Mkuu Maji ,umeme ,barabara ni huduma za jamii ,hizo kwa nchi ambazo zinajielewa ilitakiwa zitolewe bure (maji+umeme kwenye kuunganisha) iwe inalipiwa kwenye matumizi tu.
Sikubaliani na wewe kwa 100% , Serikali inakusanya kodi nyingi sana sema zinatumika ndivyo sivyo,nyingi zinaishia kwa wala rushwa serikalini ,unamnunuliaje RC/DED/DAS.RAS etc Ma Viete ya milioni 400 wakati wanafunzi wanasoma chini ya miti?
Mimi napendekeza kabisa tena zifutwe kabisa hata hiyo 27k waunganishe bure,Maji siku hizi wanaunganisha kwa mkopo ,mkuu hiyo laki 3 au laki 5 gharama sio wote wanaweza mkuu ,hata kama wewe una kipato kizuri huko marekani ,jaribu kufikiria hawa wanaijibanabana kujenga vyuma vya polisi post waweze kujistiri.
Kama ni kweli wameweka flat rate kwa watu wa single phase kuunganishwa kwa 27k basi nampongeza sana waziri,tambua kwamba hao wa vijijini wanaounganishwa kwa elfu 27 nao wana mafremu na maghorofa vile vile na vile vile hapa town kuna watu wana vyumba viwili vya paa moja lakini wanaounganishwa kwa laki 3 ,sioni mantiki yako!!
Pia tambua REA watu wote wanachangia pindi ukinunua umeme na kwanini wabague wa mjini wakati tunachangia wote? Halafu vijiji karibia vyote viashaunganishwa na umeme ,je unataka kutuambia kwamba sasa tusichangie tena REA? Hizo fedha za REA ndio zinapunguza unafuu kwa watu wote.