambacho wataalamu wetu wa hayo mambo kama akina Prof.Shivji,Dr Mwakyembe hawakijui au ndio ufujaji wa kodi zetu,ina maana alishajua kuwa lazimaatakuwa Mwenyekiti wa Bunge la Katiba na akaanza kufanya mandalizi ya kuwaleta hao watu,Kweli Sitta ni ku sita kumchagua kwa kila uongozi anaotaka,Mungu anazidi kutuonyesha tabia ya Sitta,na Mungu ni mkubwa katuonyesha mapema kabla ya 2015,jamani Mungu ni mkubwa hasindwa kuonyesha ubaya wa mtu mbaya kwa waja wake
 
uko wapi uzalendo kwa viongoz wa tanzania?eti kuna watu toka visiwan na tanganganyika wataelezea historia ya mungano kwa faida ipi?nan asiyejua historia hiyo toka shule ya msingi?!
 
Naanza kuamini kuwa nchi yetu inaongozwa tokea nje.
 
Back
Top Bottom