Ghetto Qura'n na kisa cha 50 Cent kupigwa risasi..

Huyu Jamaa 50Cents "Curtis Jackson" ni mtu mwenye gubu na Wivu sana.

Pia 50Cents ana chuki na wasanii mbalimbali akiwemo Diddy "Sean Combs".

In short ni ngumu kwa yeye kuweza kua karibu na Diddy. Kama ambavyo ma GOAT wengine wakina JayZ, Ricky Roose, Dj khaleed, Nas, Snoop wanavyoonyesha Love kwa pamoja.

Maywether ana IQ kubwa katika maisha na anamuelewa sana.

50 Cents kwenye Bifu lake na Jefrey Artkins "Jarule" ilimsaidia sana kua Maarufu duniani.

Pia 50 Cents anaamini sana kupanda chati kwake kunategemea zaidi kiki na bifu.

Ndio maana amewekeza ubongo wake huko kuliko kitu kingine. Mpaka anaonekana kama ana akili ya kitineja wakati ni jitu zima linalo zeeka.

50Centa amewahi kushawishiwa na watu wengi sana, kupunguza lugha ya matusi kwenye Nyimbo zake. Akakataa na kulinganisha kitendo hiko ni sawa na kuondoa mstari Mwekundu kwenye bendera ya Marekani.

Alipigwa marufuku kukomunika na kanisa na pia marufuku kuvaa misalaba shingoni na Askofu wa kanisa katoliki kwasababu ya kuvaa kwenye miziki iliojaa matusi na tabia za kishetani.

Stori ya kupigwa risasi 9 inabaki kua ya kusadikika. Manake wakati inatumiwa kama kiki ya kumtoa kwenye moja ya Albamu yake miaka ile ya 2000s, ma Sherifs Nchini Marekani walianzisha uchunguzi kuhusu tukio hilo, manake walikua hawaijui.

Bifu lake la kulazimisha penzi kwa Olivia lilipelekea kumshusha sana. 50cents ni mtu anayeongea vibayavibaya. Hana Class.

Kwa sasa jama amefilisika. Na alishatangaza kufilisika. Hana tena Pesa ya kumpa Kibri.
Anajaribu tasnia ya Filamu. Na filamu pekee iliommulika vizuri itakua ni 14.

Kikundi chake cha G unit ndo hivyo tena kimeshapitwa na wakati.

Mtu anayeweza kua fascinated na 50 Cents atakua ni Immature. Anapenda mikwara ya kitoto na ya kimuvimuvi na kisinema zile za bolo young na Van dame.

But kwa wenye akili iliyokomaa hawawezi kubaliana na huyu mtu. Lyrically 50cents sio GoAt kabisa.
 
Ain't eat this layer

50 hajawahi kulazimisha penzi kwa Olivia

They were just best friends
 
Fifty ni moja kati ya wanamziki watata USA .......Hata ukiangalia anavyowazinguaga manguli akina P. Diddy na Jay z .........Jamaa huwa anawachana makavu.......Kuna video clip moja aliwachana wote wawili kuwa wameuza roho zao kwa Shetani (Lucifer) na kusema kuwa. hata tungo zao ziko kishetani shetani. tu .......
 
Wakati Beef la 50 na Fat Joe limefika pabaya,Fat Joe akaongea na vyombo vya habari anamuomba 50 beef liwe kwenye nyimbo Tu wasije wakataftana mtaani coz anajua Curtis mtu WA aina Gani..FIF,FERRARI..daah mmenikumbusha years ago

huu ni uongo uliotukuka!!
 
Wakati 50 anajaribu kubreak the mainstream kuna beats kibao maproducer walikuwa nazo hazina watu wa kuzitumia unaambiwa wasanii walikua hawawezi zitumia lakini 50 akiingia booth ana rap kama kazitengeneza yeye!

Hivi unajua beat la 'In Da Club' lilitengenezwa kwa ajiri ya kundi la D12 lakini wakashindwa litumia ikabidi 50 apewe, akaua na matokeo ya hiyo nyimbo fatilia.

Hivi unajua beat ya gharama zaidi miaka hiyo ilikua Candy shop by Scott scorch!?.

Unajua unaposema ana chuki kisa hana mafanikio unashangaza. unajua 50 ndio msanii wa kwanza duniani kuingiza nyimbo 3 top 5 Billboard ndani ya wiki ya kwanza "Candy Shop, Disco Inferno na How We Do."

50 hana chuki isipokuwa mazingira aliyokulia ya beef sana na kama hujui beef la Jah rule na 50 moja ya sababu ni kuwa 50 alikuja kumshusha popularity Jah rule!.

Lile Jengo zima la Mike tyson 50 alilinunua kwa nyimbo ya 'In da Club' pekee.

Unajua Mobb Deep waliwahi kumilikiwa na 50 kwenye G-Unit na jamaa akawapa wote magari ya Porsche (Prodigy na Havoc).

Tony Yayo, Busta Rhymes na Rakim walipewa beat ya Heat wakashindwa kuiimbia, 50 akapewa akaua unasemaje jamaa ni kick.

Unajua jamaa ana BET, Billboards, Grammy Awards na Tuzo nyingne ngapi!?. au mafanikio kwako ni yapi!?.

Unajua 50 aliwahi fika hadi top 5 ya wasanii matajiri zaidi duniani? mafanikio yapi ya kick hapo au forbes nao wanahesabu hadi kick?.

Kifupi kila kitu kina downfall kipindi cha 50 Cent kimepita kama kilivyo kipindi cha Jigga, Nas, Lil wayne na wengine.

Eti wewe ndio wa kusema 50 hakupigwa risasi 9 really!?.. Ina maana unapingana na ripoti za NYPD?.

Umeongea pumba sana!!..rudi research
 
Aliwasaini hata M.O.P Billy Danze & Lil Fame
 
Aliwasaini hata M.O.P Billy Danze & Lil Fame
sasa huyu jamaa anakuja anasema 50 hana mafanikio kwa style ipi sijui!..
Me sina ushabiki na wasanii nakubali mafanikio yao wote na 50 Cent alileta ushindani sana kwenye muziki kipindi chake!!..
 
Duuuuhhhhh,noma sana...huwa kuna movie fulani ya 50 Cent siifaham kwa jina lkn ndani yake huwa kuna mauaji sana na matumizi ya madawa wa kulevya,kama unaifaham kwa jina naomba unifahamishe!
Get rich or die rich
 
Mbona umewekeza sana kumuelewa mwanaume mwenzako???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…