Gharama za umeme: Rais Samia muwajibishe Waziri Kalemani na uongozi wote wa TANESCO

Gharama za umeme: Rais Samia muwajibishe Waziri Kalemani na uongozi wote wa TANESCO

Akili za kimasikini kabisa

Uganda umeme na maji uwa vinaunganishwa bure sio kwa tajiri wala masikini

Issue sio kuunganishiwa bure issue ni mapato yatakayopatikana kutokana na matumizi ya umeme

Tajiri atanunua umeme mwingi kwa haraka na kurudisha pesa yote iliyotumiwa na tanesco kumuunganishia umeme.

Masikin wengi wanatumia umeme wa elf 5 kwa mwezi

Hii imewekwa ili kuondoa urasimu wa kutokuwepo kwa bei inayoeleweka ya kuunganisha umeme.

Tanesco itakuwa na wateja wengi na mapato yatakuwa mengi kwa haraka

Tuache ujuaji na siasa uchwara za kuturudisha nyumba

Waziri yupo sahihi na kapewa maelekezo hawezi kuamua mwenyewe.

Labda kama wewe ni mfanyakazi wa Tanesco sawa.
 
Umeambiwa hii 27,000 ni kuunga single phase,
Less than 10% ya watanzania ndio wanajenga apartments, huoni hoja yako inataka kukatili asilimia zaidi ya 90 ya watanzania?
Sijahawahi kumpongeza kalemani Ila kwa hili ninampongeza. Kijijini mtu anafungiwa umeme kwa 27,000 matumizi yake kwa mwezi ni 4,000 Ila kwa mjini mtu atafungiwa umeme kwa 27,000 Ila matumizi yake kwa mwezi ni zaidi ya 60,000 Sasa mjini wakifunga umeme watumiaji mamilioni?
 
Matatizo na changamoto za Tanesco kwa wananchi ni mengi sana kuliko hilo nazani tungejikita zaidi kwenye hayo .

Matharani ; kukosekana na kukatika katika kwa huduma ya umeme kwa maeneo ambayo tayari yamefikiwa.

Halafu hawatoi fidia ya hasara ilosababishwa na Tanesco kwa kukatakata kwao umeme hovyo.
 
Hayo maamuzi sidhani kama yatakuwa ni yake pekee bali yatakuwa na baraka za baraza zima la mawaziri.
 
Sijahawahi kumpongeza kalemani Ila kwa hili ninampongeza. Kijijini mtu anafungiwa umeme kwa 27,000 matumizi yake kwa mwezi ni 4,000 Ila kwa mjini mtu atafungiwa umeme kwa 27,000 Ila matumizi yake kwa mwezi ni zaidi ya 60,000 Sasa mjini wakifunga umeme watumiaji mamilioni?
Yap, wateja wanaongezeka mapato yanaongezeka
 
Mfano lile tatizo la juzi la kukosekana kwa luku watu wamepata hasara kubwa sana lakini waTZ ni watu wakushangaza hakuna hata mmoja nilosikia ameenda kuishtaki Tanesco na kudai fidia ya hasara zilotokea sababu yao!

Uzembe utaendelea hadi wananchi watakapoanza kujitambua na kujua haki na wajibu wao na kuepuka kuzani ni hisani.
 
Halafu CAG hakukagua.

Na waziri kila siku anaenda kufanya kazi ya CEO hadi kusimamisha watu kazi
Hili shirika lishaishinda serikali.
Serikali ibadili sheria iondoe permanent jobs watu waajiriwe kwa mikataba mifupi mifupi ili akizingua atupwe mbali
 
Ninashauri tanesco Kila mkoa watengeneze kiwanda Cha kutengeneza nguzo ndogo na kubwa , za kuweka au kupitishia umeme kwa kutumia zenge na vyuma ili kukabiliana na upungufu wa nguzo pamoja na kupunguza gharama za maintaince kwa uharibifu wa nguzo
 
Tanesco wanashangaza sana eneo dogo ambalo limefikiwa na umeme uwezo wa kuwapa umeme wa uhakika throughout the year haupo lakini wanajinadi kutaka kuongeza wigo wa usambazaji wa huduma nchi nzima.

Mbona hili eneo dogo linawashinda kuwapatia huduma ya uhakika ya umeme throughout the year?

Halafu urasimu na yale mambo mengine Ndiyo usiseme.
 
HUYO ALOANDIKA AMEKATIWA NJIA ZA RUSHWA KWA MATAJIRI.
Ikiwa ghorofa 40 huoni atakuwa na matumizi makubwa na ndio faida.

Wewe tunajua ni mtumishi watanesco,KALEMANI UKIMPATA HUYO PELEKA KIHANZI AKAWE ANAHESABU MAJI YANAYOPOTEA.

MAKAO MAKUU WAMEKAA KIMAJUNGU,PELEKA TARAFANI HUKO
 
Nipo kwenye rekodi hapa ya kumtetea waziri Kalemani huko nyuma lakini Leo naomba Rais Samia amfukuze tena ikibidi haraka Sana huyu waziri..

Kwa mujibu wa maagizo aliyowapa Tanesco waziri Kalemani anataka sasa karibu watu wote Tanzania nzima wakitaka kuunganishiwa Umeme walipe Elfu 27 Tu ...bila kujali gharama halisi za kuvuta umeme Kwa mtu huyo ..anasema
Serikali imepitisha hela ya ruzuku Kwa Tanesco...

Sasa hebu twende taratibu huku tunatumia akili kidogo...
Mtu anajenga ghorofa lenye apartments 20...mfano Masaki huyu mtu sio masikini why asigharamie gharama halisi?

Why Tanesco ijinyime mapato Kwa kutoa ruzuku hadi Kwa matajiri wa Masaki Hadi Upanga?..

Anaejenga Fremu 20 mbeya mjini au Dodoma mjini?Why alipe elfu 27
Wakati Tanesco wananunua hizo Mita moja laki moja 20??..

Kwanza hii tafsiri yake ya Mjini kuwa ni Ilala City center kaitoa wapi?

Anajua maana ya Urban and Rural?
Anajua history ya kuanzisha REA?

Why anakuja kuleta siasa za kutafuta umaarufu Kwa nguvu Kwa gharama za kuiua Tanesco??..kama mpaka sasa Tanesco haipati Faida ..inaishi Kwa ruzuku
Why anakuja na maamuzi ya kupunguza mapato Kwa Tanesco?..

Mapato ya service charge yamefutwa
Mapato ya kulipisha fomu yamefutwa
Sasa hata gharama za kuvuta Umeme iwe Upanga au Masaki ziwe za REA kweli?

Huyu waziri anafanya siasa za hatari za kujifanya 'mtetezi wa wanyonge aliebaki'
Itasababisha Tanesco huko mbeleni ishindwe kujiendesha wala kulipisha wateja wake gharama halisi za Umeme ...

Anataka aonekane yeye alipokuwepo gharama zilishuka wakati si kweli
Gharama zipo zile zile anachofanya ni kutumia ruzuku ya serikali ambayo sio ya uhakika na haina guarantee ya kuwepo kila mwaka....

Tayari foleni ya umeme unaohitaji nguzo Tanesco inafika miezi sita sasa na bado waziri anaongeza tatizo badala ya kupunguza....

Utaratibu wa REA ulikuwepo kabla ya hata Kalemani hajawa waziri.... REA ibaki Rea Kwa wananchi wa vijijini na wenye vipaji vya chini...

Kulazimisha REA itumike nchi nzima ni siasa za kufeli na kuja kulaumiana huko mbele wakati huduma itakapokuwa ngumu kupatikana baada ya mapato kushuka...REA hadi Masaki na Sinza?
Wenye Bar na mafremu 40?
Wenye ghorofa zenye apartment 40?

Hi ruzuku ni pesa ambayo wananchi hasa masikini wanachangia ..why itumike kufaidisha Hadi matajiri Kwa siasa tu?


Viongozi wa Tanesco kuanzia Bodi Hadi CEO wake wote wapigwe chini Kwa kukubali maagizo haya ya huyu waziri...

Watu wenye uwezo walipie gharama halisi za umeme
REA ibaki vijijini na Kwa watu masikini..
Kazi ya TANESco ni kuunganisha umeme kwa wateja. Nao wanapata faida kutokana na kuuza umeme si kwa kuweka umeme
 
Bila shaka wewe utakuwa muuza solar.
Unataka gharama iwe kubwa watu washindwe kuvuta umeme wa tanesco hili uwauzie Solar zako.
Acha uchawi mkuu
mama Siti mwinyi na majenereta yake kipindi hiyo, mpaka mzigo wa kontena zake 40 zilipoisha ndio umeme wa uhakika ukarudishwa.
 
Nipo kwenye rekodi hapa ya kumtetea waziri Kalemani huko nyuma lakini leo naomba Rais Samia amfukuze tena ikibidi haraka Sana huyu waziri.

Kwa mujibu wa maagizo aliyowapa Tanesco waziri Kalemani anataka sasa karibu watu wote Tanzania nzima wakitaka kuunganishiwa Umeme walipe Elfu 27 tu bila kujali gharama halisi za kuvuta umeme kwa mtu huyo anasema Serikali imepitisha hela ya ruzuku kwa Tanesco.

Sasa hebu twende taratibu huku tunatumia akili kidogo. Mtu anajenga ghorofa lenye apartments 20. Mfano Masaki huyu mtu sio masikini why asigharamie gharama halisi?

Why Tanesco ijinyime mapato Kwa kutoa ruzuku hadi Kwa matajiri wa Masaki Hadi Upanga?

Anaejenga Fremu 20 Mbeya mjini au Dodoma mjini? Why alipe elfu 27 wakati Tanesco wananunua hizo Mita moja laki moja 20?

Kwanza hii tafsiri yake ya Mjini kuwa ni Ilala City Center kaitoa wapi?

Anajua maana ya Urban and Rural? Anajua history ya kuanzisha REA?

Why anakuja kuleta siasa za kutafuta umaarufu Kwa nguvu Kwa gharama za kuiua Tanesco??..kama mpaka sasa Tanesco haipati Faida inaishi kwa ruzuku. Why anakuja na maamuzi ya kupunguza mapato kwa Tanesco?

Mapato ya service charge yamefutwa. Mapato ya kulipisha fomu yamefutwa. Sasa hata gharama za kuvuta Umeme iwe Upanga au Masaki ziwe za REA kweli?

Huyu waziri anafanya siasa za hatari za kujifanya 'mtetezi wa wanyonge aliebaki'. Itasababisha Tanesco huko mbeleni ishindwe kujiendesha wala kulipisha wateja wake gharama halisi za Umeme.

Anataka aonekane yeye alipokuwepo gharama zilishuka wakati si kweli.

Gharama zipo zile zile anachofanya ni kutumia ruzuku ya serikali ambayo sio ya uhakika na haina guarantee ya kuwepo kila mwaka.

Tayari foleni ya umeme unaohitaji nguzo Tanesco inafika miezi sita sasa na bado waziri anaongeza tatizo badala ya kupunguza.

Utaratibu wa REA ulikuwepo kabla ya hata Kalemani hajawa waziri. REA ibaki REA kwa wananchi wa vijijini na wenye vipaji vya chini.

Kulazimisha REA itumike nchi nzima ni siasa za kufeli na kuja kulaumiana huko mbele wakati huduma itakapokuwa ngumu kupatikana baada ya mapato kushuka REA hadi Masaki na Sinza?

Wenye Bar na mafremu 40?

Wenye ghorofa zenye apartment 40?

Hi ruzuku ni pesa ambayo wananchi hasa masikini wanachangia. Why itumike kufaidisha hadi matajiri kwa siasa tu?

Viongozi wa Tanesco kuanzia Bodi hadi CEO wake wote wapigwe chini kwa kukubali maagizo haya ya huyu waziri...

Watu wenye uwezo walipie gharama halisi za umeme.

REA ibaki vijijini na kwa watu masikini.
Ila watanzania tuna akili za kipekee sana.

Siku zote masuluhisho yetu ni Rais fukuza huyu, Rais fukuza yule .......

Anyway, Ukifuatilia kisa cha Rockafeller yule bilionea wa Marekani utajua kuwa wakati anaanzisha biashara ya mafuta alipata changamoto kubwa kutokana na watu kutokuwa na taa ( chemney )

Akichokifanya ni kugawa chemney bure ili watu wanunue mafuta.

Hata SIM CARD za simu siku hizi kupewa bure ni kitu cha kawaida.

TANESCO inatoa huduma ambayo inalipiwa mara kwa mara, hata wakisema waunganishe umeme bure mimi sioni kama watapata hasara yoyote kutokana na wingi wa wateja watakaokuwa nao.
 
Ninashauri tanesco Kila mkoa watengeneze kiwanda Cha kutengeneza nguzo ndogo na kubwa , za kuweka au kupitishia umeme kwa kutumia zenge na vyuma ili kukabiliana na upungufu wa nguzo pamoja na kupunguza gharama za maintaince kwa uharibifu wa nguzo
Kuna mwaka niliona wanazindua kiwanda cha nguzo cha bilioni 30. Sasa imagine kila mkoa ukijenga kiwanda cha bilioni 10 tutafika kweli
 
Mkuu ulipaswa kutueleza ni kiasi gani cha Fedha Tanesco inakusanya kutokana na Ankara za matumizi ya umeme ili tuone mapungufu.
Vinginevyo, Tanesco wanauza umeme, wao ndiyo wenye dhamana ya kuweka miundombinu ya kumfikia mteja wao.
Hata hiyo alfu 27 ifutwe.

Haiwezekani mtumiaji awasaidie kuweka miundombinu ambayo inawasaidia wao wenyewe kukusanyia bili.
Kama Shirika hilo linapata upungufu, mmiliki ambaye ni serikali atafute njia nyingine badala ya kutujazia gharama za kuunganisha umeme.
 
Back
Top Bottom