Gharama za Ujenzi kwa Nyumba za ‘Contemporary’ Vs ‘Traditional’ Roof

Gharama za Ujenzi kwa Nyumba za ‘Contemporary’ Vs ‘Traditional’ Roof

Hilo Gutter dogo kwa 3 bedrooms? Howtf?
IMG_20220527_143214.jpg
IMG_20220529_094325.jpg
 
Tafuta fundi mtaalam wa kupaua hizi contemporary, siyo fundi wa kupaua tu. Na hakikisha kwenye makutano ya paa na tofali mnaweka Bitumat Synroof HB+Bitumat fabric, hii ni muhimu kuliko hata hiyo kuflash.

Na bitumen au bitumat kazi yake kuzuia kutu na kuoza Kwa bati sindio mkuu
 
Tatizo lipo kwa mafundi wenyewe! Mnatoa bei za kukomoana! Nani alikuambia ww kunijengea nyumba yangu ndio unaponea kutatua matatizo yako yote? Muwe reasonable bana mfyuuuuu 😡!
Sitasahau fundi alinaimbia kupiga plasta tu nyumba ya vyumba vi3 milioni 4
 
Tatizo lipo kwa mafundi wenyewe! Mnatoa bei za kukomoana! Nani alikuambia ww kunijengea nyumba yangu ndio unaponea kutatua matatizo yako yote? Muwe reasonable bana mfyuuuuu [emoji35]!
Ni Uzi wa zamani Ila nikichangia maada sio tatizo.
Kuna jamaa mmoja Tanga, alikwepa gharama ya wataalam Kama 2M hv, akatoa kazi kwa fundi sababu alisema anaweza. Fundi akaharibu kazi kwa kuchakachua ratio za materials kuanzia nondo, cement ya plaster, n.k (maana ni ghorofa). Nyumba ilibomolewa mpaka slab na kuanza upya. Marekebisho yote yamekula around 30M.
So, endeleeni kukimbia wataalam.
NB: sio kila fundi ni mwizi/sio mwaminifu kitaaluma na kipesa pia.
 
Sure mkuu unamwita tu mtaalamu anakusaidia mahesabu kwa mzigo huo wa slab marefu na mapana kutokana na nyumba yako utahitaji nguzo ngapi nondo ngapi mm ngapi maana si ghorofa chap unasahau kbs hizi mbwembwe za slope sijui material gani na gani ni temporary tu unaweza jikuta material yote hayo plus bati mbao gati unachosevu ni kdg sana.ukiweka zege umemaliza ila huu mpango mwingine baada ya miaka kadhaa lazima uvue uvalishe tena,hili zoezi utarudia na kurudia kila baada ya muda,ukija kujumlisha cost baada ya kipindi flani unaweza ukakuta umeenda maradufu ya gharama ya awali,tukumbuke material hupanda bei kila siku pia.Leo si sawa na jana.
Pambavu zao kabisa, kelele zote za kwamba nyumba hizo zinavuja sana kumbe hawaweki zege juu? Mimi kila nikisoma na kusikia habari za kuvuja huwa najiuliza sana, how comes zege la nyumba hizo tu ndiyo livuje? Mbona maghorofa hatuyasikii yakivuja?
 
Nimejenga hiyo contemporary baada ya mke na watoto kutaka mtindo huo japo niliwatahadhalisha kwa uzoefu wa kusikia uvujaji wake....nikakubaliana nao ila iwe ni ya mapaa mawili tuu na imejengwa na tukakubaliana hatuweki gypsum board mpaka msimu wa masika upite ili tuone wapi na wapi kuna vuja na nini cha kufanya kudhibiti huo uvujaji
Masika ndo hii,uvujaji kiasi (kwa matone)upo kwenye misumari km sehemu tano,fundi aliipiga kwa pembeni ya mbao,gutter (mfereji)unakuwa na unyevu kiasi kuna sehemu mpaka kunadondosha matone ya maji na kunakuwa na unyevu kwenye tofali za juu kulipochimbiwa bati (kuna sehemu humu nimesoma kuwa ni kosa kuchimbia bati)
Kwa muktadha huu naombeni ushauri wa nini cha kufanya au nani(experts)wa kuwaona sio mafundi mchundo
Kwahio ulifuata ushauri wa mke na watoto?
 
Back
Top Bottom