Hapa ndipo kuna pointi ukiiweka kiuchanya.
Ngoja nianze kwanza kwa kuwapa pole wote wanaokumbana na shida hiyo ya ghafla. Mungu awasaidie na kuwatia nguvu.
Unaonaje suala la, badala ya kuwalazimisha wananchi wote wakate bima. Basi kuwe hata na bima ya makundi maalumu mfano. BIMA YA UZAZI tu wakate wote wenye mpango wa kujifungua miezi mitano ijayo?
Tuliona jinsi bima ya watoto ilivyofanikiwa, labda watanzania tunataka bima hizo. Watu wasaidiwe kupitia bima serikali ijitahidi kuongezea ruzuku huko lakini sio kiholela?
Kivyovyote vile ni lazima tuchangie gharama ya kuwasaidia watoto njiti. Muhusika na jamii (serikali na ndugu) ili kuwe na uwajibikaji pande zote. RESPONSIBILITY. Hili halikwepeki.
Aione pia
cocochanel 3 Angels message jerryempire na wengineo. Poleni sana tutafute sasa njia inayoweza kuwa suluhisho linalowezekanika.
Katika hili itabidi tutumie akili ya
Kiranga yeye (strategy yake) analimudu vizuri kwa sababu kiimani anakubali dunia ipo hivyo ni fujo, lolote laweza kutokea (chaos) na ameonelea ni muhimu KILA MMOJA kuweka mipango yake kwa namna hiyo. Ni wazo zuri sana hili katika kukabili majanga. Kuhamishia gharama serikalini kwanza kimsingi ni kurudisha gharama kwa wananchi wenyewe maana serikali ni watu.
Ni lazima tunyumbulike, tuishi kama vile tunapanga kila kitu (we make things happen)..... na wakati huohuo mahala fulani tujipange kama vile mambo yanalipuka tu (shit happens).
Ninapotetea kujipanga simaanishi kila mmoja aweke milioni kumi (10M+) kwa ajili ya uzazi tu!!. Lakini mipango ipo mingi tu, mfano hilo la kutumia bima kuwalipa wao kuibeba hiyo hatari. Naamini gharama ya kulipa mtu binafsi haiwezi fika milioni hizo. Huu mpango utawasaidia watu wenye nia moja WAZAZI