Gharama zinazotozwa Muhimbili Hospital kuwahudumia “Watoto njiti” zinatuumiza tunaouguza

Licha ya Mamlaka za Kiserikali pamoja na Wadau kueleza mipango mikakati na kuchukua hatua mbalimbali za kupunguza vifo vya Mama na Mtoto hasa vinavyotokana na Watoto Njiti (Watoto waliozaliwa kabla ya muda) lakini hali inaonekana kuwa sio shwari katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Ambapo kwa siku za hivi karibuni kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa baadhi ya Wazazi ambao wamejifungua Watoto Njiti kutozwa gharama kubwa hali ambayo inatufanya wengine kulazimika kuweka bondi ya mali zetu au kukopa ili kupata fedha za kulipia kupata watoto.

Baadhi ya sisi wazazi ambao tumekumbana na changamoto hiyo kwa kukaa Hospitalini kwa muda wa wiki moja hadi mbili tumekuwa tukitakiwa kulipa kati ya Shilingi Milioni 2 hadi 6.

Hali hii inasababisha baadhi ya Wazazi hasa wenye hali duni Kiuchumi kulazimika kuweka bondi ya mali au vitu vya thamani kwa lengo la kupata fedha ili matibabu yakiisha tuweze kuruhusiwa hospitalini.

Hali hii imeongeza maumivu kwa baadhi ya wazazi huku wengine wakifikia hatua ya kutaka kutelekeza Watoto hao hospitalini kutokana na gharama kuwa kubwa.

Matukio mawili ya hivi karibuni, wapo wazazi waliambiwa kama wanataka kuchukua Watoto wao watoe Shilingi Milioni 5 lakini baada ya Wazazi hao kudai kuwa hizo ni pesa nyingi kwao ndipo waliambiwa watoe Shilingi Milioni 3, kinyume na hivyo wakaambiwa hawezi kupewa Watoto, hali ambayo imewalazimu nao kuuza na kuweka bondi baadhi ya mali ili kupata fedha hiyo.

Nimelazimika kuandika hapa baada ya kuona wenzangu yamewakuta wakiwa hawana uwezo wa kulipia gharama hizo.

Nitoe wito kwa Wizara ya Afya pamoja na mamlaka nyingine za Kiserikali kufuatilia kwa ukaribu suala hili kwa sababu limekuwa kilio kwa wengi.

Kulingana na hali ya maisha gharama hizo ni kubwa, sio rahisi Wananchi hasa wenye kipato duni kuzimudu hali ambayo binafsi nahofia kuna wakati baadhi ya wazazi wanaweza kushindwa kuzimudu na uenda wakati mwingine ikawa inapelekea changamoto ya kutohudumiwa ipasavyo kwa wakati na kusababisha vifo kwa watoto njiti jambo ambalo tungeweza kuliepuka kwa kuweka gharama au utaratibu rafiki kwa wahusika.

Kama endapo huduma za kuwahudumia Watoto Njiti ni ghali sana basi mamlaka ziongeze uwekezaji katika eneo hilo kwa lengo la kusaidia wazazi wanaojifungua watoto njiti ili kuepuka makali ya gharama ambayo yanafanya baadhi wafikie hatua ya kuuza mali ambazo pengine zingewasaidia katika kugharamikia matunzo ya watoto hao.

Nilipouliza wanadai Mashine zinazotumiwa na Watoto hao wanaozaliwa kwamba zipo chache na zina gharama kubwa katika uendeshaji wake, kama ni hivyo, basi naomba Serikali iingilie kati kujua namna ya kutusaidia Wananchi wake wenye kipato cha kawaida.

Pia soma
~
Watoto njiti zaidi ya laki mbili Nchini huzaliwa kwa mwaka
~ Serikali na Mkakati wa Kupunguza Vifo Vya Watoto Njiti Nchini
KUZALISHA kwa usalama hilo ni jukumu la Serikali
ILA
Malezi ya MTOTO hilo ni jukumu laki
 
Furahia uliyebarikiwa wewe, anzisha nyuzi yakwo uyaandike haya.
Hapa ndipo mnaposhindwa.

Badala ya kujadili hoja mnajadili mtoa hoja.

Mimi nimeleta hoja dhahania, ila wewe umeshindwa kuona hoja unaona mtoa hoja tu.

Na wala sijasema nimebarikiwa, sijui umetoa wapi hilo.

Na sina haja ya kuanzisha uzi, uzi tayari upo huu. Usinifanyie censorship kwa sababu hupendi hoja zangu tu.

Kama unaweza kuzijibu, zijibu hoja.

Usinifunge mdomo nisitoe hoja zangu ninavyopenda mimi.

Tatizo watu wanapenda kuzaa bila mpango. Wanazaa kama bahati nasibu tu. Wanazaa kwa kusema "kila mtoto anakuja na riziki yake". This is the problem.

Uzazi wa mpango kama zero vile.

Of course mkizaliana kibahatibahati kwa mashindano kama sungura lazima mfumo wa public health support system u fail na gharama ziwe juu sana.

Hamna insurance scheme ya kueleweka, hamna tax base ya kueleweka, hamna exports za kueleweka, mnazaa sana bila mpango.

Mtatoboa vipi hapo?

Lazima pawe na kizungumkuti.

Huo ndio ukweli wa mambo. Penda usipende.

Usinilaumu mimi, sijapanga hivyo mimi.

Mimi ni mjumbe nakuambia ukweli tu.
 
Yaani Umepata HASIRA kwa maisha yasiyokuhusu, mwenye pesa wewe unayewezs kuzaa muda wowote. Sasa sepa kafungue uzi wako, acha yanaowahusu walalamikie wanayotaka. Haujalazimishea kuandika yako kwa uzi wa mwingine na wewe hata haujapitia haya.
Sijapata hasira, nimeweka hoja za kidhahania tu.

Ila wewe kwa sababu ni guluguja huna ubongo wala uti wa mgongo unaona hoja za kidhahania ni hasira.

Huna uwezo wa kuelewa hoja za kifalsafa na kidhahania.
 
Aisee manoendelea kukuza familia Mungu awafanyie wepesi, mambo yamekua mengi.....
Nashukuru kuvuka hicho kikombe cha kutafuta uzazi na kujifungua bila changamoto salama
 
IVF ni gharama duniani kote..... ila swala la watoto njiti serikali inaweza kufanya jambo
Rais Samia hivi karibuni kalalamika kasi ya kuzaana Tanzania iko juu sana, serikali inaelemewa kutoa huduma za jamii.

Soma hapa kwa habari zaidi

Watanzania tunaongezeka kwa asilimia takriban 3 kila mwaka.

This is a ticking timebomb.

Kwa kasi ya kuzaliana ya sasa, kila miaka 24 idadi ya Watanzania inazidi mara mbili.

Yani kufikia mwaka 2048 tutakuwa tushafika zaidi ya watu milioni 130 kutoka idadi ya sasa ya kadiri watu milioni 65.

Hapo hapo mfumo wa huduma bora za afya ya jamii unategemea sana pesa za walipa kodi, Tanzania tax base ni ndogo, uchumi mdogo. Watu wengi effectively ni kama hawalipi kodi kabisa.

Na hawa masikini ndio wanaozaliana sana. Kuna mikoa wastani wa kuzaa ni watoto 7. Ina maana kuna familia mpaka leo zina watoto zaidi ya 10.

Sasa uchumi mdogo, kodi inayokusanywa ndogo, demands kwenye public health system kubwa, serikali itatoa wapi funds za kuweka resources katika hali kama hii?

Serikali yenyewe viongozi ndio hawa vipaumbele vyao ma VX.

Wananchi wenyewe ndio hawa hawana utamaduni wa kufikiri kwa kina na kuweka mipango endelevu.

Kila mtu anashindana kuzaa kwa style ya "kila mtoto anakuja na riziki yake".

Hapo lazima gharama zipande tu. Hakuna jinsi.

This is a natural reponse of an overwhelmed system that is choking from unplanned usage.
 
Hapa ndipo mnaposhindwa.

Badala ya kujadili hoja mnajadili mtoa hoja.

Mimi nimeleta hoja dhahania, ila wewe umeshindwa kuona hoja unaona mtoa hoja tu.

Na wala sijasema nimebarikiwa, sijui umetoa wapi hilo.

Na sina haja ya kuanzisha uzi, uzi tayari upo huu. Usinifanyie censorship kwa sababu hupendi hoja zangu tu.

Kama unaweza kuzijibu, zijibu hoja.

Usinifunge mdomo nisitoe hoja zangu ninavyopenda mimi.

Tatizo watu wanapenda kuzaa bila mpango. Wanazaa kama bahati nasibu tu. Wanazaa kwa kusema "kila mtoto anakuja na riziki yake". This is the problem.

Uzazi wa mpango kama zero vile.

Of course mkizaliana kibahatibahati kwa mashindano kama sungura lazima mfumo wa public health support system u fail na gharama ziwe juu sana.

Hamna insurance scheme ya kueleweka, hamna tax base ya kueleweka, hamna exports za kueleweka, mnazaa sana bila mpango.

Mtatoboa vipi hapo?

Lazima pawe na kizungumkuti.

Huo ndio ukweli wa mambo. Penda usipende.

Usinilaumu mimi, sijapanga hivyo mimi.

Mimi ni mjumbe nakuambia ukweli tu.

Haya yote kwa nini haukuandika mwanza!!! nasema tena acha watu na yao nchini. Unafikiri sijui kusoma maana yako nje ya BOKSI..!!!!
 
Sijapata hasira, nimeweka hoja za kidhahania tu.

Ila wewe kwa sababu ni guluguja huna ubongo wala uti wa mgongo unaona hoja za kidhahania ni hasira.

Huna uwezo wa kuelewa hoja za kifalsafa na kidhahania.

Maneno yako hayo ona sasa ulivyo.. Uzi wanaoyaishi wanaandika yao wewe unakuja na yako.. Ungeupita uzi huu ungepungukiwa nini? Umeandika nakusema wewe.. 😅😅😅😅 Umeshindwa una anza kuniita yale yote unajua wewe.. Ukweli nimekupa acha HASIRA kwa maisha ya watu. Waandike wazaliane wawe na pesa hawana wewe inakuuma nini. Umejaa HASIRA kwa issue hata unadai wa pesa haikuhusu..

Umeandika maneno machafu mie najua umejiongelea sijui ikoje eeeh umeyajuaje kama wewe haupo hivyo... 😅😅🤣🤣🤣🤣 Wa pesa weye.. Leo wasio nazo wanakutoa pangoni..
 
Wewe guluguja huna ubongo wala uti wa mgongo, huwezi kunielewa.

Sishangai kwamba hunielewi, nitashangaa ikitokea ukanielewa.

Na hapa nakupeleka ignore list sitaona tena unachoandika kuanxia hapa.

Na nitaandika popote ninapotaka hunifanyi kitu.
 
Unapopanga kuzaa mtoto unatakiwa ujue mtoto anaweza kutokea njiti na unatakiwa uwe na mpango wa kumhudumia akiwa njiti.

Usipoweza, usizae.

Ukizaa mtoto halafu akawa njiti halafu huwezi kumhudumia, umemleta mtoto duniani bila kuweza kumhudumia.

Ni bora usingemleta kabisa.
Maisha ya watanzania wengi hasa waliojibana huko dar ni magumu sana,je waache kuzaa kwa k
Sababu ya maisha yao?
Mi naona serikali ingetenga fungu angalau wawaboost.
 
Serikali itenge fungu kutoka wapi wakati imeelemewa na mambo mengi, watu hawalipi kodi, uchumi mbovu.

Hivi mnafikiri serikali inatenga fungu kwa mazingaombwe?
 
Licha ya Mamlaka za Kiserikali pamoja na Wadau kueleza mipango mikakati na kuchukua hatua mbalimbali za kupunguza vifo vya Mama na Mtoto hasa vinavyotokana na Watoto Njiti (Watoto waliozaliwa kabla ya muda) lakini hali inaonekana kuwa sio shwari katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Ambapo kwa siku za hivi karibuni kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa baadhi ya Wazazi ambao wamejifungua Watoto Njiti kutozwa gharama kubwa hali ambayo inatufanya wengine kulazimika kuweka bondi ya mali zetu au kukopa ili kupata fedha za kulipia kupata watoto.

Baadhi ya sisi wazazi ambao tumekumbana na changamoto hiyo kwa kukaa Hospitalini kwa muda wa wiki moja hadi mbili tumekuwa tukitakiwa kulipa kati ya Shilingi Milioni 2 hadi 6.

Hali hii inasababisha baadhi ya Wazazi hasa wenye hali duni Kiuchumi kulazimika kuweka bondi ya mali au vitu vya thamani kwa lengo la kupata fedha ili matibabu yakiisha tuweze kuruhusiwa hospitalini.

Hali hii imeongeza maumivu kwa baadhi ya wazazi huku wengine wakifikia hatua ya kutaka kutelekeza Watoto hao hospitalini kutokana na gharama kuwa kubwa.

Matukio mawili ya hivi karibuni, wapo wazazi waliambiwa kama wanataka kuchukua Watoto wao watoe Shilingi Milioni 5 lakini baada ya Wazazi hao kudai kuwa hizo ni pesa nyingi kwao ndipo waliambiwa watoe Shilingi Milioni 3, kinyume na hivyo wakaambiwa hawezi kupewa Watoto, hali ambayo imewalazimu nao kuuza na kuweka bondi baadhi ya mali ili kupata fedha hiyo.

Nimelazimika kuandika hapa baada ya kuona wenzangu yamewakuta wakiwa hawana uwezo wa kulipia gharama hizo.

Nitoe wito kwa Wizara ya Afya pamoja na mamlaka nyingine za Kiserikali kufuatilia kwa ukaribu suala hili kwa sababu limekuwa kilio kwa wengi.

Kulingana na hali ya maisha gharama hizo ni kubwa, sio rahisi Wananchi hasa wenye kipato duni kuzimudu hali ambayo binafsi nahofia kuna wakati baadhi ya wazazi wanaweza kushindwa kuzimudu na uenda wakati mwingine ikawa inapelekea changamoto ya kutohudumiwa ipasavyo kwa wakati na kusababisha vifo kwa watoto njiti jambo ambalo tungeweza kuliepuka kwa kuweka gharama au utaratibu rafiki kwa wahusika.

Kama endapo huduma za kuwahudumia Watoto Njiti ni ghali sana basi mamlaka ziongeze uwekezaji katika eneo hilo kwa lengo la kusaidia wazazi wanaojifungua watoto njiti ili kuepuka makali ya gharama ambayo yanafanya baadhi wafikie hatua ya kuuza mali ambazo pengine zingewasaidia katika kugharamikia matunzo ya watoto hao.

Nilipouliza wanadai Mashine zinazotumiwa na Watoto hao wanaozaliwa kwamba zipo chache na zina gharama kubwa katika uendeshaji wake, kama ni hivyo, basi naomba Serikali iingilie kati kujua namna ya kutusaidia Wananchi wake wenye kipato cha kawaida.

Pia soma
~
Watoto njiti zaidi ya laki mbili Nchini huzaliwa kwa mwaka
~ Serikali na Mkakati wa Kupunguza Vifo Vya Watoto Njiti Nchini
Hizo ni gharama zinafukuzana karibu kqbisa na za Agakhani.m6 kwa wiki mbili tena kwa mtoto.au mimi sijaelewa
 
Rais Samia hivi karibuni kalalamika kasi ya kuzaana Tanzania iko juu sana, serikali inaelemewa kutoa huduma za jamii.

Soma hapa kwa habari zaidi

Watanzania tunaongezeka kwa asilimia takriban 3 kila mwaka.

This is a ticking timebomb.

Kwa kasi ya kuzaliana ya sasa, kila miaka 24 idadi ya Watanzania inazidi mara mbili.

Yani kufikia mwaka 2048 tutakuwa tushafika zaidi ya watu milioni 130 kutoka idadi ya sasa ya kadiri watu milioni 65.

Hapo hapo mfumo wa huduma bora za afya ya jamii unategemea sana pesa za walipa kodi, Tanzania tax base ni ndogo, uchumi mdogo. Watu wengi effectively ni kama hawalipi kodi kabisa.

Na hawa masikini ndio wanaozaliana sana. Kuna mikoa wastani wa kuzaa ni watoto 7. Ina maana kuna familia mpaka leo zina watoto zaidi ya 10.

Sasa uchumi mdogo, kodi inayokusanywa ndogo, demands kwenye public health system kubwa, serikali itatoa wapi funds za kuweka resources katika hali kama hii?

Serikali yenyewe viongozi ndio hawa vipaumbele vyao ma VX.

Wananchi wenyewe ndio hawa hawana utamaduni wa kufikiri kwa kina na kuweka mipango endelevu.

Kila mtu anashindana kuzaa kwa style ya "kila mtoto anakuja na riziki yake".

Hapo lazima gharama zipande tu. Hakuna jinsi.

This is a natural reponse of an overwhelmed system that is choking from unplanned usage.
Aanze na ndugu zake wa kuoa wake wengi na kuzaa kama kitimoto. Awapige marufuku hao
 
Kaongea na nchi nzima kwa hivyo na wao wamo.
Kwa kauli hiyo hana tofauti na mtu ambaye atamwambia mwenye njaa, "haya na ukashibe". Ni sawa na kusema, "acheni madawa ya kulevya. Yana madhara"
 
Back
Top Bottom