Gharama za umeme: Rais Samia muwajibishe Waziri Kalemani na uongozi wote wa TANESCO

Gharama za umeme: Rais Samia muwajibishe Waziri Kalemani na uongozi wote wa TANESCO

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Posts
49,282
Reaction score
117,244
Nipo kwenye rekodi hapa ya kumtetea waziri Kalemani huko nyuma lakini leo naomba Rais Samia amfukuze tena ikibidi haraka Sana huyu waziri.

Kwa mujibu wa maagizo aliyowapa TANESCO waziri Kalemani anataka sasa karibu watu wote Tanzania nzima wakitaka kuunganishiwa Umeme walipe Elfu 27 tu bila kujali gharama halisi za kuvuta umeme kwa mtu huyo anasema Serikali imepitisha hela ya ruzuku kwa TANESCO.

Sasa hebu twende taratibu huku tunatumia akili kidogo. Mtu anajenga ghorofa lenye apartments 20. Mfano Masaki huyu mtu sio masikini why asigharamie gharama halisi?

Why TANESCO ijinyime mapato Kwa kutoa ruzuku hadi Kwa matajiri wa Masaki Hadi Upanga?

Anaejenga Fremu 20 Mbeya mjini au Dodoma mjini? Why alipe elfu 27 wakati TANESCO wananunua hizo Mita moja laki moja 20?

Kwanza hii tafsiri yake ya Mjini kuwa ni Ilala City Center kaitoa wapi?

Anajua maana ya Urban and Rural? Anajua history ya kuanzisha REA?

Why anakuja kuleta siasa za kutafuta umaarufu Kwa nguvu Kwa gharama za kuiua TANESCO??..kama mpaka sasa Tanesco haipati Faida inaishi kwa ruzuku. Why anakuja na maamuzi ya kupunguza mapato kwa TANESCO?

Mapato ya service charge yamefutwa. Mapato ya kulipisha fomu yamefutwa. Sasa hata gharama za kuvuta Umeme iwe Upanga au Masaki ziwe za REA kweli?

Huyu waziri anafanya siasa za hatari za kujifanya 'mtetezi wa wanyonge aliebaki'. Itasababisha TANESCO huko mbeleni ishindwe kujiendesha wala kulipisha wateja wake gharama halisi za Umeme.

Anataka aonekane yeye alipokuwepo gharama zilishuka wakati si kweli.

Gharama zipo zile zile anachofanya ni kutumia ruzuku ya Serikali ambayo sio ya uhakika na haina guarantee ya kuwepo kila mwaka.

Tayari foleni ya umeme unaohitaji nguzo TANESCO inafika miezi sita sasa na bado waziri anaongeza tatizo badala ya kupunguza.

Utaratibu wa REA ulikuwepo kabla ya hata Kalemani hajawa waziri. REA ibaki REA kwa wananchi wa vijijini na wenye vipaji vya chini.

Kulazimisha REA itumike nchi nzima ni siasa za kufeli na kuja kulaumiana huko mbele wakati huduma itakapokuwa ngumu kupatikana baada ya mapato kushuka REA hadi Masaki na Sinza?

Wenye Bar na mafremu 40?

Wenye ghorofa zenye apartment 40?

Hi ruzuku ni pesa ambayo wananchi hasa masikini wanachangia. Why itumike kufaidisha hadi matajiri kwa siasa tu?

Viongozi wa TANESCO kuanzia Bodi hadi CEO wake wote wapigwe chini kwa kukubali maagizo haya ya huyu waziri...

Watu wenye uwezo walipie gharama halisi za umeme.

REA ibaki vijijini na kwa watu masikini.
 
Ukiunganisha wengi utapata mapato.

Tanesko itakufa kwa kutegemea mapato ya kuunganisha umeme.

Kinachotakiwa wateja waunganishiwe haraka ili walipie bili na kutumia(hapa ndipo mapato yalipo)

by the way umeme huo wa 27000 ni single phase
 
Ndo kuvutia uwekezaji huko kaka relax, kuwa Tajiri hakumfanyi mtu apandishiwe tu bei. Bei sawa kwa wote. Balance of payment inafanyika kwenye kodi sio Tanesco
 
Kama Watu walikuwa wanalipa around laki 3 na inawachukuwa Tanesco miezi zaidi ya Mitatu kuja kukuunganishia huduma ya Umeme, sasa hii elf 27 tutarajie kuunganishiwa Umeme zaidi ya Miezi sita baada ya kulipia!
 
Hili shirika linaendeshwa kisiasa, mtu kajenga nyumba anashindwaje gharamia mita


Na sasa anataka mtu hata aliejenga fremu 40 za biashara nae alipe elfu 27.
Au ghorofa Upanga la apartment 40 alipe elfu 27.. imagine that
 
Yani hilo tu lipelekee kumfukuza waziri?

Basi atafukuza wengi kama ni hivyo!

Labda yawepo makosa/mapungufu mengine mengi nyeti ambayo waziri ameonekana kushindwa ku improve performance yake ndipo unaweza kuomba afukuzwe lakini kama ni hilo tu bora awaite waziri na mgt ya Tanesco awaulize wajadiliane kisha wafikie muafaka kwa manufaa ya Umma .
 
Hakukua na haja ya kujifanya aggressive namna hio ungeandika vizuri kwa kutulia ungeeleweka sana

Watu wachache sana watakuelewa.

Impact ya hiyo kitu utakuja mbeleni, pale ambapo ruzuku hakuna, nguzo hazipatikani kwa mwenye nacho na asiyenacho.
Ilani ya CCM 2020-2025 hii ndio utekelezaji wake. Kalemani piga kazi. Wanaokuangusha ni Tanesco makao makuu, hamisha watumishi wa makao makuu peleka huko wilayani wakasimamie haya maelezo na chukua wengine huko wilayani peleka makao makuu uone ufanisi wao mkubwa.
 
Back
Top Bottom