Gharama za Ukataji Passports/Hati ya kusafiria nje ya nchi

THE BULL

Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
23
Reaction score
12
Jamani wadau,

Naomba mnisaidie kujua gharama za kupata hati ya kusafiria nje ya nchi.

shughuli yake c ndogo ila kikubwa usitumie wale vishoka itachukua mda mrefu sana kuliko kuifuatilia ww mwenyewe taratibu! kihalali inaweza chukua 2weeks ila ukitumia wale jamaa itachukua hata 3 months coz wata sababisha uone zoezi ni gumu ili wakutoke zaidi
 
Asante sana mkuu nimekusoma
nitajitahidi kufanya hivyo ili niweze fanikisha hili jambo.
 
Kama upo dar ni rahisi sana ukienda mwenyewe ofisini na ukiwa na viambatanishi vyote wiki tu unapata pasport.
 
Mkuu huijui hii Tz, kweli gharama yake ni 50,000,lakini huo mzunguko wake, utaamua kutafuta shortcuts tu, ambayo ndio gharama za ziada zinatumika. We wanakuambia uende kijijini alikozaliwa baba yako, atafute mtu aliyeshuhudia baba yako akizaliwa?!!!! mi nilichoka, ndio nikajiongeza siku 3 tu nikaipata. we unafikiria mtu anakwambia nimetumia laki 3,kupata passport anatania?? labda kama unaumwa hivyo unahitaji kwenda kutibiwa nje, ndio wanaweza kukuonea huruma, ila lazima upigwe nyundo hata buku 20 ya maji. ukiwa na pesa yako hata ndani ya masaa 2 unaipata tu.
 
Tafuta shirika lolote la kidini ambalo wanafanyaga hija nje ya nchi.... ukijipenyeza na kuwatumia wao wala hutosumbuka utaipata kiulainiiiiii....... Mwenzako nilitumia 50,000 tu kuipata kwa njia hii!
 
Jamani wadau,

Naomba mnisaidie kujua gharama za kupata hati ya kusafiria nje ya nchi.
Inategemea na mkoa ulipo, Ukiwa mikoan inachukua hata mwezi bei 50k ila dar siku 3 unaweza pata...Pia huo mkoa wanapenda penda rushwa kama ni ivo utaliwa sana hadi uipate, eg uhamiaji Arusha wanapenda sana rushwa, unapigwa chajuu na immigration officer mwenyewe sio kishoka wala nini unless uunganishwe na mkubwa
 
Hivi katika hali ya kawaida wanatoa wapi ujasiri wa kudai vyeti vya wazazi?

Mkuu hali ya kawaida unaijua wewe na hali yako. Wao wako kazini na hivyo vyeti ni mojawapo na viambatanishi vya wewe kupata hiyo pasipoti. Sasa wewe ifanye hii siasa.
 
Duuh,sisi ambao wazazi wetu walizaliwa chini ya miti huko maporini kazi tunayo.

Sent from my HUAWEI Y330-U11 using JamiiForums mobile app
 
Hivi katika hali ya kawaida wanatoa wapi ujasiri wa kudai vyeti vya wazazi?
Cheti cha mzazi angalau mmoja kinahitajika kuthibitisha uraia wa wazazi wako. Kama wazazi hawana cheti cha kuzaliwa kunakile kiapo Mahakamani mwanasheria anatoa 10k nadhani... Iyo form hadi ipitishwe kutengeza passport inapitiwa na maofficer kama watatu, ukikosa document hata moja wanayoihitaji unapigwa chini
 
Duuh,sisi ambao wazazi wetu walizaliwa chini ya miti huko maporini kazi tunayo.

Sent from my HUAWEI Y330-U11 using JamiiForums mobile app

Zipo taratibu zinazofuatwa. Hofu ondoa utaelekezwa nini cha kufanya. Kwani utahitajika upeleke viapo vya kuzaliwa na kufa vya wazazi.Kuna nchi kupata pasipoti kwa raia wao ni shida sana Mfano hapo Congo tu achilia mbali nchi kama India.
 
Cheti cha mzazi angalau mmoja kinahitajika kuthibitisha uraia wa wazazi wako. Kama wazazi hawana cheti cha kuzaliwa kunakile kiapo Mahakamani mwanasheria anatoa 10k nadhani... Iyo form hadi ipitishwe kutengeza passport inapitiwa na maofficer kama watatu, ukikosa document hata moja wanayoihitaji unapigwa chini

kiongozi muongezee na vitu kama stamp duty ambazo zinauzwa TRA. Sasa hapo ndipo ataona mzunguko pasipoti inatoka uhamiaji stamp duty TRA.
 
Zipo taratibu zinazofuatwa. Hofu ondoa utaelekezwa nini cha kufanya. Kwani utahitajika upeleke viapo vya kuzaliwa na kufa vya wazazi.Kuna nchi kupata pasipoti kwa raia wao ni shida sana Mfano hapo Congo tu achilia mbali nchi kama India.
Thanks,mkuu

Sent from my HUAWEI Y330-U11 using JamiiForums mobile app
 
Inategemea na mkoa ulipo, Ukiwa mikoan inachukua hata mwezi bei 50k ila dar siku 3 unaweza pata...Pia huo mkoa wanapenda penda rushwa kama ni ivo utaliwa sana hadi uipate, eg uhamiaji Arusha wanapenda sana rushwa, unapigwa chajuu na immigration officer mwenyewe sio kishoka wala nini unless uunganishwe na mkubwa
Mbona mimi Arusha hapo hapo nilipata kihalali kabisa bila hata usumbufu na siku ilipoletwa walipiga simu kwa ndugu yangu nikaifata bila hata kuombwa senti tano,ila nilimpa yule aliyeshughulikia shs 10,000/- kama asante kwa kuwa hata yeye alitumia muda wake kupiga simu kunitaarifu kuwa pass yangu imeshafika,siku hizi hamna usumbufu sana.
 
Back
Top Bottom